Vikwazo ilivyowekewa Iran hivi sasa haijawahi kuwekeza katika kipindi chochote kile,vikwazo vilivyopita Iran iliruhusiwa baadhi ya vitu mfano kuuza mafuta kwa nchi ambazo zimepewa kibali na Marekani (Japan,S.korea, Turkey,India,nk) lakini hivi sasa nchi hizo zote zimenyimwa ruhusa ya kununua mafuta toka Iran,ndo maana kila kukicha Iran inahaha kuwatisha EU kwamba eti iwakomboe kwenye vikwazo vya Marekani au la watakiuka mkataba wa nyuklia. EU wakiongozwa na France walitaka kuwapa $15bn kama mkopo,Marekani ikakataa!
Unasemea silaha wanatoa Wapi,kwani Alshabab na Boko Haram silaha wanatoa Wapi?! Unadhani hizi ni zama za analogy,hao Hamas wanatengeza makombora yao na silaha nyingine hivyo kwa Hezbollah na vikundi vingine vya kigaidi.
Hakuna nchi ambayo intelligence yake itaweza kucover kila kitu,baadhi ya silaha zinapita hasa kupitia black market. Hata Urusi walitaka kushambuliwa na magaidi lakini CIA ndo wakawashtua wakaharibu lile shambulio kabla halijafanyika
Iran haijaingia eti Iraq sababu ya Daesh,Iran na Iraq ni washirika wazuri tu. Hao Daesh wa Iraq walitekezwa na mashambulizi ya muungano yaliyokua yakiongozwa na Marekani wakishirikiana na serikali ya Iraq wakiwatimua ISIS toka Mosul na miji mingine.
Russia ya 1990 na ya Leo ukitoa Crimea imeongezeka nini?!
MWISHO; Mimi sio mdau wa mambo ya kidini,masuala ya Taifa teule siyajui,naizungumzia Israel kama nchi ya kawaida.