Kambi ya mtaka urais 2015 yasambaratika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kambi ya mtaka urais 2015 yasambaratika

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ndutu, Mar 23, 2011.

 1. n

  ndutu Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa takribani mwezi mmoja sasa, tumekuwa tukisikia kuwa kambi ya mmoja kati ya wanaowania kugombea Urais mwaka 2015 imesambaratika. Habari hizo zinadai kuwa mgombea huyo ambaye anaonekana kuwa na nguvu sana za kifedha, kwa muda mrefu amekuwa akimtumia "Waziri" mmoja ambaye ni kijana na mwenye ushawishi mzuri ktk Jumuiya ya Vijana wa CCM.

  Waziri huyo kijana amekuwa nguzo kubwa sana ya kuandaa mtandao wa mgombea huyo ambaye ameshawahi kushika nafasi moja wapo ya juu ktk Serikali, lakini kwa bahati mbaya, kutokana na uchu na tamaa yake ya kujilimbikizia mali, alipata "ajali ya kisiasa" na kulazimishwa kukaa upenuni mwa duru za kisiasa kwa muda kidogo, akisubiri kuitwa tena ktk sebule ya siasa.

  Baaada ya kuona baba mwenye nyumba hamuiti ktk sebule hiyo, mgombea huyo ambaye ni maarufu kwa kuitwa "mstaafu", ijapokuwa hakustaafu bali, alilazimishwa kujiuzulu, aliamua kuanza makeke ya kujichongea njia ya kuelekea ktk sebule. Alikusanya timu yake iliyojaa "majeruhi wa kisiasa" na kuanza safari ya kuelekea sebuleni. Walikuwa mikakati na kupeana majukumu kedekede ya utekelezaji wa mpango wao huo. Waliamua kufanya karibu kila aina ya vituko kumchefua "baba mwenye nyumba" ili agombane nao, lakini hawakufanikiwa kwani "baba mwenye nyumba" huyu amekuwa makini saaana na watu hao, kwani anapata taarifa ya kila wanachokifanya, na anasubiri muda muafaka ufike wa kuwatendea haki stahili.

  Ukimya wa "baba mwenye nyumba" umekuwa ukiwapa kiburi kikubwa sana "majeruhi" hao hata kumdhihaki mwenye nyumba. Wananchi wamekuwa wakilalamika sana juu ya ukimwa wa "mwenye nyumba", mwishowe wamebaki kumuonea huruma tu, na kuomba kwa Mungu kusitokee jambo baya kwa nchi kutokana na hali hiyo.

  Mgombea huyu ambaye yupo tayari kutoa kiasi chochote cha hela kitakachotakiwa, ilimradi tu apate ridhaa ya kuingia sebuleni, anagubikwa na kashfa lukuki zinazomfanya asikubalike kabisa ktk jamii ya watanzania. Ndio maana anatumia hela nyingi sana kuwanunua waandishi wa habari (majina na ushahidi tunao), wabunge (majina na ushahidi tunao), viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali (majina na ushahidi tunayo). Mnada huu una lengo la kumjenga, lakini wakati huo huo kuwachafua wale anaowaona kwamba ni tishio kwa harakati zake hizo za kujijongeza sebuleni. Haishangazi kuona harakati katika vyombo vya habari na blogu mbalimbali akianzisha mada za kuwapakazia wenzake akidhani wananchi wataingia mkenge na kuwasahaulisha madhila na machungu yanayotokana na unyonyaji wake yeye na "wanafunzi wake".

  Baada ya kugundua kuwa 'MGOMBEA' huyo hauziki, kijana aliyebeba dhamana ya kutengeneza mtandao akaamua kujitwalia maamuzi ya kumkata jongoo kwa meno, kwa kuvivaa viatu vya kuendea sebuleni yeye mwenyewe, huku akisaidiwa na wadogo zake kwa nguvu zote zinazotakiwa. Hapo ndipo mfarakano ulipoanza, na kufikia sehemu ambapo mfadhili wa mpango huo, mwana siasa mmoja mwenye asili ya Asia, mwenye sifa kubwa ya wizi na ubadhirifu wa mali ya watanzania, asiye na huruma hata kidogo na baba na mama zetu wanaoteseka vijijini kwa kukosa huduma muhimu, aliamua kumkatia mawasiliano kijana huyo anayejiamini kuwa ana uwezo wa kuliongoza Taifa hili la Tanzania ifikapo mwaka 2015.

  Kwa kipindi kirefu, timu hiyo ya "majeruhi" huyo wa kisiasa imekuwa ikifanya maandalizi na kuyatekeleza kwa namna yao. Wameweza kuwapata wajumbe wengi wa NEC-CCM na baadhi ya watendaji waandamizi ktk CCM. Wamefika sehemu wanaona hata kusubiri mwaka 2015 ni mbali sana, wanatamani kutumia njia ya mkato kuingia sebuleni. Njia pekee ya mkato kuingia sebuleni ni kupitia uchaguzi wa CCM mwaka 2012. Hapo ndipo wanapoweza kutimiza azma yao. Njia nyingine za mkato ni ngumu kwao, kwani madahara yake ni makubwa zaidi. Haishangazi kuona kwamba kuna habari zinaandikwa kuhusiana na matamko ya vijana wakijaribu kutaka kutenganisha kofia ya chama na serikali, ili waige mfano wa Zuma na ANC walivyomfurusha Mbeki.

  Hivi karibuni, mbunge mmoja kijana toka mikoa ya magharibi alionekana kuchanganyikiwa saaana na hali hii, hata kushindwa kujizuia na kubwabwaja ovyo, na kutoa maneno makali dhidi ya "kijana muasi". Hofu kubwa inayowapata ni kwa sababu kijana huyo alikuwa ni tegemeo kubwa sana la mgombea huyo mwenye uchu wa kuongoza nchi hii kama vile amerogwa. Kama "majeruhi" huyu angefanikiwa kuingia sebuleni, basi angekuwa "kiumbe" wa kwanza kuuthibitishia ulimwengu kuwa maneno ya marehemu Baba wa Taifa si ya kweli. Mgombea huyo hana siha wala sifa ya uongozi. Kuna wakati aliishakemewa na marehemu Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere, pale alipotaka kuvaa viatu vya kuendea sebuleni miaka kadhaa iliyopita.

  Wana JF, hayo ndo yanayojiri katika mustakabali wa Taifa letu hili ambalo bado linaendelea kuuguza majeraha ya vitendo vya ufisadi.
   
 2. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Join Date : 22nd March 2011
  Posts : 12
  Thanks0Thanked 0 Times in 0 Posts

  Rep Power : 0

  Mtateseka sana.
   
 3. T

  Tiote Senior Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sitaki kuamini kama habari hizi njema zimetokea kwa sababu hawa jamaa wana njama nyingi sana za kuzuga watu. Pamoja na kwamba huyu waziri kijana hana ubavu wa kumshinda huyo anayeitwa majeruhi, na hata uwezo wa kukaribia hata upenuni, lakini ujumbe tunaoupata hapa ni kwamba kumbe hata miongoni mwao wanajua kwamba huyu jamaa ni sumu na hana hata chembe ya sifa ya kushika hatamu za nchi hii. Mungu ibariki Tanzania na watu wake!
   
 4. b

  banyimwa Senior Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ni kweli tutateseka sana maana vita vya tembo nyasi ndizo zitaumia, lakini ukweli ni kwambahuyu mtu hatufai na lisemwalo lipo. Kwa dhambi alizowatendea watanzania, adhabu za namna hii na nyingine yoyote zitaendelea kumuandama. Hivi mwenyewe anapita mitaani na kusalimiana na watu akasikia hisia zake, au anasubiri mpaka wakati huo ufike ndipo aumbuke?
   
 5. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Mkakati wa hii kambi kushika nchi 2015 au mapema kabla ya hapo kama wananyotamani si wa kubeza hata kidogo. Ni kikundi hatari sana kinachojivunia ni utajiri haramu waliojikusanyia.mipango yao ni kutibua kazi za serikali ili kufanikisha mikakati yao.

  Viongozi walionunuliwa kwa tamaa ya fedha ni wengi sana.miongoni mwao ni mkuu wa taasisi yenye jukumu la kusimamia serikali kwani aligawa nafasi ya uenyeviti wa kamati kwa mstaafu na wafuasi wake.

  Nimeshangaa sana hata majuzi kwenye mkutano wa baraza la vijana wajumbe wamepokea "rushwa" ya 50000 kutoka kwa wakala mmoja wapo wa mstaafu huyu.


  Wameenda mbali zaidi kwa kumuwezesha mjumbe wao kutoka mkoa wa asali kuwa mwenyekiti wa kamati ya kuleta mabadiliko ndani ya jumuiya.hii ni sawa na kumpa mbu kazi ya kutibu maralia.
   
 6. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Watamalizana wenyewe....! Na bado...ukimwaga damu ya mtu, itakutesa hadi tone la mwisho...! na ya kwako itamwagika, taka usitake...! CCM wenyewe wameyajenga yote yanayotukia, na lazima yawafike! wayavune waliyoyapanda...! Yetu macho...kwa makini tunafuatilia saana! Vita vyao ni vya panzi...ila sisi kwetu dira ni "Taifa kwanza" huo ulevi wao uje baadaye!
   
 7. shemasi

  shemasi Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ninachomsifu mstaafu huyu ni moyo wa kutokukata tamaa japo wanaomzunguka hawamuambii ukweli kuwa asahau kuingia ikulu.
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tena mdharau mwiba mguu huota tende. Hawa watu wana kiu ambayo imepitiliza na wamejiandaa kufanya lolote ili mradi wafanikishe azma yao na mimi nampa big up huyu jamaa aliyeileta thread hii jamvini ingawaje naweza kukuhakikishia thread hii haitodumu humu maana itakuwa moved sasa hivi.

  Kama Mkuu anataka kuendelea kushikilia hatamu za nchi hii ni lazima afuatilie nyendo za hawa jamaa maana sasa hivi wao wanaungua mafuta ya usiku wa manane kupanga namna ya kusambaratisha waadilifu na kutwaa nchi. Lakini huyu dogo aliyeasi ana ubavu wa kuhimili kishindo cha miamba hii? Ngoja tuone hili picha litakakoelekea.
   
 9. chairman mao

  chairman mao Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ingekuwa kwetu china huyu mtu angeshakuwa historia kitambo sana kwani haturuhusu ujinga kama huu.hatua zatakiwa kuchukuliwa na sio kuangalia tu.......this is :hatari::hatari::hatari: need to :smash::smash::smash: these guys
   
 10. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  kwanini kuumiza vichwa kwa ajili ya mgombea wa CCM 2015?
   
 11. w

  wazo mbadala Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naamini ishu kubwa sio mgombea wa CCM 2015 ila namna hawa wastaafu wanavyorudisha nyuma nchi yetu.
   
 12. i

  imara Member

  #12
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I'm tired of hearing how these crew sabotages our country.

  It's high time now for the president to take an actions.
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nakukubali mkuu! Lakini hata kugombea ni ishu kwa sababu kinachoendelea sasa ni mipango ya kuhujumu ili kujipa undue advantage kwa urais wa 2015. Hata baadhi ya mawaziri wako busy kuhakikisha kwamba wanachangia ili wasipitwe na treni hii.
   
 14. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Binafsi propaganda za namna hii wala hazinigusii kwani kama hicho kisa ni wao (CCM) sisi (CDM) hatuna kinyongo na huyoo mnayemwitaa mstaafu kabla hamjapitisha jina la mgombea wenu apambane na mgombea anayetambulika (DR SLAA) kwa umma tayari..
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ni kweli aiseee HALAFU UNAAMBIWA HAKUNA MTU WAKUMZUIA NDANI YA CCM! YAANI CCM IMEOZA KWELI!:angry:
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwani kujiunga kwake 22 mwezi huu kunahusiana nini na mada yake.
   
 17. tsar

  tsar Member

  #17
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jambo la kutilia maanani hapa ni kuhakikisha kuwa kikundi hiki hakifanikiwa hata kidogo kwani madhara yake ni makubwa na yana mgusa kila mtanzania bila kujali itikadi yake ya siasa. Uwe CDM,CUF,TLP,CCM au usiwe na chama impact yake utaipata tu kwani hata sasa nadhani twaonja utamu wake kupitia mgawo wa umeme ambao ni zao lao kupitia Richmond.

  Ya uchaguzi wa 2015 tuyaweke pembeni tu deal na maendeleo ya nchi kwa sasa kwani badala yake wabunge,mawaziri,makatibu wakuu na viongozi waadamizi wa serikali wanakalia kuharibu tu kazi.

  Wenye nafasi za maamuzi hebu wachukue hatua sasa.
   
 18. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari hizi hazibebi mantiki yoyote ya mstakabali wa taifa letu, Watanzania tumeisha amua kwamba URAIS 2015 CHADEMA, hizi habari za nani ndani ya CCM anategemea kuwa rais 2015 ni uchafu, ni matusi, ni dharau na kejeri kwa watanzania.

  Hakuna Mahusiano ya CCM na urais mwaka 2015.
   
 19. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Atakuwa ameshangaa amewezaje kupost post 12 kwa siku moja!!! Au siku hizi kuna walioajiriwa kuandika humu JF??????
   
 20. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  You couldn't be more clear! Vitendo vya hawa jamaa vinavuka kiwango cha kiitikadi na wale wanaodhani kwamba siyo wana-CCM (nami pia siko CCM) wajue kwamba hawaishi nchi ya peke yao. Tunasaga nao lami na tunahangaika wote na mishumaa na mashimo ya barabarani wakati katika hali ya kawaida tungeweza kujadili ajenda ya maendeleo badala ya kujadili namna ya kutafuta solar power.
   
Loading...