Kamati Kuu CHADEMA yawavua Uanachama Madiwani 5 walioingia muafaka Arusha

Wakuu,Salaam.

Pamoja na mijadala inayoendelea hapa nimeona niwawekee tamko la kamati kuu ya maamuzi yalifanyika usiku wa leo kuhusu Madiwani Arusha.

Jisomee mwenyewe..

Nawatakia Majadiliano mema.

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).TAARIFA KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CHADEMA YALIYOFIKIWA KATIKA MKUTANO WA DHARURA ULIOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI/JUMAPILI TAREHE 06-07 AGOSTI 2011 KATIKA HOTELI YA IMAGI MJINI DODOMA.
Kamati Kuu ya CHADEMA ilikutana katika Mkutano wa Dharura uliofanyika siku ya Jumamosi na Jumapili tarehe 06 Agosti 2011 katika Hoteli ya Imagi Mjini Dodoma. Pamoja na mambo mengine Ilifikia maamuzi yafuatayo :

1. Kamati Kuu ilipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo iliyoyatoa katika Mkutano wake wa tarehe 17 Julai 2011 iliyowataka madiwani wa CHADEMA Arusha kujiuzulu nafasi walizozipata pamoja na kuomba radhi kwa makosa waliyoyafanya kutokana na mwafaka uliofikiwa baina yao na madiwani wenzao wa TLP na CCM kwa kuwa chama hakikuridhia wala kuutambua mwafaka huo.

2. Kamati Kuu imezingatia kuwa, kati ya madiwani 10 waliopewa maelekezo na Kamati Kuu, madiwani watano (5) ndio wametekeleza maelekezo kikamilifu wakati madiwani wengine watano (5) wamekataa kuyatekeleza maelekezo hayo.

3. Baada ya kutafakari kwa kina taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kuu, na kuwapa nafasi ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu Madiwani ambao walikuwa hawajatekeleza maelekezo,Kamati Kuu imezingatia kuwa madiwani wamekataa kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu.

Aidha, Kamati Kuu imezingatia kuwa kitendo cha madiwani kukataa kutekeleza maagizo halali ya Kamati Kuu ni utovu mkubwa wa nidhamu na ni kuvunja maadili na kanuni za chama, na kinaenda kinyume na msingi mama wa CHADEMA wa uwajibikaji.

Hivyo basi, kwa kutumia mamlaka ya Kikatiba Kamati Kuu imewafukuza uanachama madiwani watano wafuatao kwa kosa la kukataa kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu:

i) Ndugu Estomih Mallah

ii) Ndugu John Bayo

iii) Ndugu Charles Mpanda

iv) Ndugu Rehema Mohamed

v) Ndugu Reuben NgowiWatajwa hapo juu wamejulishwa maamuzi ya Kamati Kuu ndani ya Mkutano tarehe 07 Agosti 2011 saa 7:57 usiku, Aidha, kila mmoja wao atakabidhiwa barua yenye kueleza maamuzi ya Kamati Kuu.

4. Aidha, Kamati Kuu imepokea taarifa ya mazungumzo baina ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Mbowe, na Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda, juu ya nia na azima ya kumaliza tatizo la mgogoro wa umeya Arusha, waliyoyafanya asubuhi ya siku ya Jumamosi, Tarehe 06 Agosti 2011 nyumbani kwa Waziri Mkuu Mjini Dodoma.

Kamati imezingatia kuwa:

a. Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Waziri Mkuu wamekubaliana kuunda Kamati ya Kitaifa ya kushughulikia mgogoro wa umeya wa Arusha itakayojumuisha wajumbe kutoka sehemu mbili zinazohusika katika mgogoro huu ambazo ni CCM na CHADEMA

b. Kamati ya Kitaifa ya Maridhiano itaundwa haraka iwezekanavyo, na kwa vyovyote mgogoro wa u meya Manispa ya Arusha ulikubalika uishe ndani ya mwezi mmoja tangu tarehe ya mazungumzo ya Mwenyekiti wa Taifa na Waziri Mkuu

c. Uenyekiti wa Kamati ya Kitaifa utakuwa chini ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Ndugu John Tendwa, na kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa ataratibu uundwaji wa Kamati hiyo ya Kitaifa.

5.  Kamati Kuu imetambua juhudi za Waheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Mbowe, kwa hatua yao chanya ya kumaliza mgogoro wa Arusha.

6. Pamoja na hatua njema kuelekea kumaliza mgogoro wa umeya Arusha, Kamati Kuu ya CHADEMA itaendelea kusitisha kumtambua rasmi Meya wa Arusha hadi pale mazungumzo yaliyoanishwa hapo juu yatakapokamilika na mwafaka bayana kupatikana.
Imetolewa na:

Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe (Mb)

MWENYEKITI WA TAIFA

CDM kuweni makini kwa vyote mtakuwa na kazi ya ziada kuokoa KATA nne na ikitokea CCM au TLP basi ndoto ya kuwania umeya imekufa. Na shida ni umeya tu au ni ulaji tu? I am leberal viongozi wote wawe CDM au CCM ni kugombea maslahi binafsi.

Nadhani hujawajua chadema.

Kama unataka kujua sura halisi ya chadema waangalie wafuatao na ndipo utajua chadema wanataka nini na wanaelekea wapi. Kama utakuwa huwapendi hawa watu basi wewe huitakii mema nchi yetu na hii ndo chadema na huu ndiyo ukombozi wa nchi yetu. Hawa ndo kipenzi na tegemeo la watanzania wote hata wananmagamba.
1. Dr. Slaa
2. Freeman Mbowe
4. Mnyika
5. Lema
6. Msigwa
7.Mdee
8.wenje
9.Lisu
10.Nyerere
11. And All other Heros

Hawa watu ukweli miyoyo imeunganika na mioyo ya watanzania wengi na ndiyo wanawakilisha Matakwa ya jamii kubwa!

Watu hawa kila mtu hutamani kuwasikiliza kwa maana hugusa mioyo ya watu wanapoongea.

Chadema inahitaji kujenga viongozi wenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kututoa hapa tulipo leo. Hatuhitaji viongozi wenye mtazamo wa kimagamba. Tunahitaji watumishi wa watu na si watu wa kutumikia matumbo yao!

Nadhani hujawajua chadema.

Kama unataka kujua sura halisi ya chadema waangalie wafuatao na ndipo utajua chadema wanataka nini na wanaelekea wapi. Kama utakuwa huwapendi hawa watu basi wewe huitakii mema nchi yetu na hii ndo chadema na huu ndiyo ukombozi wa nchi yetu. Hawa ndo kipenzi na tegemeo la watanzania wote hata wananmagamba.
1. Dr. Slaa
2. Freeman Mbowe
4. Mnyika
5. Lema
6. Msigwa
7.Mdee
8.wenje
9.Lisu
10.Nyerere
11. And All other Heros

Hawa watu ukweli miyoyo imeunganika na mioyo ya watanzania wengi na ndiyo wanawakilisha Matakwa ya jamii kubwa!

Watu hawa kila mtu hutamani kuwasikiliza kwa maana hugusa mioyo ya watu wanapoongea.

Chadema inahitaji kujenga viongozi wenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kututoa hapa tulipo leo. Hatuhitaji viongozi wenye mtazamo wa kimagamba. Tunahitaji watumishi wa watu na si watu wa kutumikia matumbo yao!
Ukiondoa 10&11...Hao wengine sijaona walichokifanya kwa watanzania,let's raise our expectations and stop worshiping circus hollers!

Baada ya hapo nini kinaendele kwa hawo mapacha wa tano lakini kuna
taarifa kuwa watatu kati ya hawo wanatumia majani

Maamuzi ni mazuri na yanatia moyo,Big up CHADEMA.Tunaomba kujua pia ni hatua gani zimefikiwa kwa Mh Shibuda (Mb) wa Maswa.Chema cha jitembeza!Big up Kamati kuu.

ndo maana kuna umuhimu wa kuwa na wagombea binanfsi ili u-bullinism kama huu wa kina slaa na mbowe na unofanywa na ccm kwa wakina lowasa usiwe unatokea na kuwapotezea wananchi wawakilishi wao!,ushauri kwa chadema slaa aende kugombea igunga ili apate angalau kazi ya kufanya kawa idle sana!

Nenda kagombee wew huko Igunga, DR. SLAA NI kATIBU WA CHADEMA NA MAJUKUMU HAYA NI MAKUBWA NDO MAANA ANAWEZA KUWANYOSHA AKINA MALLAH!

Chama makini huteua wagombea makini na huchaguliwa na watu makini, kura zilizo wapitisha hao waliotimliwa ndizo zitakazo waptisha wagombea wengine kupitia chadema, ninaimani kuwa wana nchi wa A town hawta iangusha Chadema hata kwa kununuliwa.

Siungi mkono kwa Madiwani hawa kufukuzwa kwani kauli mbovu za Dr. Slaa ndizo zimechangia waonekane hawana nidhamu otherwise huu mgogoro ungepata watu wa Centre for Conflict Management (CCM) nadha ungemalizika vizuri.Pengine hatua hii japo ni mbovu kwangu lakini inaweza kuchochea Magamba sasa wafanye kweli kwa mafuswadi wao!japo hawapaswi kufananishwa na hawa dagaa.

Chama chako unawaita wana magamba? Nadhani kazi uliyotumwa sasa inataka kukushinda utarudisha hizo hela,laptop na modem za ccm!

Kawashauri Magamba wenzenu mfanye kama cdm maana hamna jipya kazi yenu kuiga tu toka cdm siku hizi!

Ukiondoa 10&11...Hao wengine sijaona walichokifanya kwa watanzania,let's raise our expectations and stop worshiping circus hollers!

Utaona wapi huku wewe uko Uruguru unakula mihogo tu mzee! Ukweli Morogoro bado kunahitajika nguvu ya ziada kuwavua magamba wananchi wake kama wewe unayejua na kizungu bado hujaelewa kazi ya cdm!

Swali ni jamaa wataamua kuingia CCM ili wajaribu kugombea tena?
si rahisi namna hiyo babu (kutakinzana na maslahi ya vigogo) hapo kuna uwezekano mkubwa CCM wakawa na watu wao tayari! si unajua chama kile kina wenyewe? watakachoweza kufanya ni kuwatumia katika kampeni halafu baada ya hapo wanawekwa kando!

walidhan ccm haifai walipofika CDM wakaona ndo utumbo kabisa nahsi sasa wanashukuru kwa kuvuliwa uana chama coz pengine ingekuwa ngumu kwa wao kufanya hivyo kwa aibu

mhe shibuda john mbunge wa maswa nae kwesha kwenda na maji
taarifa ziisizo rasmi anaelekea kibra

Acheni makelele, kutimua madiwani sio uamuzi mgumu hata kidogo, Mbona ZITTO muna mgwaya kila siku? Kumbukeni madiwani wapo kwa maslahi ya wananchi sio ya chama, magwanda hamna tofauti na magamba mnaweka chama mbele nchi nyuma. Hili litawatafuna sana hakuna chakushabikia hapo..........

Hongera kwa kuongeza posts ingawaje zote ni za kipuuzi kwangu.

• Thanks
Reactions: LAT

Utaona wapi huku wewe uko Uruguru unakula mihogo tu mzee! Ukweli Morogoro bado kunahitajika nguvu ya ziada kuwavua magamba wananchi wake kama wewe unayejua na kizungu bado hujaelewa kazi ya cdm!
Taja walichokifanya....Waluguru walikuwa opposition tangu enzi za Uhuru,wakati nyie mlikuwa manjagu.....Punda wee!!

kwa kosa la kuwatapeli wapiga kura wao wa arusha kumbe ni
matapeli wananchi wamewakata wapo ofs ya kata hapo chini
ya sungu sungu watuhumiwa wawili wamekimbia wananchi
wanataka michango ya maendeleo waliochanga MAPESA
waliokusanyia warudishe mara moja bila mashariti yoyote,
ngamia mzee ndiyo natoka huku kwenye mbuga ya ngoro ngoro
kwenda kuongeza nguvu

Hii ndio inaitwa nidhamu katika kufanya mageuzi ukiona kama kuna watu ambao watasumbua katika kazi ya mageuzi ni bora kuwatoa ili kazi iende kwa kuwajibika bado shibuda kiboko chake kinakuja maana alisha onekana mwanzo kuwa anashida tangu katika azimio la chama la kuondoka bungeni.

ingekua chichiemu ungesikia porojo nyingi zisizo kua na msingi wowote ni sawa na mbwa asie kua na makali ya kuuma.

Back
Top Bottom