Kamati za bunge:hatutaki wabunge wa zanzibar kwenye kamati isiyokuwa ya muungano.

..kitendo cha kuteua wabunge toka Zenj ktk kamati zisizoshughulikia masuala yaliyo ktk Muungano ni kukiuka mkataba na makubaliano ya Muungano wa Tanganyika na Zenj.

..pia wapiga kura wa Zenj wamewapigia kura wabunge wao waje kutetea masuala yao ktk bunge la Muungano. sasa wabunge hao wanapoteuliwa kwenye kamati ambazo zinashughulika na mambo ya Tanganyika, hamuoni kwamba ni dhuluma dhidi ya wapiga kura wa Zenj?
 
Naona mnaconfuse na sheria za Muungano. Hakuna kitu Tanganyika baada ya Muungano bali kuna Tanzania.
 
Hizo ni baadhi ya kamati za bunge.....hatutaki mbunge wa zanzibar kwenye kamati isiyokuwa ya muungano.....tutawakubali kwenye washirikishwe kwenye kamati zenye masuala ya muungano....mfano kamati kama ya serikali za mitaa au madini watakuwa wanafanya nini huko .... kuna baadhi ya kamati wao kule zanzibar tayari zipo kwenye serikali ya mapinduzi.........wenzetu wanataka kufanya siasa hapa lakini wajuwe watu wameamka na wanajuwa mipaka ya kila mmoja kwenye muungano wetu.....
 
Last edited by a moderator:
Mimi naona huyu mkuu Phillemon ame underestimate wana JF. Nadhani kwa mawazo yake anaona majority ya wanaJF ni Wabara basi chochote kinacho tetea "Ubara" kita pigiwa makofi na kugongewa thanks nyingi. Watanzania ni zaidi ya uwajuavyo. Ni watu very fair na mara nyingi humpa mtu stahili yake.

Anyway kuhusu mada hapo juu kama nilivyo sema awali Bunge ni la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Last time I checked Wazanzibar nao ni Watanzania. Japo katiba yetu hasa linapo kuja swala la muungano lina nyufa nyingi ila kusema Wazanzibar wasiwepo kwenye baadhi ya kamati za Bunge la muungano ni sawa sawa na kusema huwa tambui kama Watanzania wenzako.

Mimi binafis kusema ukweli nashauri na napigania tuwe na serikali moja tu ya Kitaifa. Si mbili, wala si tatu! Huku kuwa na hizi serkali ambazo ni subset za serikali kuu naona kuna kufanya watu wajione kwamba kuna "wao" na "sisi". Tutengeneza serikali moja halafu tuanze nation building tujione kama wamoja.
MwanaFalsafaI,

Mchango wako wa kuhusu wabunge umeuleza vizuri. Pia naungana na wewe pale uliposema kuwa nyufa ni nyingi katika katiba yetu. Kwa bahati mbaya umesahau kuwa katika Tanzania kuna katiba Tatu,. visible ones ziko mbili ile ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar(Tanzania) na invisible one, ile ya Tanganyika.


Na kwa mujibu wa magwiji wa katiba na sheria, akiwemo Prof,. Shivji, baina ya Katiba hizi,hakuna iliyo superior juu ya nyengine. Lakini inapokuja "The articles of the Union" na Katiba ya Jamhuri basi "The articles " ni superior na Katiba ni subordinate. In the court of law, katiba yetu inapo-contravene na The articles of the union, basi "the articles" ina-prevail.

Ni kusema kuwa the articles of the Union ndio Suprime instrument ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar, kwani ndiyo iliyozaa Katiba ya Muungano.Na kwa maana hiyo, katiba ya muungano haiwezi kujiundia uwezo wa kujipa madaraka bila ya idhini ya Tanganyika na Zanzibar; wadau waliosaini "The articles". Inawezekana hili ni katika hizo nyufa unazozisema.


Unapokuja na Serikali moja kama solution, sio tu kuwa umeongeza upana wa ufa, bali unakuwa umeuangusha chini ukuta wote. Ile hofu ya kumezwa na Tanganyika,waliyokuwa nayo na waliyo nayo leo Wazenj itakuwa tumeitimiza.


Mwalimu pia aliliona hili, yeye aliamuwa kutumia back door, alikuwa anaongeza orodha ya mambo ya muungano, kila ukizidisha urefu wa orodha huu ni kuwa the weaker the Zanzibar Government becomes, in the end, inapoteza maana ya kuwepo kwake. Uliviona vita vya wazenj pale Pinda aliposema Zanzibar si nchi, sasa utakapowambia,"tunaimeza kabisa", Patakalika hapo? Hiyo itakuwa ni Annexation.


But let us assume kuwa Wazenj wataridhia hili la Nchi moja ,Serikali moja, jee sisi kama Tanzania tutakuwa pia tayari Kuungana na Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kuunda nchi moja, na serikali moja na utaifa mmoja?


Mtihani huu!


Mimi binafsi ningependelea Muundo wa Serikali tatu,
Au mfumo wa One country, two systems (Hong Kong na China)
Au mfumo kama wa US,federal Gvt na State Gvts and the least Muundo wa EAC au EU
 
Naona thread ya bwana huyu imeeleweka vibaya; kwanza siyo kweli kusema kuwa wabunge wote wana haki na madaraka yanayolingana wanapokuwa bungeni. Kwani chini ya katiba ya muungano kuna maswali yanayohusu muungano ambayo uamuzi wake unahitaji wabunge wa pande zote mbili za muungano kila upanda upige kura ya peke yake. Nakupitishwakwa jambo lolote kuhusu maswala hayo kunahitaji theluthi mbili ya wabunge wa kila upande uafiki. Kwa maneno mengine kuna wakati wabunge kutoka Zanzibar wanakuwa na nguvu kubwa kupita wale wa bara; kwa maana kwamba pamoja na idadi yao kuwa karibu asilimia 15 ya wabunge wote, lakini wana uwezo kikatiba kukwamisha maamuzi fulani fulani hata kama yanaungwa mkono na wabunge wote wa bara. Suala la pili ni kwamba maadam mambo yanayohusu Tanganyika pekee nayo yanashughulikiwa na serikali ya muungano hakuna mantiki yeyote kumshirikisha mtu asiye Mtanganyika katika kushughulikia masuala hayo. Kama mambo ya wazanzibari yanashughulikiwa na wazanzibari wenyewe kwanini hisiwe hivyo kwa watanganyika?
 
Nani kakwambia wazenj hawapendi muungano?wao ndio wafaidika no 1 wa huu muungano,cheki walivyojitwalia ardhi,cheki idadi ya wabunge,cheki mawaziri nk yaani muungano unawaacomodate kuliko ambavyo zanzibar ingewaacomodate


wewe umenielewa..

Nimetoa changamoto hii nikiwa na maana moja..muungano tunaupenda na wazanzibar ni ndugu zetu......lakini kinachonitatiza ni kuwa wabunge wa zanzibar ni hodari wa kutetea zile hoja zenye masilahi yao tu..mfano mafuta[tumeshasema na mafuta wachukue]...na kero zingine za muungano zinazowagusa...
Ikija hoja ambayo haiwaumizi ....wanajiweka nyuma kwa nini?? haata hili la katiba ya Muungano kuna ambao wanaona kama haliwahusu......

Naomba nikumbusheni mbunge mmoja wa zanzibar ambaye ...amesimama kidete kuwatetea wanyonge wa maeneo kama nyamongo,kilombero,Namtumbo....etc..............nadhani kuna umuhimu wa kuwapatia wabunge wa zanzibar [wapya] study tour ya kuitembelea Tanzania yote hadi vijijini....na wale wa bara watembelee zanzibar hadi mashamba...ili kuwapa ufahamu mkubwa zaidi wa nchi wanayoiwakilisha na mahitaji yake....
Tangu mwaka 1995 au hata enzi ya kina Njelu kasaka na G55 Nani amekuwa mtetezi wa Watanzania bila kujali upande...kwa nini wengine wasubiri uteuzi au hoja zinazowagusa tu???
 
Nadhani Phelemon has a point, illa miss presentation. Labda tuseme hivi, Is it fair kwa mbunge wa znz kushiriki maamuzi kwa jambo ambalo serikali ya Muungano haina madaraka kulitekeleza znz? wao si wana Baraza lao. Such points should precursors of rewriting Constitution!
 
Nadhani Phelemon has a point, illa miss presentation. Labda tuseme hivi, Is it fair kwa mbunge wa znz kushiriki maamuzi kwa jambo ambalo serikali ya Muungano haina madaraka kulitekeleza znz? wao si wana Baraza lao. Such points should precursors of rewriting Constitution!
o

..chukua mfano kamati aliyokuwa akiiongoza zitto ya hesabu za mashirika ya umma....au ile ya SLaa ya serikali za mitaa....umakini na uchungu wao umesaidia kwa kiasi kikubwa ...nina mashaka kuwa wapinzani waliokuwa wakizishika nafasi hizi huko nyuma walikuwa wakifumbia macho masuala...
Ni wazi kiongozi anayependa siasa atachagua kuweka wabunge wasiokuwa na uchungu kwenye kamati kama hizi........na ndio pia suala la katiba linapokuwa na umuhimu....
 
Mtoa mada umekwenda mbali mimi ni moja ya ambao huwa naungalia muungano kwa viulizo lakini sijawahi kwenda mbali kwa fikra za kibaguzi kiasi hicho.

Unaweza kuwa na point labda kwa kamati zinazohusu bara zinaweza zikawa hazihitaji mbunge wa zanzibar lakini haya ni makubaliano ya kiutashi baina ya wabunge husika.

Halafu Philemoni kauli yako yaonyesha chuki, hila na fitna, zidhani kama unatokea kwenye jamii ya kistaarabu na wala siamini wewe ni chdema kama wengine walivyodai maana hata Dr Slaa aliwaahidi wazanzibar kuwa mafuta ya bara yatabaki kuwa ya bara na mafuta ya zenji yatawanufaisha wazenji kama ambavyo madini ya bara hayawanufaishi wa zanzibar
 
  1. finance and economic affairs
  2. public accounts
  3. social services
  4. social welfare & community development
  5. constitutional, legal and public administration
  6. standing orders
  7. parliamentary privileges, ethics and powers
  8. energy and minerals
  9. hiv/aids affairs
  10. infrastructure
  11. public corporation accounts
  12. miscellaneous amendments
  13. land, natural resources and environment
  14. agriculture, livestock and water
  15. foreign affairs, defence and security
  16. industries and trade
  17. local government accounts
hizo ni baadhi ya kamati za bunge.....hatutaki mbunge wa zanzibar kwenye kamati isiyokuwa ya muungano.....tutawakubali kwenye washirikishwe kwenye kamati zenye masuala ya muungano....mfano kamati kama ya serikali za mitaa au madini watakuwa wanafanya nini huko .... Kuna baadhi ya kamati wao kule zanzibar tayari zipo kwenye serikali ya mapinduzi.........wenzetu wanataka kufanya siasa hapa lakini wajuwe watu wameamka na wanajuwa mipaka ya kila mmoja kwenye muungano wetu.....

acha kubabaisha watu ...unachotakiwa kudai tanganyika yako kwanza....hiyo ndio solution...
 
Back
Top Bottom