Tuliwahi kuandika hapa jamvini kuwa mwishoni mwa siku ZITo ataibuka mshindi, someni nnipashe leo. sakata la wale wabunge wanaotuhumiwa kula rishwa sasa ni wazi limefikia mwisho, na badala yake PROFESA NA MWASWI ndo watuhumiwa wa kwanza kwa kupindisha taratibu za manunuzi.
Ni vema wananchi kuwaelewa viongozi wao, hasa wanapotaka kuugeuza ukweli kuwa uongo ili kushangiliwa. nani asiyejua kuwa nchi ipo kwenye mgao mkali wa umeme? lakini wafanyakazi waTanesco wameonywa kuwa endapo mtu atasema ukweli kuhusu mgao unaondelea atafukuzwa kazi.
Nchi ya waongo wanaoishi kwa kusema uongo, hata profesa anakuwa sehemu ya uongo!!!!
Sijaona uongo wa Prof Muhongo na Maswi. Alisema tangu June 2012 kwamba hakutakuwa na mgao,na kweli mpaka sasa sijaona mgao ingawa ni kiangazi. Mtoa hoja tuambie hapa huo mgao upo wapi?. Alisema bei ya kuunganishiwa umeme itashuka na kweli imeshuka-kwa sasa mtwara ukiwa na 96,000/= tu unaungiwa umeme. Alisema nguzo zetu zitokazo Mufindi zinapelewa kenya kisha tunauziwa kama imported kwa milioni moja kila nguzo ni kweli hayo tumeyaona. Sasa hapo mkweli ni nani? Aliyeondoa mgao na kupunguza gharama za umeme (whatever creativity he did) au waliokuwa wanatupa migao na hadithi kila kukicha!? Tunachopima ni shughuri zetu kutoathirika na migao na mlalahoi nae aweze kuunganishiwa umeme kwa gharama nafuu,kitu ambacho viongozi wa nyuma wa wizara na Tanesco walishindwa kufanya!