Ndugu yangu Mizizi naomba ufafanuzi kidogo.
Humo ndani ya kikao cha kamati kuu siku hizi kuna wajumbe waalikwa?
Maana kwa nijuavyo, Si Lowasa, Chenge, wala Membe ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu.
Chenge aliwahi kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Maadili siku za nyuma, lakini kwa kanuni mpya za maadili CCM za February 2010, Mwenyekiti ni rais na wajumbe wote ni lazima wawe members wa Kamati Kuu.
Sasa napata tabu kukufuatilia, maana mara unasema Guninita haungi mkono hoja za Nape, mara Chenge kaonesha dharau za wazi kwa mwenyekiti, mara Lowasa yupo kimya wanamsemea wengine. Yani haya yote ni ndani ya kikao au vipi?
Maana kwenye wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM sioni majina ya Lowasa, Chenge, Guninita, Membe etc etc