Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,162
- 10,890
Kamati iliyoahidiwa na mheshimiwa Rais Samia Suluhu ya kuchunguza corona inabidi iweke hadidu rejea zake kwa umakini bila kupendelea upande wowote.Mambo yafuatayo ni muhimu kuyaweka kwenye utafiti wao.
Jinsi corona inavyoambukiza watu wa rika tofauti na sababu zake?
Je, dawa za kiasili zinasaidia kupunguza ugonjwa huo kwa kiasi gani?
Je, ni kweli chanjo zinazotolewa zinazui corona?
Ni chanjo ipi bora zaidi kutumiwa kati ya zile za Uiengereza, Marekani, China na Urusi.
Na ni yepi madhara ya muda mrefu yatokanayo na chanjo wakati utafiti umefanyika muda mfupi.
Baada ya kujadili vitu hivyo na vyengine vingi watakavyoviingiza hapo ndipo nchi ichukue maamuzi bila kufuata shinikizo la taifa lolote na bila kupuuza baadhi ya misimamo iliyochukuliwa na hayari Rais Magufuli.
Zaidi ya hivyo hapo itakapoonekana kuna umuhimu wa Tanzania kutojitenga kama kisiwa kuhusiana na ugonjwa wa corona basi nchi yetu isikubali kupokea chanjo za bure kupitia Covax. Tanzania inunue chanjo kwa pesa zake kwani sisi si miongoni mwa mataifa masikikini tunaopaswa kupokea chanjo za bure.
Zinunuliwa chanjo chache kabisa na isiwe lazima kuchanja. Anayetaka au atakayehitajika kuchanjwa aruhusiwa kufanya hivyo na wote wengine wasilazimishwe chanjo wala kuvaa barakoa.