Mkuu Mungi kwanza kabisa lengo kuu la kuanzishwa kwa hiyo kamati si jema kabisa,ni imani yangu kubwa kuwa kila mwana chit chat anapenda kuona ndoa zilizopo zinastawi na walio nje ya ndoa wanadumisha upendo baina yetu wanachit chat wote,ndio maana ikaundwa tume yangu na kamati zake ili kuhakikisha kuwa wanaoingia katika mahusiano na ndoa wanafurahia bila kuwepo kwa vitisho vya ndoa yao kuvunjwa.
Napinga kuanzishwa kwa kamati yako kutokana na WASIWASI wangu juu ya hatma ya ndoa za watu,nahofia kwamba ENDAPO HAKUTAKUWA NA MIGOGORO KATIKA NDOA NA KAMATI IPO NA LAZIMA IFANYE KAZI,Matokeo yake itakuwa ni kutafuta visababu vya kuvunja ndoa za watu ili kamati iendelee kuwa hai.
PIA tutambue kuwa sio kila ndoa inayokumbwa na mgogoro ni lazima iishie kuvunjika, kunapotokea mgogoro ndani ya ndoa sisi wadau wengine tushirikiane na wanandoa husika kutatua mgogoro baina yao lakini suala la ndoa kuvunjika au kuendelea kudumu ni la wanandoa wenyewe.ndoa inafungwa bila kusudio la kuvunjika baadae.tudumishe hilo
NDOA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.
Baba V
Mwenyekiti.