Kambi ya Upinzani Bungeni kusoma bajeti Jumatatu, CCM waja na mkakati wao wa mchanga

Mkuu Nemesis,upinzani mara nyingi huwa wanacheza muziki wa maCCM tena kwa tone ya maCCM. Uahauri wako ni wa maana sana kama ukitekelezwa. Wao wajikite kwenye issues zinazomgusa mwananchi wa kawaida na si makelele yasio na mashiko. Upinzani wakiacha "retaliations" za mapovu dhidi ya maCCM,wakaja na hoja za msingi,wananchi watawaelewa,na serikali ya maCCm pia itayafanyia kazi japokuwa huwa ni kwa mlango wa nyuma na kimyakimya ili upinzani usipate credits.
Exactly
 
Nakumbuka tamko la kutoza kodi (18%) kwenye miamala yote ya fedha bajeti ya mwaka 2016/2017. Mlipotosha kadili ilivyowezekana lakini muda umewaumbua. Na hii pia ya 2017/2018 najua mtakuja na tafsiri zenu lakini muda utasema pia
 
Wakuu..Jumatatu ni siku ya Bajeti mbadala ya Wizara ya fedha hivyo tunapaswa kujiandaa kuisambaza Bajeti hiyo na kuleta utofauti na Ile ya kwao ya mbwembwe nyingi ambayo kiuhalisia haina utekelezaji.

Kutokana na kujua ya kwamba Bajeti yetu mbadala itawavua nguo wameamua kuja na mkakati wao Mwingine ili kutuhamisha kwenye Bajeti Mbadala yenye kuzingatia uhalisia wa Wananchi wengi.

Tunapaswa kujua tusiruhusu mjadala watakao uanzisha ili kutaka kunyamazisha Bajeti yetu Mbadala ya Wizara ya fedha.... Tunapaswa kuitumia siku ya jumatatu kwaajili ya Bajeti yetu mbadala na siyo propaganda nyingine kama ambavyo bango lao linapita likitaka kuwachota watu macho na masikio yasihamie kwao bali yabaki kwenye Bajeti yetu mbadala ya kuwasaidia Wananchi.

Tumewaacha muda mrefu na propaganda zao,zimewapati sifa ambazo hawasitahili kuzipata hata kidogo.

Kwasasa tunapaswa kuwaonyesha kuwa tuliamua kuwapuuza na kwakuwa wanaendelea kudanganya basi wakiweka mkono tunaweka mguu yaani Bampa 2 Bampa mpaka kieleweke.

Tunapaswa kujua ya kwamba tumaini pekee kwa sasa kwa Wananchi ni sisi pekee... Tusiwaangushe Wananchi wetu.....
Hiyo takataka inatekelezwa na serikali gani? budget ilisha somwa ijumaa zingine ni kelele tuu na kudandia ya wenzenu
 
Habari njema hiyo though hata kama ingekuwa anasoma mpango ni ngumu kuacha kumsikiliza JPM akisema masaju ,lionchawene ,Chenge, Ngeleja et al waende wenyewe segerea JPM hatabiriki yule
 
Upuuzi mtupu. Bajeti ya nchi keshasoma Dk mpango . Ninachojua jumatatu ni mhe rais anapokea ripoti ya pili saa tatu asubuhi. over

Upi ni upuuzi kupanga Bajeti kuubwa usiyo weza kuitekeleza hata kwa 35% ?..
 
Siku tatu mnapiga tuition baada ya Dr Mpango kuwapiga butwaa na bajeti yenye mashiko. Ngoja tusubiri bajeti ya kutetea mafisadi na waiba mchanga wa madini.
Nadhani sio vizuri kutoa hukumu kwa kitu ambacho huna uhakila nacho. Katika sheria zetu ...mtu ana kuwa ni ntuhumiwa mpaka pale mahakama inapotoa hukumu stahiki.

Tujadiriane kwa weledi bila kutoa lugha za kashfa kama wanavyo fanya watunga sheria wetu.

Mathalani nani mwizi wa makinikia?Ali hukumiwa katika mahakama gani?
 
Mawazo ya Mbowe ziro form 6 ndio kakwambia uje uandike huu utumbo hapa??? Zoezi la Uchunguzi wa Mchanga liko chini ya Rais. Tangu lini Ratiba za Rais zikapangwa kulingana na shuguli za Bunge??? HERI MTU YULE ATAKAYE KUPUUZA
Lakini mbowe na pumba mahalage mbona wanafanana tu elimu zao tofauti iko wapi wote wanaongoza watu.
 
Back
Top Bottom