Kamati ya Bunge yawasilisha hoja ya fidia

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,207
4,703
Kamati ya Bunge Mambo ya Nje na Usalama imewasilisha hoja maalum katika Kamati ya Bunge ya Uongozi kuhusu migogoro ya fidia kati ya wananchi na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Jumatatu Aprili 12 2021 Spika wa Bunge Job Ndugai amewataka wabunge kuwa na subira kuhusu fidia kwa watu wenye migogoro na JWTZ.

Amesema suala hilo liliwasilishwa kwenye Kamati ya ya Bunge ya Uongozi na kwamba linatazamwa ili waweze kulipwa kabla ya Juni mwaka huu.

Ufafanuzi huo wa spika ulitokana na baadhi ya wabunge kutaka kuuliza maswali ya nyongeza baada ya maswali yaliyoulizwa na Mbunge wa Tarime(CCM) Mwita Michael.

Mbunge huyo alitaka kufahamu ni lini Serikali itaupatia ufumbuzi mgogoro wa ardhi kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na wakazi wa Mtaa wa Kinyambi na Bugosi katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.
 
Hii haituhusu, hapa bado tunajadili ukatili aliofanyiwa mh Mbowe na report ya CAG
 
Yule mnyapara angekuwepo hata kujadili fidia kwa hao watu bunge lingeogopa.
 
Back
Top Bottom