Elections 2010 Kambi ya mtaka urais 2015 yasambaratika

Jambo la kutilia maanani hapa ni kuhakikisha kuwa kikundi hiki hakifanikiwa hata kidogo kwani madhara yake ni makubwa na yana mgusa kila mtanzania bila kujali itikadi yake ya siasa. Uwe CDM,CUF,TLP,CCM au usiwe na chama impact yake utaipata tu kwani hata sasa nadhani twaonja utamu wake kupitia mgawo wa umeme ambao ni zao lao kupitia Richmond.

Ya uchaguzi wa 2015 tuyaweke pembeni tu deal na maendeleo ya nchi kwa sasa kwani badala yake wabunge,mawaziri,makatibu wakuu na viongozi waadamizi wa serikali wanakalia kuharibu tu kazi.

Wenye nafasi za maamuzi hebu wachukue hatua sasa.
nakubaliana na wewe kwa 100% hili kundi litolewe ni virus kwenye nchi hiii!
 
habari hizi hazibebi mantiki yoyote ya mstakabali wa taifa letu, watanzania tumeisha amua kwamba urais 2015 chadema, hizi habari za nani ndani ya ccm anategemea kuwa rais 2015 ni uchafu, ni matusi, ni dharau na kejeri kwa watanzania.

Hakuna mahusiano ya ccm na urais mwaka 2015.
mkuu hizi isue usichukue kirahisi tuu mkuu si unajua hawa watu kwa kuchakachua! Lazima tujiandae mapema lowasa hatakiwi! Wewe lowasa ni mchafu tuu!
 
mkuu hizi isue usichukue kirahisi tuu mkuu si unajua hawa watu kwa kuchakachua! Lazima tujiandae mapema lowasa hatakiwi! Wewe lowasa ni mchafu tuu!

Hii vita transcend party affiliations ndugu zangu.mstaafu ana madhara kwa watanzania wote na sio wanachama wa chama fulani pekee.
tuamke
 
Ndugu zangu, hii nchi itarudishwa kwenye mstari wake na huyu Mstaafu sababu ndie aliyetuletea huyu Mkwele. Tunapashwa tumpe nchi hii aisafishe sababu ameshatubu na kwetu wakristo ukishatubu kwa Mungu wako unasamehewa. Mimi nashauri tumsamehe na apewe nchi chini ya Katiba Mpya, nahakika mtachonga sanamu yake baada ya Nyerere!
 
Habari hizi hazibebi mantiki yoyote ya mstakabali wa taifa letu, Watanzania tumeisha amua kwamba URAIS 2015 CHADEMA, hizi habari za nani ndani ya CCM anategemea kuwa rais 2015 ni uchafu, ni matusi, ni dharau na kejeri kwa watanzania.

Hakuna Mahusiano ya CCM na urais mwaka 2015.

Asante sana kwa maneno ambayo nadhani yanafaa kujibu hii hoja,
Mimi mwenyewe nimetamani kuweka maneno lakini nimeona yatakuwa makali sana,nimeamua kuacha kidogo presha ishuke maana nina hasira sana na huyu aliyekuja tofauti na kaka yake Moringe.
 
Mkakati wa hii kambi kushika nchi 2015 au mapema kabla ya hapo kama wananyotamani si wa kubeza hata kidogo. Ni kikundi hatari sana kinachojivunia ni utajiri haramu waliojikusanyia.mipango yao ni kutibua kazi za serikali ili kufanikisha mikakati yao.

Viongozi walionunuliwa kwa tamaa ya fedha ni wengi sana.miongoni mwao ni mkuu wa taasisi yenye jukumu la kusimamia serikali kwani aligawa nafasi ya uenyeviti wa kamati kwa mstaafu na wafuasi wake.

Nimeshangaa sana hata majuzi kwenye mkutano wa baraza la vijana wajumbe wamepokea "rushwa" ya 50000 kutoka kwa wakala mmoja wapo wa mstaafu huyu.


Wameenda mbali zaidi kwa kumuwezesha mjumbe wao kutoka mkoa wa asali kuwa mwenyekiti wa kamati ya kuleta mabadiliko ndani ya jumuiya.hii ni sawa na kumpa mbu kazi ya kutibu maralia.

KITENDO CHA JK KUWAONYESHA BAADHI YA WATOTO WAKE NDANI YA CCM 'HATI YA URITHI' NDIO HASA IMEGEUKA 'SUMU YA MAMBA' UPENUNI MWAO HIVI SASA

Kama hela ingalikuwa ni kila kitu kiasi hicho basi matajiri wafu wote wangejirejeshea uhai mara moja tu na kujiwekea uzio mkubwa sana kifo kisiwakute hata siku moja duniani.

Mbali na ukweli kwamba hicho kiringe cha kujongea sebuleni kushinwa hata kabla ya safari yake ndefu kufikia malengo dhalimu kuanza, tathmini yangu ni kwamba hakuna mtu amabaye yuko kwenye HATARI KUBWA na kikundi hicho kama Kikwete hapa nchini.

Nasema hivyo kwa misingi ya maelekezo ya fikra kwamba tayari kundi hili, kama toto tundu alivyo kwa mzazi, alishapekua mikabati ya siasa za CCM nchini na kugundua kwamba KWENYE HATI YA URITHI jina kaandikwa yeye kuwa ndiye chanda chema kwa JK kutua uongozi wa Jamhuri ya Muungano wetu huu wa Tanzania.

Lakini kwa kuwa ni wazi kwao kwamba wale watoto wengine ambao majina yao hayamo kwenye hati ya urithi kupewa hata uongozi wa kata lakini wazidi sana tu kupendwa na wana-ukoo wa CCM waliowengi na kusemwasemwa kufaa kwao kumrithi baba yao 2015 basi wasiwasi wote kwa hiki kikundi cha mteule wa urithi waweza kabisa kukituma kufikiria kuhakikisha kwamba Baba 'ANAPISHA' ili uhakika wa urithi huo kutwaa salama mikononi mwao, kwa gharama yoyote ile, inajipa.

Kwa kuhitimisha wazo nawaasa wazazi mnaoandika HATI YA URITHI ndani ya familia zenu, kitendo cha kukiacha ovyo tu ikazagaa tu na kufikika na ama watakaoneemeka na au watakaokosa kabisa 'mgao wa mkate wa familia', kwa tathmini yangu ni jambo la hatari mwisho wa reli Chigoma na hata kuweza kuwa chanzo cha mzazi kupatiwa usafiri wa mapema zaidi ahera na ule uzao wake mwenyewe.

Sumu ya mama ya CCM iko upenuni mwa sebule yao na hivi sasa ina hali ni tete zaidi chini ya bahari na kutiwa wazimu hasa kukikumbukwa KIASI CHA RASILMALI zilizokwishawekeshwa na kikundi chenyewe ndani ya takriban miaka saba mpaka hivi sasa ili wakafikie kwenye ndoto zao hizi za ki-Alinacha Tanzania.
 
Ndugu zangu, hii nchi itarudishwa kwenye mstari wake na huyu Mstaafu sababu ndie aliyetuletea huyu Mkwele. Tunapashwa tumpe nchi hii aisafishe sababu ameshatubu na kwetu wakristo ukishatubu kwa Mungu wako unasamehewa. Mimi nashauri tumsamehe na apewe nchi chini ya Katiba Mpya, nahakika mtachonga sanamu yake baada ya Nyerere!

Ni kitubio cha aina gani amefanya HUYO? Wakristu twa-AMINI kwamba kitubio kinaanza na kumwomba MSAMAHA uliyemkosea (Yule unayemwona) kabla ya kwenda kutubu kwa Muumba wako (Asiyeonekana). Kitubo kingine cha aina yoyote kinachofuata mfumo tofauti na huu sifikiri kama hakitakuwa BATILI.
 
Naamini ishu kubwa sio mgombea wa CCM 2015 ila namna hawa wastaafu wanavyorudisha nyuma nchi yetu.

Ni Jambo la kutia shaka sana kama kweli Watanzania tutaendesha nchi kama tunaendesha na kusimamia kombe la Dunia. World Cup safari hii Afrika ya Kusini, miaka minne ijayo Waraabu, Miaka minne ijayo Bara fulani. Kati ya uchaguzi na Uchaguzi hakuna kushughulikia maendeleo ni kuandaa viwanja vya ku-host Uchaguzi ujao. Hizi ndizo siasa za Vyama vingi ??? Mbona tunapotea huku tukijiona !!!!
 
Nilishasema kwenye thread moja humu JF kuwa, LOWASSA NA JAKAYA NA ROSTAM HAWATENGANISHWI NA CHOCHOTE, NI WAMOJA! Hivyo kuhusu Lowassa kugombea urais 2015 ni jambo la muda tu na JF itashuhudia hii ndoto ikitimizwa panapo uzima na Mungu akiwaweka hai hawa wenye utatu mfisadifu, ukiweza kutegua kitendawili na kiza kinene mbeleni tegua!
 
Ndugu zangu, hii nchi itarudishwa kwenye mstari wake na huyu Mstaafu sababu ndie aliyetuletea huyu Mkwele. Tunapashwa tumpe nchi hii aisafishe sababu ameshatubu na kwetu wakristo ukishatubu kwa Mungu wako unasamehewa. Mimi nashauri tumsamehe na apewe nchi chini ya Katiba Mpya, nahakika mtachonga sanamu yake baada ya Nyerere!

huyu dhambi yake ni kama kumkashifu Roho Mtakatifu hivyo hasameheki...labda kwako
 
Akifanikiwa tunamsubiria jukwaani,aje atuombe kura,uamuzi ni wetu,ikumbukwe kuwa tutakuwa tushabadili katiba na tutakuwa na tume huru ya uchaguzi.
 
Kwan we ndutu uko kambi gani!?

Mimi naona huyu kambi yake ni watanzania wanyonge, wazalendo na waathirika wakubwa wa hila, wizi na unyang'anyi wa rasilimali na jasho la wananchi maskini ambao kila siku wanayoamka basi mambo ni afadhali ya jana. Wewe mwenzetu uko na hao waliolaaniwa?
 
'kijana muasi' anacheza sana na media,kumbe ni maandalizi kuelekea 2015?

Ameng'ang'ania media kinoma. Kwa kweli anamnyima usingizi mzee wa watu. Mwenyewe keshaweka miundo mbinu ya kum-prove wrong baba wa Taifa halafu yeye anaharibu dili!
 
kikawaida mimi si mchangiaji lakini taarifa hii imenikuna sana. Hivi pamoja na scandal za kujiuzulu kwa kashfa bado mtu anaweza kuwa na uchu wa urais. Tufike mahali tusiwafanye watu ni mbumbumbu. Baba wa Taifa alishasema yote. Kwamba huyo bwana hafai
 
Mimi naona huyu kambi yake ni watanzania wanyonge, wazalendo na waathirika wakubwa wa hila, wizi na unyang'anyi wa rasilimali na jasho la wananchi maskini ambao kila siku wanayoamka basi mambo ni afadhali ya jana. Wewe mwenzetu uko na hao waliolaaniwa?

naunga mkono hoja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom