Swala la kusameheka kanisani kuna uhusiano gani na urais. Watanzania wanaendelea kukaa gizani alafu mtu mzima anaongelea suala la kusamehewa. Leo hii serikali inalazimika kulipa pesa za dowans kwa umeme ambao haupo. Haiingii akilini kuongelea suala la kutubu wakati watanzania wa kawaida wanaishi bila umeme. Ni vizuri tukaongozwa na uzalendo kuliko maslahi binafsi.