Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,726
Juma hili linalomalizika, serikali ya Uganda Chini ya Rais Museveni imepata wakati mgumu mbele ya mabunge mawili - Bunge la Uingereza na Bunge la Ulaya.
Vyombo vya habari na mitandao imeonyesha mijadala motomoto ikiishutumu serikali ya Uganda kwa yafuatayo:
-Kukiuka haki za binadamu
-Kuwakamata na kuwatesa wapinzani
-Kuzuia uhuru wa kujieleza, kukusanyika na kutoa maoni
-Kutumia bunge vibaya kwa kutunga sheria zinazopingana na katiba
-Kutesa, kuua na kufanya ukatili
Hitimisho lao likawa ni:
-Uganda iko chini ya mfumo wa kidikteta rasmi
-Hali hiyo haikubaliki na jumuia ya kimataifa
-Wito wa kuiondoa madarakani kwa njia zozote.
Sipendi nchi za Magharibi kuingilia uhuru wa nchi za Kiafrika, lakini sipendi zaidi viongozi wa nchi za kiafrika kuwatesa watu hao kuliko walivyoteswa na wakoloni. Tanzania tumejifunza nini?
Kwanza nikiri wazi, yanayosemwa kutendwa na serikali ya Uganda kwa wananchi wa Uganda, hayafikii nusu ya yale tunayotendewa na serikali yetu hapa Tanzania. Mbunge Lusinde ameyaanika vizuri katika kampeini za Monduli na Ukonga. Hatuhitaji ushahidi kuonyesha kuwa serikali inaliendesha bunge; inatesa wapinzani, inaua wapinzani, na kusimamia ukiukwaji wa haki za binadamu. Hayakusemwa na wapinzani, yamesemwa na Mbunge wa CCM akiwatumia Spika, waziri Mkuu na mawaziri kama mashahidi wake.
Kinachoonekana kukosekana Tanzania ni utashi wa wanasheria wetu kuyapeleka haya katika vyombo vya kimataifa ili yafahamike. Vyama vya upinzani, wana harakati, na media zetu, ama hawana uwezo, au hawana utashi na uthubutu wa kuyafanya waliyofanya watu wa Uganda. Kuna tweet inazunguka kwenye mitandao kuwa Washington imemfutia visa Museveni na mawaziri wake, na kijana wake anayesoma hapa anarudishwa Kampala. Sipendi haya yatufike. Nimemsikia balozi wetu mmoja wa nchi za Magharibi akisema "wamechoka" kutetea mambo yasiyokuwa na msingi!