Kamati Ya Slaa Yalamba Posho Mara Mbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati Ya Slaa Yalamba Posho Mara Mbili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sumaku, May 19, 2009.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  May 19, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kamati ya Dk. Wilbroad Slaa yalamba posho mara mbili

  12 May 2009

  Na Mwandishi Wetu

  MAELEZO yalivowahi kutolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, kwamba wapo baadhi ya wabunge wanaopokea posho mara mbili, yamethibitishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.

  Ripoti hiyo ya CAG inathibitisha hali hiyo kutokana na ukaguzi wa hesabu za Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, ikidhihirika kuwa malipo yaliyofanywa kupitia vocha ya malipo yenye namba 1/8/066145, yaliyosainiwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo yalitumika kulipa wabunge posho.

  Katika hali ya kawaida, wabunge hulipwa posho na ofisi ya Bunge hususan wanapokuwa katika shughuli za kawaida zinazohusiana na kamati za Bunge.

  “Katika ukaguzi tulioufanya tuliweza kubaini matumizi yasiyostahili yenye thamani ya Sh 8,472,200 ambayo yasingeweza stahili kulipwa kwa kutumia fedha za miradi ya TASAF,” anasema CAG kupitia ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka ulioshia Juni 30, mwaka 2008, ripoti ambayo hata hivyo imekwishawasilishwa bungeni.

  Maelezo yaliyotolewa kwa CAG kuhusu malipo hayo yanasema; “Posho kwa ajili ya vikao vya kamati ya Bunge ya hesabu za serikali za mitaa Agosti 7 hadi 16 mwaka 2007 yalikuwa Sh 1,050,000.

  Kutokana na kubainika kwa hali hiyo huenda hadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Dk. Wilbroad Slaa, Mbunge wa Karatu, ikaingia doa mbele ya umma wa Watanzania.

  Aprili 2, mwaka huu, Dk. Hosea aliwaeleza wabunge waliojaribu kuhoji uhalali wake wa kuiongoza TAKUKURU wakati akiwa anakabiliwa na tuhuma za kusafisha kashfa ya zabuni ya mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond, kuwa kama watafanya hivyo basi nao pia wawe tayari kusikia kashfa zao mbele ya umma. Mara baada ya kutoa kitisho hicho kwa wabunge wakati wa semina ya miundombinu ya uadilifu iliyoandaliwa na Takukuru na Chama cha Wabunge wa Afrika (APNAC) na kufanyika kwenye Hoteli ya Whitesands, jijini Dar es salaam, Dk. Hosea alijikuta katika wakati mgumu.

  “Inakuwaje wakati wa mjadala wa Richmond, wewe mkururugenzi wa Takukuru ulikanusha kuwapo rushwa na uchunguzi wa kamati ya Bunge ulibaini kuwepo rushwa ndani ya kampuni hiyo?

  Je ni nani mwenye dhamana ya kukuadhibu wewe na taasisi yako kuhusu rushwa’’ alihoji Mbunge wa Busega, Dk.Raphael Chegeni katika semina hiyo.
  Swali hilo halikutegemewa na Dk Hosea na lilionekana kumuudhi na kulazimika kuchukua kipaza sauti na kusitisha maswali na kuanza kujibu kwa ghadhabu.

  “Hapa siyo jukwaani hivyo tusilete siasa. Nipo hapa kwa ajili ya kufundisha na kama ni suala la Richmond waziri mkuu alishaliongelea na ndiyo mwenye dhamana ya kujibu hilo. Mimi sina jibu kwa hilo na kama mtu hapendi kuvuliwa nguo kwanini umvue mwenzako,” alisema Dk Hosea.

  “Mjadala huu aachiwe Waziri Mkuu Mizengo Pinda na aliyeuliza swali hilo hanitendei haki kwani hakuna hoja nyingine ya maendeleo kwa jamii ambalo inaweza kujadiliwa… mbona mnang’ang’ania kujibu hilo pekee.

  “Najua kuna watu wanatumiwa ili niongee halafu nibabaike katika kujibu na nishindwe kufanya kazi yangu. Mbona mnang’ang’ania jambo hilo tu wakati kuna hoja nyingine za maendeleo kwa jamii. Kuhusu suala la Richmond sijibu ng’o.”


  Chanzo:
  Gazeti la Kwanza Jamii
   
 2. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Asante sana Sumaku, lete evidence ya Dr Slaa aliposaini kuchukua vijisenti vya Halmashauri zetu ndipo tumwage upupu!
   
 3. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #3
  May 19, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Habari ya gazeti la kwanza jamii yaweza kwa njia moja ama nyingine kupotosha kwa kuonesha kuwa Dkt. Slaa aliruhusu Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kutoa posho kwa wajumbe wa kamati yake na hivyo kupata posho mara mbili.

  Napenda kueleza kuwa mwaka 2007, Kamati ya LAAC ilikuwa chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Mgana Msindai. Kamati hizi za 'oversight' - ile ya LAAC na ile ya POAC zimeanza kuongozwa na wabunge wa upinzani kuanzia mwezi machi mwaka 2008. Kama kamati hii ililamba posho kutoka Halmashauri masikini kama ya Sumbawanga, jamii ijue kuwa haikuwa kamati ya Dkt. Slaa, ilikuwa kamati ya Msindai na dkt. Slaa hakuwa sio tu mwenyekiti, wala hakuwa mjumbe.

  Hivyo, habari hii ya kwanza Jamii inaposomwa izingatie ufafanuzi huu.
   
 4. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...asante sana Zitto kwa ufafanuzi! Naanza kuamini kuwa kuelekea uchaguzi magazeeti mengi yataundwa kwa malengo kadha wa kadha!!
   
 5. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Bora mkuu umemaliza ubishi mapema kwani wanaongeza magazeti yao wapake matope watu maskini kama Slaa...(Zitto check PM ZAKO)
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Asante Mh. Zitto kwa ufafanuzi wako. Kwa sababu evidence zita prove kuwa ni kumdhalilisha Dr. Slaa hasa tunapoelekea uchanguzi nataka kupitia vyombo vya sheria yafanyike yafuatayo:

  1. Gazeti liamriwe kusahihisha habari hizi kwa umma

  2. Kudai fidia ya kuchafuliwa jina Dr. Slaa na Kamati yake

  Hii itasaidia magazeti kupata adabu na fundisho ili waweze kuandika habari zilizofanyiwa utafiti wa kina na si ufisadi wa kuuza vichwa vya habari vya magazeti na kupata kipato cha kifisadi.
   
  Last edited: May 19, 2009
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Fisadis at work, na bado tutasoma mengi
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Gazeti lakikina Majid Mjengwa hilo? Sikujua yule dogo naye yuko cheap kiasi hicho!
   
 9. m

  mnozya JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Tunashukuru kwa ufafanuzi wako, ila tunaomba umshauri Slaa alichukulie hatua hilo gazeti ili iwe fundisho.

  Pia naomba email yako.
   
 10. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...nadhani Majid anatumiwa tu!
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Dogo anatumika tu.....! who are behind the whole business?
   
 12. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni muda wa kulamba kwa wenye moyo mdogo na watakao utajiri wa haraka
   
 13. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Maji taka
   
 14. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,721
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Zilipotoka habari za Majid kuanzisha gazeti lake, mimi nilikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kutoa maoni kwamba Majid Mjengwa ni mganga njaa tu; na anatumiwa na baadhi ya vibosile wenye historia yenye utata (ufisadi).

  Baadhi ya members walinishukia nitoe ushahidi.
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Who is that dude?
   
 16. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #16
  May 20, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  MAJJID MJENGWA HUU NI MWANZO MBAYA SANA, WENZAKO HUWA WANAJIFICHA KWANZA LAKINI WEWE KUANZA TU NA SPEED 180 LoL!
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Njaa mbaya sana Ndege Uchumi watu husahau hata basics!
   
 18. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  ... ule utabiri kuhusu nia ya gazeti bila shaka unaanza kujidhihirisha wazi, wengi tulitoa maoni kuhusu vyombo vya habari vingi kuibuka kabla ya uchaguzi na misingi ya ujengaji wao wa hoja. Kama kuna wakati tunahitaji vyombo vya habari kuwa makini nadhani ni sasa, haya mambo ya kumtumikia kafiri, yafike mwisho na tuanze kuwa watanzania kwanza kabla ya lingine lolote. Mwisho wa siku wanaoumia ni wananchi kwa miaka mi5 mingine, na kutibu majeraha hayo inachukua muda.
   
 19. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mungu akubariki Zitto kwa ufafanuzi wa kina usio tia shaka
   
Loading...