Kamati ya Bunge yabaini Mwendokasi wanajiendesha kwa hasara

We tiketi hawachani wanazungusha zinarudi tena kupitisha watu wengine. Lile shirika ni taka taka. Tutegemee ili pia siku sgr ikianza kufanya kazi.

Kwani serikali au shirika lisije na mfumo wa kadi ili kuingia mwendokasi lazima uwe na card, na card inakuwa buku.. then unakua una nunua tiketi kwa mfumo wa kadi na scanning zifanye kazi maana tangu max malipo aondokw ni mfu.

Waongeze ubunifu wangekuja na vip mwendokasi kama mdau mmoja alivyosema, seat safi, kiyoyozi.

Pia watazame upya swala lao wa nauli kuna mahali sio wa kuenda na 650, wapunguze na mida ya watu kungoja bus
 
Wakulaumiwa ni Magufuli na roho mbaya yake.. kulikuwa na mfumo mzuri sana wa kulipia kuhusu tiketi yeye na roho korosho yake akawatoa wale Maximalipo na ukawa mwanzo wa wizi wa tiketi. Pesa zinaibwa sana sijui kwanini waliua ule mfumo wa tiketi. Majaliwa kapiga mdomo kawa kimya. Bashungwa ndio mtu wa ajabu sana katembelea pale kakuta changamoto zake akampa muda meneja afanye utaratibu zimalizike. Kuna wizi sana.
Hao maxmalipo nao wezi wameipiga Sana serikali.
Watu kibao walilipa faini na tozo za magari kupitia maxmalipo na hazikusoma kwenye system wakalazimika kulipa mara mbili.
Mswahili hawezi fanya kitu kikafanikiwa.
Menejement zote tungewapa wageni
 
We tiketi hawachani wanazungusha zinarudi tena kupitisha watu wengine. Lile shirika ni taka taka. Tutegemee ili pia siku sgr ikianza kufanya kazi.

Kwani serikali au shirika lisije na mfumo wa kadi ili kuingia mwendokasi lazima uwe na card, na card inakuwa buku.. then unakua una nunua tiketi kwa mfumo wa kadi na scanning zifanye kazi maana tangu max malipo aondokw ni mfu.

Waongeze ubunifu wangekuja na vip mwendokasi kama mdau mmoja alivyosema, seat safi, kiyoyozi.

Pia watazame upya swala lao wa nauli kuna mahali sio wa kuenda na 650, wapunguze na mida ya watu kungoja bus
Gharama za kuprint Kadi tena yake itazidi buku kwa kadi
 
Hasara ni kwa kutokuwa Wabunifu...

Ongezeni ,Tengeni Ma-bus kadhaa kwa huduma ya VVIP zenye Kadi Maalumu ...Mbezi Kivukoni 3000/=
Ubungo - Posta 2000/=
Level Seat
Tutayaacha Magari Nyumbani
Level siti kwa nauli hiyo ailipi
 
Kwa mfumo wa yale mabasi kupata level seat na liondoke itakuwa ni hasara
By default yanategemea sana abiria wa kusimama as number za seats ni chache
Zinatumia mafuta kiasi gani na gharama za matengenezo zipoje Mkuu labda iwe gari ya plastic lakini kwa jinsi navyozijua gari mpaka ziharibike kwa kutembea mileage kadhaa na wewe unapata chochote sio kwa hasara hiyo inayotangazwa kila kukicha mimi ntabisha hata kodi sidhani kama wanasumbuliwa kama makampuni binafsi..
 
Wakulaumiwa ni Magufuli na roho mbaya yake.. kulikuwa na mfumo mzuri sana wa kulipia kuhusu tiketi yeye na roho korosho yake akawatoa wale Maximalipo na ukawa mwanzo wa wizi wa tiketi. Pesa zinaibwa sana sijui kwanini waliua ule mfumo wa tiketi. Majaliwa kapiga mdomo kawa kimya. Bashungwa ndio mtu wa ajabu sana katembelea pale kakuta changamoto zake akampa muda meneja afanye utaratibu zimalizike. Kuna wizi sana.
Maxmalipo si ndio hawa wakina Charamila waliopiga bilioni 2 uko Iringa?
na hao maxmalipo ndo walewale tu team moja.
 
Ngoja niwaambie kitu ambacho wengi hamkifahamu.
Taasisi za kiserikali zina posho za vikao, posho za safari, posho za overtime n.k
Hizo posho kama kampuni ingekuwa chini ya mtu binafsi hasa Muhindi asingelipa hata posho moja.
Pia watumishi wa serikali muda wote ni kutega mitego ya fedha tu ndio mawazo yao.
Mabasi yanajaza kila siku, kodi nyingi wameondolewa, foleni hawana je, hasara inakuwaje?
Basi la kawaida kutoka Kariakoo mpaka Mbezi linaweza kutumia masaa 2-3 kwaajili ya foleni na faida inapatikana.
Ila basi la mwendikasi litatumia masaa 2_3 kufanya mizynguko mpaka 4 na hasara wanapata.
 
Miradi ya serikali mingi hujiendesha kwa hasara. Huendeshwa kwa nadharia zaidi na ajira za watu wengi wasio na ufanisi wowote.
Hata SGR itakuwa hivyo hivyo.
Uthibitisho ni TRC na treni ya zamani kwa sababu abiria na mizigo itakuwa Ile ile.
Kama siyo nadharia, SGR ingejengwa baada ya reli ya zamani juonesha ufanisi mkubwa.
 
Wasimamizi wa huo mradi wenyewe kutwa wanashinda manzese wakinywa supu ya utumbo wa mbuzi na K vant..hakuna wanachofanya
 
Nadhani suluhisho serikali wange-outsource service kwa private company wao wanapata kwa kila abiria a given percentage kutoka kwenye nauli. Cha msingi malipo yawe electronically na monitoring iwe electronically pia ili serikali ipate malipo stahiki.
 
Kauli ya kamati ya bunge imeniacha hoi na mshangao sana kwamba eti kampuni ya mwendokasi inajiendesha kwa hasara

Hili nalipinga kwa nguvu zote, kwa jinsi wanavyojaza abiria na wateja wake ni wengi hakuna muda unakuta mwendokasi haijajaa sasa hizo kauli za kwamba wanajiendesha kwa hasara zinatoka wapi?
Unachopinga ni nini? Ni kitu gani serikali iliendesha kwa faida, wewe tangu upate ufahamu wako? Magari mangapi ya mwendo kasi yame pack wala hayafanyi kazi? Mara ngapi abilia wanarundamana vituoni na hasa kivukoni, wakati abiria wakiwa wamejaa wanasubiri usafiri, lakini waheshimiwa wateule wa serikali wakiwa sijui wanafanya nini? Umeona mara ngapi magari ya mwendo kasi yanaondoka kituoni yakiwa tupu bila kuchukua abiria hata kama wamejazana?

Pamoja na hayo hapo juu, unajua ujenzi wa miundombinu ya mwendokasi uligharimu na unaendelea kugharimu kiasi gani cha pesa, na unadhani itachukua muda gani kuzirejesha, pamoja na gharama za uendeshaji ili shirika lianze kutengeneza faida, ukizingatia umangi meza kwa sehemu niliouleza hapo juu?

Mwisho badilisha heading yako isomeke "Laendeshwa kwa hasara", ukisema linajiendesha ina maana "linajitosheleza".
 
Back
Top Bottom