Kamati ya Maadili ya CCM ina wajumbe wangapi?

Ile kamati ya maadili iliyokaa siku mbili Dodoma ikiwasubiri Makamba na Kinana (pengine kwa kukosa usafiri) huku aliyetoka Mtama Lindi akiwahi, tumeambiwa iliamua kuonana na hao wazee Dar.

Lakini la ajabu, hakuna mjumbe yeyote aliyetambuliwa kuongea na hao wazee zaidi ya Mangula na Katibu Mkuu, Bashiru.

Je, haya yalikuwa mahojiano na kamati kama wanavyo aminishwa watu au yalikuwa mazungumzo ya agenda nyingine tofauti?

CCM ya sasa ikikutangazia kuwa kuna mvua kubwa inanyesha basi toka nje uhakikishe kweli kuna mvua kabla ya kuamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na eti Kinana anaonekana kwenye picha tu hakuna sehemu nyingine alikoonekana, mbona hawakutoa video clips za kufika kwake Kamati ya Maadili?

Na kwanini Makamba hawakumwonyesha?
 
Nasikia member anatafutwa kwa kulikisha maswali kwa wahojiwa Wawili kinana na makamba
 
Nakurekebisha usiyoyajua. Kamati ndogo ya usalama na maadili inaongozwa na makamu mwenyekiti wa CCM Ina wajumbe wanne lakini kamati ya usalama na maadili Ina wajumbe 12 na inaongozwa na mwenyekiti wa CCM.
Dogo tuchukulie uko sahhi, je kamati huwafuata watuhumiwa walipo na kuwafungulia milango ya magari, kisha kuwabembeleza kushuka ili ikawahoji???
huo ndo utaratibu??
 
masoudkipanya_B8aXqczlNRm.jpeg
 
Nadhsni suala hili limemalizwa kiutu-uzima baada ya wazee na wenye chama kuingilia kati kunusuru chama chao. Bila shaka kilichokuwa kinagomba ni wazee kutokubaliana na uamuzi wa kuhojiwa. Katika mwafaka uliofikiwa bila shaka kipaumbele ilikuwa ni 'damage control' na kulinda "ego" ya mamlaka kwa kuonyesha kuwa mahojiano yamefanyika.
 
Back
Top Bottom