babykailama
JF-Expert Member
- Mar 5, 2012
- 251
- 243
Yaani yule Mh. GF wa Muhando alivyokuwa anatuzungukia tumtetee Muhando na kumkandamiza Maswi si la kweli? Yaani Mh. Kabwe alivyohamasisha wanakamati na wanabodi kupinga Muhando alichukuliwe hatua si kweli?
Sote tunakutana huko mjengoni siku hiyo: Tuna akili timamu na hakuna haja ya kuoneana haya kuwalinda mafisadi na kuwachafua viongozi wachache ambao hakika tunaona wanajitahidi kuajibika kwa nafasi walizopewa.
Swali la msingi ni hili: Ni namna gani bila kuacha mashaka yoyote (approach & methodological) kamati ilijilidhisha kuwa hakukuwa na jaribio au utoaji au upokeaji wa rushwa wowote. Kumbuka kuwa kamati ilikuwa inafanya kazi yake baada ya tukio kufanyika na kwamba rushwa hutolewa au hujaribiwa kutolewa katika mazingira ya usiri. Kama ni kutokana na mahojiano tu, Je mlitegemea kuwa Mbuge mwizi, fisadi au kuwadi wa mafisadi aje kwenu aseme mimi nilipokea rushwa kama alinyamaza kimya Bungeni siku hiyo? Kama watu wananyea kazi lakini hakuna anayestep down mwenyewe utategemea mla rushwa afike kwenye Kamati na kujisema mwenyewe? You have got to stop being naive!
1. Kama kweli kamati ilitakiwa kufanya kazi ya uchunguzi wa jinai, mlitakiwa kuangalia na kuchambua kwa undani juu ya mazingira, mfano: Wizara imemkuta CEO wa TANESCO na ukiukaji mkubwa wa kiuendeshaji na kwa kupitia Bodi yake imeamliwa asimame kazi kupisha uchunguzi halafu anakuja mwenzetu Mh. Kabwe anajitahidi kwa nguvu zote kuzuia hilo akishilikiana na mpenzi wa Mhando je hilo nayo ni siri? Je kamati ilikwenda deep kujiuliza wale Waarabu na wahindi waliokatiwa ulaji na ufisadi wa kusuply mafuta waliojaa Dodoma na wakawa wanazunguka na baadhi ya wabunge na ilipokaribia siku ya bajeti ya Nishati na Madini wakawa restless ni kwa nini?
2. Je kamati iliwasiliana na makampuni ya simu na kujaribu kutrack jinsi mazungumzo yalivyokuwa siku hizo kati ya CEO TANESCO- Mwenyekiti wa Bodi- wale wabunge wawili (dada zangu na wengine walitajwa humu) akiwemo Mh. Kabwe?
3. Kwa vile kamati ilikuwa inashughulikia jambo nyeti ambalo lingekuja kuleta ubishi kama ambavyo tunaona sasa, kwa nini hamukuhusisha makachero wenye uzoefu wa ku- interrogate watu wenye tuhuma za jinai hata wangekuwa ni wa kutoka nje ili kazi hiyo iwe independent nay a uhakika kweli. Kuwa na Wanasheria t u haitoshi tena kama ni wa aina ya Gosbert Blandes ambaye alisemwa toka mwanzo kuwa si msafi kimaadili mlitegemea tushangae matokeo ya kuwalinda mafisadi?
Mnafikiri ingemfaa nini mtu kama huyu Prof. Sospeter mwenye hadhi yake na kusifika duniani ambaye ndio kwanza ameteuliwa uwaziri na Rais na ni kikao chake cha kwanza aamuwe tu kuwazushia Wabunge au kuwadanganya juu ya jambo ambalo halikuwepo. Na ikimbukwe kuwa hata kabla ya kutoa hotuba yabajeti ya Wizara, hawa viongozi (Maswi na Wizara kwa ujumla walipokelewa vyema kwa kushangiliwa na wabunge wengi wakati wa utambulisho na wakati Waziri anakwenda kusoma hotuba.
Siamini haya yanayosemwa mpaka nishuhudie mwenyewe Spika akisoma maneno hayo kwamba Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara ndiwo wamekutwa na hatia tuone. Maana hii itathibisha hakika kuwa nchi yetu ina mtandao mkubwa wa kutaka mafisadi waendelee kupeta na yeyote anayejaribu kupambana nao lazima ageuziwe kibao. Nina wahakaishia kuwa hakika Bunge litagawanyika, tutakuwepo tusiokubali kutumika kuwakuwadia mafisadi kutuibia rasilimali zetu.
Nami nakubaliana na aliyetoa wazo kuwa Waziri asikubali kabisa kuomba msamaha kwa jambo ambalo hana kosa. Sisi tunasema Wizara iendelee kuboresha miundo mbinu umeme usikatike katike (mnakumbuka hao mafisadi walitabiri kuwa baada tu ya bajeti nchi yote ingeingia gizani lakini sasa tumeona hakuna mgao isipokuwa TANESCO wakikaza butu kufanya matengenezo yanayopaswa tutapata umeme wa uhakika.