Kamati yaanza kupokea kero za wafanyabiashara Kariakoo

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Kamati ya watu 14 ya kushugulikia changamoto za wafanyabiashara nchini imeanza kazi kwa kukutana na makundi tofauti ya wafanyabiashara. Kamati hiyo ilisema Dar es Salaam jana kuwa itafanya kazi kwa weledi, itasikiliza maoni yote na itazunguka katika masoko nchini.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk John Jingu ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamil, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu alisema hayo wakati kamati hiyo ilipokutana na wawakilishi wa makundi 15 tofauti ya wafanyabiashara katika eneo la Kariakoo.

Dk Jingu alisema jana ilianza kukutana na makundi ya wafanyabiashara wa sekta tofauti na kuwataka wazungumze changamoto katika ya kushughulikia changamoto sekta ya biashara hizo na wao watazichukua na kuzifanyia kazi kisha kuwasilisha taarifa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

"Semeni changamoto zote, sisi tumejitoa kufanya kazi hii kwa weledi, kusikiliza maoni na ushauri wenu wote, tunachotaka ni kupata suluhu, tuwahakikishie tutafanya kazi ndani ya muda na kuzingatia hadidu za rejea tulizopewa kwa wiki mbili na kuikamilisha," alisema.

Katika mkutano wa jana, makundi ya wafanyabiashara wa vitenge, vipuri vya pikipiki, vipuri vya magari na vilainishi vyake, vifaa vya umeme, simu, elektroniki, nguo, ujenzi, bidhaa mchanganyiko, dawa za binadamu, vifaa vya shule na ofisini, mafuta ya kupikia na sukari na vipodozi walitoa maoni yao.

Wakizungumzia changamoto katika biashara ya vitenge, wafanyabiashara wa bidhaa hizo walisema viwango vikubwa vya kodi vilivyowekwa katika kuingiza vitenge nchini vimeua bi-ashara hivo na sasa wameitawala wafanyabiashara wa nchi jirani.

"Kodi kubwa inayotozwa kwe nye kontena la vitenge linapoingia nchini imeua biashara, hii kodi ili-wekwa tu bila kuangalia hali halisi ya soko, kwa kivuli cha kusema tunalinda viwanda vya.ndani ambavyo navyo havifanyi kazi. "Kati ya viwanda sita vinavyofanya kazi ni viwili na tena sasa ni kimoja na hakizalishi vya kutosha," alisema Beatrice Joseph.

Alisema kutokana na kuwepo kwa kodi zisizo halisi kulingana na biashara husika, soko la vitenge zilihamia nchi jirani na hivyo kuikosesha nchi mapato ambayo awali wafanyabiashara walikuwa wanaingiza kontena 80 hadi 100 kwa mwezi la vitenge. Benatus Mlelwa allishauri kamati hivo kupeleka ushauri kwa serikali kufumua mfumo wa kodi na uwe wa pamoja ambao unatoza kodi zote ili kuepusha usumbufu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, Martin Mbwana alisema watatoa ushirikiano kwa kamati hiyo. "Niihakikishie serikali kuwa wafanyabiashara tutaendelea kulipa kodi, sisi ni wazalendo kwa nchi yetu, ila tunachotaka ni mazingira rafiki na tulipe kodi halisi kulingana na hali halisi ya biashara," alisema Mbwana.
 
“....Benatus Mlelwa allishauri kamati hivo kupeleka ushauri kwa serikali kufumua mfumo wa kodi na uwe wa pamoja ambao unatoza kodi zote ili kuepusha usumbufu...”
 
Kamati ya watu 14 ya kushugulikia changamoto za wafanyabiashara nchini imeanza kazi kwa kukutana na makundi tofauti ya wafanyabiashara. Kamati hiyo ilisema Dar es Salaam jana kuwa itafanya kazi kwa weledi, itasikiliza maoni yote na itazunguka katika masoko nchini.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk John Jingu ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamil, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu alisema hayo wakati kamati hiyo ilipokutana na wawakilishi wa makundi 15 tofauti ya wafanyabiashara katika eneo la Kariakoo.

Dk Jingu alisema jana ilianza kukutana na makundi ya wafanyabiashara wa sekta tofauti na kuwataka wazungumze changamoto katika ya kushughulikia changamoto sekta ya biashara hizo na wao watazichukua na kuzifanyia kazi kisha kuwasilisha taarifa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

"Semeni changamoto zote, sisi tumejitoa kufanya kazi hii kwa weledi, kusikiliza maoni na ushauri wenu wote, tunachotaka ni kupata suluhu, tuwahakikishie tutafanya kazi ndani ya muda na kuzingatia hadidu za rejea tulizopewa kwa wiki mbili na kuikamilisha," alisema.

Katika mkutano wa jana, makundi ya wafanyabiashara wa vitenge, vipuri vya pikipiki, vipuri vya magari na vilainishi vyake, vifaa vya umeme, simu, elektroniki, nguo, ujenzi, bidhaa mchanganyiko, dawa za binadamu, vifaa vya shule na ofisini, mafuta ya kupikia na sukari na vipodozi walitoa maoni yao.

Wakizungumzia changamoto katika biashara ya vitenge, wafanyabiashara wa bidhaa hizo walisema viwango vikubwa vya kodi vilivyowekwa katika kuingiza vitenge nchini vimeua bi-ashara hivo na sasa wameitawala wafanyabiashara wa nchi jirani.

"Kodi kubwa inayotozwa kwe nye kontena la vitenge linapoingia nchini imeua biashara, hii kodi ili-wekwa tu bila kuangalia hali halisi ya soko, kwa kivuli cha kusema tunalinda viwanda vya.ndani ambavyo navyo havifanyi kazi.
"Kati ya viwanda sita vinavyofanya kazi ni viwili na tena sasa ni kimoja na hakizalishi vya kutosha," alisema Beatrice Joseph.

Alisema kutokana na kuwepo kwa kodi zisizo halisi kulingana na biashara husika, soko la vitenge zilihamia nchi jirani na hivyo kuikosesha nchi mapato ambayo awali wafanyabiashara walikuwa wanaingiza kontena 80 hadi 100 kwa mwezi la vitenge. Benatus Mlelwa allishauri kamati hivo kupeleka ushauri kwa serikali kufumua mfumo wa kodi na uwe wa pamoja ambao unatoza kodi zote ili kuepusha usumbufu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, Martin Mbwana alisema watatoa ushirikiano kwa kamati hiyo. "Niihakikishie serikali kuwa wafanyabiashara tutaendelea kulipa kodi, sisi ni wazalendo kwa nchi yetu, ila tunachotaka ni mazingira rafiki na tulipe kodi halisi kulingana na hali halisi ya biashara," alisema Mbwana.
Imesnza kupokea tena.. sio kufanyia kazi??!
 
Back
Top Bottom