Kamati ya Ngwilizi yawatia hatiani Prof. Muhongo na Eliakim Maswi, yawasafisha Zitto na wenzake!

Its very open kwamba Muhongo na maswi walipindisha utaratibu.. swali ni, Je walipindisha utaratibu kwa manufaa ya Uma au kwa manufaa ya wanyonyaji wachache? kamati ilitakiwa kujibu hili swali na sio kushadadia upindishaji wa utaratibu

I still stand for Muhongo and Maswi

wanatuibia sana,muhongo sio mwanasiasa wameona anabana na kuziba mianya ya konakona zao za wizi wameamua kumning'iniza
 
Its very open kwamba Muhongo na maswi walipindisha utaratibu.. swali ni, Je walipindisha utaratibu kwa manufaa ya Uma au kwa manufaa ya wanyonyaji wachache? kamati ilitakiwa kujibu hili swali na sio kushadadia upindishaji wa utaratibu

I still stand for Muhongo and Maswi

well said
 
Mnajadili ripoti ambayo hamjaisoma!!!! I am amazed. Kama kuna mtu anayo aweke jamvini.
 
Hii nchi ni ya kisanii na ndio maana hatuwezi kuondoka hapa tulipo. Suala la rushwa si rahisi kuthibitishwa beyond reasonable hasa hizo kubwa kubwa (grand corruption). The principle to apply here ni ile ya mke wa Kaisari kutuhumiwa kutembea nje ya ndoa tayari ni kosa bila kutafuta ushaidi. Hawa viongozi waliotuhumiwa kula rushwa wajifikirie wafanye uamuzi kama alivyofanya Lowasa. Lakini tukianza kuunda tume kwa mamiloni ya shilingi kama ile ya jaji Ihemi ni ubadhirifu. Matokeo ya tume zote Watz tunajua pale inapoundwa tu hawana jipya. Mpeni Mwakembe muone tume inavyofanya kazi. Lowasa hatakaa aisahau maisha yake yote, maana Mwakembe anafanya kweli. Wizara ya nishati inawahusu vigogo (magogo?)ndio maana kila kitakachofanyika kitaishia kulaumiana tu. Muongo anaweza kusema uongo 50% lakini 50% nyingine ina ukweli tupu. Ebu leteni umeme wa hakika hapa, hayo malumbano yenu mtakatana hukohuko mjengoni(jumba tukufu la vioja na vijembe).
 
tuliwahi kuandika hapa jamvini kuwa mwishoni mwa siku ZITo ataibuka mshindi, someni nnipashe leo. sakata la wale wabunge wanaotuhumiwa kula rishwa sasa ni wazi limefikia mwisho, na badala yake PROFESA NA MWASWI ndo watuhumiwa wa kwanza kwa kupindisha taratibu za manunuzi. ni vema wananchi kuwaelewa viongozi wao, hasa wanapotaka kuugeuza ukweli kuwa uongo ili kushangiliwa. nani asiyejua kuwa nchi ipo kwenye mgao mkali wa umeme? lakini wafanyakazi waTanesco wameonywa kuwa endapo mtu atasema ukweli kuhusu mgao unaondelea atafukuzwa kazi. nchi ya waongo wanaoishi kwa kusema uongo, hata profesa anakuwa sehemu ya uongo!!!!

Mkuu mbona sikuelewi! Prof. alieleza kila kitu Bungeni na kwamba alipewa go-ahead na wakubwa zake baada ya kuwaelimisha kinacho endelea Wizarani in particular UNUNUZI wa mafuta machafu. Kwa nini Prof. ana andamwa kwa kufanikisha kuvunja mtandao wa ulaji ulio kithili ndani ya Shirika la Tanesco na Wizara ya Nishati; wanao jitia kumshikia bango wengi wao ni wabunge walio kuwa wapewa upendeleo wa tenda ya ku supply bidhaa za uongo na kweli kwenye shirika - baada ya kuhumbuliwa ndio sasa wanatafuta njia mbadala ya ku-get even na Prof. na mwenzake Maswi kwa kupitia migongo ya wengine.

Watanzania tumekubuhu sana katika nyanja za fitina na uzushi, Prof. kakosea nini ku-short circuit mirija ya MAFIA wa mafuta ambao wana hold TAIFA letu at rasom, wajifanya as if wao ni Govt within Govt - watu hawa ni wahuuaji tu hawana uchungu wowote na TAIFA letu - wasivyo na haya, majangili hawa walikuwa wanakwenda kununua mafuta kutoka kampuni ya BP (PUMA) alafu wanawahuzia Tanesco bei ya mwendo wa kuruka!!! Kumbuka BP(PUMA) ni kampuni yenye ubia na Serikali - logic hiko wapi hapo. Mzalendo mwenzetu Pro. Muhogo alipo gundua hilo na kulifanyia kazi FASTA, watu wasio na uchungu na TAIFA letu wanataka kumgeuzia kibao eti "ATIMULIWE KAZI" kisa? kupindisha taratibu za manunuzi!!! eti "manunuzi" my foot - tenda gani zinazo fanana ni michezo ya kuigiza!!!!!

Raisi au Waziri mkuu mwenye upeo hawezi kukubaliana na njama zenu za kupika za kutaka kumung'oa Prof.Muhogo, the guy ni mzalendo to CORE - uhamuzi alio fanya ni sahihi kabisa, wakati mwingine kiongozi anapaswa kutoa mahamuzi ya kijeshi jeshi akiona mambo ayaendi au yamegubikwa na mizengwe hisiyo ya LAZIMA - Bravo Muhongo na luteni wake - Taifa liko pamoja nanyi. Mkuu Prof na mwenzako jitayalisheni kwa kusemwa mengi na kuzuliwa MENGI, achana na WANNA BE na HAS BEEN - we chapa kazi msaidieni JK historia ndio itawahukumu.
 
wanatuibia sana,muhongo sio mwanasiasa wameona anabana na kuziba mianya ya konakona zao za wizi wameamua kumning'iniza

Ni kweli, kama ni kweli basi Ngwilizi na kamati yake watakuwa wamekamata pesa chafu ya hao waathirika wa kibano cha Muhongo na Maswi ili waje na maamuzi ya hovyo tu yasiyokuwa na manufaa kwa nchi yetu. Inabidi ifike mahali tuanze kubeba mabango na kuandamana kupinga hizi ripoti uchwara.
 
tuliwahi kuandika hapa jamvini kuwa mwishoni mwa siku ZITo ataibuka mshindi, someni nnipashe leo. sakata la wale wabunge wanaotuhumiwa kula rishwa sasa ni wazi limefikia mwisho, na badala yake PROFESA NA MWASWI ndo watuhumiwa wa kwanza kwa kupindisha taratibu za manunuzi. ni vema wananchi kuwaelewa viongozi wao, hasa wanapotaka kuugeuza ukweli kuwa uongo ili kushangiliwa. nani asiyejua kuwa nchi ipo kwenye mgao mkali wa umeme? lakini wafanyakazi waTanesco wameonywa kuwa endapo mtu atasema ukweli kuhusu mgao unaondelea atafukuzwa kazi. nchi ya waongo wanaoishi kwa kusema uongo, hata profesa anakuwa sehemu ya uongo!!!!

Ukitaka kugundua watanzania ni wavivu wa kusoma na wanapenda umbeya ndo utajua sehemu kama hizi. Mmeambiwa chanzo ni Nipashe lakini hata kusumbua akili kusoma hiyo nipashe hakuna.

Kweli mkuu umewapata wengi japo siyo 01 April
 
Ndugu zangu niliandika hapa jukwaani jinsi William lukuvi kwa kusaidiana na maswi walitengeneza zile tuhuma ili kuondoa concentration ya nini kijadiliwe kwenye bajeti ya nishati, na walifanikiwa sana, ni kweli kuna wabunge wanafanya biashara na tanesco wapo, taarifa imewataja na Bahati nzuri,wote ni ccm. Kamati haijathibitisha rushwa yeyote na badala yake inayeonekana alikula rushwa ni maswi , kwa nini aliondoka akaenda mlango wa nyuma akaipa zanuni kampuni ya puma kisa Ina bei ndogo bila kuziuliza kampuni zingine ukizingatia kuwa hapo awali puma alibid kwa bei kubwa? Sasa wameumbuka wakiwamo waliotaka kushambulia Akina zitto kisa tu wanasema sheria ifuatwe, nimeongea na j Mushi , nitaiweka hiyo taarifa ya bunge hapa wiki hii.

Afisa wenzio bafo tunasubiri hiyo taarifa. Tunaheshimu ahadi yako. Lete hiyo kitu tuidadavue mtu wangu.
 
Ripoti ya Ngwilizi yaiumbua Serikali

JUMANNE, OCTOBA 16, 2012 06:40 NA MWANDISHI WETU


ngwilizi.jpg
Mbunge wa Mlalo, Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi
*Yawasafisha wabunge waliotuhumiwa kwa rushwa
*Waziri Muhongo, Maswi sasa wakutwa na hatia
*Lukuvi adaiwa kuhaha kuizima ili kuinusuru Serikali
RIPOTI ya Kamati ndogo ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemuweka pabaya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa ripoti hiyo inadaiwa kuwakaanga viongozi hao, huku ikiwasafisha wabunge waliokuwa wakituhumiwa kwa rushwa.

Chanzo chetu cha habari kimeweka wazi kuwa umeibuka mvutano baina ya Serikali, ofisi ya Bunge na Kamati ya Nishati na Madini kuhusiana na ripoti hiyo.

Kamati hiyo iliyokuwa chini ya Mbunge wa Mlalo, Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi (CCM), imekamilisha kazi yake ya uchunguzi na tayari ripoti hiyo imekabidhiwa kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.

Kamati hiyo ilikuwa ikichunguza madai ya baadhi ya wabunge kuhongwa ili wakwamishe bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, jambo lililozua mjadala mkubwa.

Ripoti hiyo ilitarajiwa kusomwa wakati wa kikao cha Bunge kitakachoanza Oktoba 29, mwaka huu, lakini Serikali inadaiwa kuhaha kutaka kuizima ripoti hiyo isisomwe hadharani.

Baada ya uchunguzi uliofanywa na kamati hiyo, imebainika kuwa wabunge hao hawakuhusika na rushwa na badala yake ikawaweka hatiani Profesa Muhongo na katibu mkuu wake.

Pamoja na mambo mengine, ripoti hiyo inadaiwa kutoa mapendekezo ambayo yakitekelezwa kama yalivyo, itakuwa ni sawa na kuivua nguo Serikali.

Ripoti hiyo inamtaka Spika Anne Makinda kumpa dakika tano Waziri Muhongo ili aweze kuliomba radhi Bunge kutokana na kauli za uwongo ambazo zimeonekana kuwadhalilisha wabunge.

Mbali na hilo, ripoti hiyo pia imependekeza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kosa la kumpotosha waziri wake.

Mvutano baina ya Serikali, Bunge na Kamati ya Nishati na Madini umetokana na wajumbe wa kamati kubaini mkakati wa kutaka kuizima ripoti hiyo.

Chanzo hicho kilieleza kuwa mkakati huo ulianza kufahamika, kutokana na kupishana kwa taarifa kutoka Ofisi ya Bunge kwenda kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.

Inadaiwa kuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Selemani Zedi, alipata taarifa kutoka ofisi ya Katibu wa Bunge Alhamisi wiki iliyopita, ikimuarifu kuwa anatakiwa kufika Dar es Salaam Jumatatu (jana) ili kupanga ratiba ya mkutano ujao wa Bunge.

“Sasa kilichotokea ni kwamba, wakati Zedi akijiandaa na ratiba hiyo, siku ya Jumamosi akapokea taarifa kutoka ofisi hiyo hiyo ikimpa taarifa nyingine.

“Taarifa ya pili ilimweleza kuwa kikao hicho kimeahirishwa na badala yake anatakiwa kuwajulisha wajumbe wa kamati yake wajichagulie kamati nyingine ili waweze kuingizwa humo,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilisema kuwa taarifa hiyo ya pili ilichangiwa na hoja zilizotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Uratibu) Wiliam Lukuvi, ambaye alipinga ripoti hiyo kusomwa hadharani.

“Inavyoonekana Spika amekubaliana na hoja za Lukuvi za kwamba ripoti hiyo ni mbaya kwa Serikali na iwapo spika ataruhusu isomwe hadharani itaivunjia heshima.

“Ripoti imependekeza kuwa spika atoe dakika tano kwa Waziri Muhongo kuliomba radhi Bunge kwa kupotosha umma na kuwadhalilisha wabunge kwamba wamehongwa.

“Pili, ripoti imemtia hatiani katibu mkuu wa wizara kwa kutaka achukuliwe hatua za kinidhamu kulingana na taratibu za utumishi wa umma kwa kosa la kumpotosha ‘bosi’ wake.

“Wao walitaka ripoti hiyo isisomwe ili kuilinda Serikali. Utakumbuka Kamati ya Nishati na Madini ilivunjwa kutokana na tuhuma hizo za rushwa, sasa wakataka wajumbe hao wajichagulie kamati nyingine za kwenda.

“Wajumbe wote wa kamati hii wamekataa na walituma ujumbe kwenda Ofisi ya Bunge, kwamba suala hilo hawaliafiki na badala yake wanataka ripoti hiyo isomwe hadharani ili iwasafishe kwani walichafuliwa.

“Wabunge wamekataa kujichagulia kamati, kwani wao hawana mamlaka ya kujichagulia kamati, mwenye mamlaka ya kufanya hivyo ni spika, sasa iweje leo waambiwe wajichagulie kamati?” kilihoji chanzo hicho.

Hivi karibuni, Naibu Spika wa Bunge, Jobu Ndugai, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema suala la ripoti hiyo kusomwa bungeni au vinginevyo inategemea uamuzi wa Kamati ya Uongozi ya Bunge.

Ndugai alisema baada ya kamati kuwasilisha ripoti kwa Spika, Kamati ya Uongozi ya Bunge itakaa kujadili na kama itaona kuna umuhimu ripoti hiyo itaingizwa katika ratiba ya vikao vya bunge ijadiliwe.

Wakati wa mkutano wa bunge la bajeti ya mwaka 2012/13, baadhi ya wabunge walidai kuwa kuna wenzao wamehongwa na kampuni za mafuta ili kukwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

Pia katika mkutano huo ilidaiwa kuwa hatua hiyo ililenga kushinikiza Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliakim Maswi, wang’olewe katika nafasi zao kwa kukiuka Sheria ya Manunuzi wa Umma.

Kweli wadanganyika tunaweza
 
Kwa hiyo wewe unamuamini ngwilizi sio?

Mkuu watu wengine wanawasaidia sana mafisadi kwa staili hii hii ya kujaribu ku pre -empty mambo kwa maslahi wanayoyajua wao? na kwa ilivyo siasa yetu chafu huu ni mkakati maalum wa kumzoofisha Prof Muhongo, na kwa hakika watafanikiwa kama unavyoweza ona Rushwa wamekula wao (wabunge) na wanajichunguza wao, na kudai hakuna mazingira hayo huku wangali wakijua kuna mpaka ile kesi ya Jailo waziri wa nishati by that time na michango aliyoomba kwa ajili ya kuwalainisha wabunge
 
Wabunge wamejichunguza wenyewe kisha wakajisafisha

kwa uelewa wako wa elimu uliyoipata shule wabunge walitakiwa kuchunguzwa na nani? mimi nadhani hakuna sababu ya kulaumu bunge,zilaumu taasisi za uchunguzi na mashitaka ambazo zimeshindwa kufanya kazi yake!
 
Mkuu watu wengine wanawasaidia sana mafisadi kwa staili hii hii ya kujaribu ku pre -empty mambo kwa maslahi wanayoyajua wao? na kwa ilivyo siasa yetu chafu huu ni mkakati maalum wa kumzoofisha Prof Muhongo, na kwa hakika watafanikiwa kama unavyoweza ona Rushwa wamekula wao (wabunge) na wanajichunguza wao, na kudai hakuna mazingira hayo huku wangali wakijua kuna mpaka ile kesi ya Jailo waziri wa nishati by that time na michango aliyoomba kwa ajili ya kuwalainisha wabunge

kama utaweza nishawishi kwamba Muhongo na Maswi wanaweza fanya mageuzi ya msingi ktk wizara yao,basi nitakubaliana nawe kwamba 2015,CCM kitaendelea kuwa chama tawala uchaguzi ujao!!
 
tuliwahi kuandika hapa jamvini kuwa mwishoni mwa siku ZITo ataibuka mshindi, someni nnipashe leo. sakata la wale wabunge wanaotuhumiwa kula rishwa sasa ni wazi limefikia mwisho, na badala yake PROFESA NA MWASWI ndo watuhumiwa wa kwanza kwa kupindisha taratibu za manunuzi. ni vema wananchi kuwaelewa viongozi wao, hasa wanapotaka kuugeuza ukweli kuwa uongo ili kushangiliwa. nani asiyejua kuwa nchi ipo kwenye mgao mkali wa umeme? lakini wafanyakazi waTanesco wameonywa kuwa endapo mtu atasema ukweli kuhusu mgao unaondelea atafukuzwa kazi. nchi ya waongo wanaoishi kwa kusema uongo, hata profesa anakuwa sehemu ya uongo!!!!

Mimi Binafsi, niliposikia Kamati hiyo inaongozwa na Ngwilizi, nilishakata tamaa na kujiaminisha kuwa ripoti itakayo toka lazima itatetea wabunge wa CCM na kuwageuka watendaji wa Serikali. Mimi nadhani hayo mambo ni rahisi sana, wawekwe hadharani akina Maswa na Prof, pamoja na Ngwilizi na Kamati yake, kila mmoja atoe details na information walizonazo na ushahidi wake na sisi wananchi tuamue nani ni msema kweli na nani ni mwongo. Ila kwa Ngwilizi, historia itakuhukumu muda si mrefu - Shauri yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom