Kamati Kuu CHADEMA yawavua Uanachama Madiwani 5 walioingia muafaka Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati Kuu CHADEMA yawavua Uanachama Madiwani 5 walioingia muafaka Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Aug 7, 2011.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mkutano wa cc ya CHADEMA ndio umeisha muda huu, wamewafukuza kwenye chama madiwani watano waliokaidi agizo la chama.

  Na kadi wamenyang'anywa

  CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).TAARIFA KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CHADEMA YALIYOFIKIWA KATIKA MKUTANO WA DHARURA ULIOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI/JUMAPILI TAREHE 06-07 AGOSTI 2011 KATIKA HOTELI YA IMAGI MJINI DODOMA.
  Kamati Kuu ya CHADEMA ilikutana katika Mkutano wa Dharura uliofanyika siku ya Jumamosi na Jumapili tarehe 06 Agosti 2011 katika Hoteli ya Imagi Mjini Dodoma. Pamoja na mambo mengine Ilifikia maamuzi yafuatayo :

  1.
  Kamati Kuu ilipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo iliyoyatoa katika Mkutano wake wa tarehe 17 Julai 2011 iliyowataka madiwani wa CHADEMA Arusha kujiuzulu nafasi walizozipata pamoja na kuomba radhi kwa makosa waliyoyafanya kutokana na mwafaka uliofikiwa baina yao na madiwani wenzao wa TLP na CCM kwa kuwa chama hakikuridhia wala kuutambua mwafaka huo.


  2.
  Kamati Kuu imezingatia kuwa, kati ya madiwani 10 waliopewa maelekezo na Kamati Kuu, madiwani watano (5) ndio wametekeleza maelekezo kikamilifu wakati madiwani wengine watano (5) wamekataa kuyatekeleza maelekezo hayo.

  3. Baada ya kutafakari kwa kina taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kuu, na kuwapa nafasi ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu Madiwani ambao walikuwa hawajatekeleza maelekezo,Kamati Kuu imezingatia kuwa madiwani wamekataa kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu.

  Aidha, Kamati Kuu imezingatia kuwa kitendo cha madiwani kukataa kutekeleza maagizo halali ya Kamati Kuu ni utovu mkubwa wa nidhamu na ni kuvunja maadili na kanuni za chama, na kinaenda kinyume na msingi mama wa CHADEMA wa uwajibikaji.

  Hivyo basi, kwa kutumia mamlaka ya Kikatiba Kamati Kuu imewafukuza uanachama madiwani watano wafuatao kwa kosa la kukataa kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu:


  i)
  Ndugu Estomih Mallah


  ii)
  Ndugu John Bayo


  iii)
  Ndugu Charles Mpanda

  iv) Ndugu Rehema Mohamed

  v)
  Ndugu Reuben Ngowi
  Watajwa hapo juu wamejulishwa maamuzi ya Kamati Kuu ndani ya Mkutano tarehe 07 Agosti 2011 saa 7:57 usiku, Aidha, kila mmoja wao atakabidhiwa barua yenye kueleza maamuzi ya Kamati Kuu.

  4. Aidha, Kamati Kuu imepokea taarifa ya mazungumzo baina ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Mbowe, na Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda, juu ya nia na azima ya kumaliza tatizo la mgogoro wa umeya Arusha, waliyoyafanya asubuhi ya siku ya Jumamosi, Tarehe 06 Agosti 2011 nyumbani kwa Waziri Mkuu Mjini Dodoma.

  Kamati imezingatia kuwa:

  a. Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Waziri Mkuu wamekubaliana kuunda Kamati ya Kitaifa ya kushughulikia mgogoro wa umeya wa Arusha itakayojumuisha wajumbe kutoka sehemu mbili zinazohusika katika mgogoro huu ambazo ni CCM na CHADEMA

  b.
  Kamati ya Kitaifa ya Maridhiano itaundwa haraka iwezekanavyo, na kwa vyovyote mgogoro wa u meya Manispa ya Arusha ulikubalika uishe ndani ya mwezi mmoja tangu tarehe ya mazungumzo ya Mwenyekiti wa Taifa na Waziri Mkuu


  c.
  Uenyekiti wa Kamati ya Kitaifa utakuwa chini ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Ndugu John Tendwa, na kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa ataratibu uundwaji wa Kamati hiyo ya Kitaifa.


  5.
  Kamati Kuu imetambua juhudi za Waheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Mbowe, kwa hatua yao chanya ya kumaliza mgogoro wa Arusha.


  6.
  Pamoja na hatua njema kuelekea kumaliza mgogoro wa umeya Arusha, Kamati Kuu ya CHADEMA itaendelea kusitisha kumtambua rasmi Meya wa Arusha hadi pale mazungumzo yaliyoanishwa hapo juu yatakapokamilika na mwafaka bayana kupatikana.
  Imetolewa na:
  ……………….
  Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe (Mb)
  MWENYEKITI WA TAIFA
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kamati kuu ya chadema imechukua maamzi mazito ya kuwafukuza madiwani watano kati ya sita baada ya mmoja kutokufika mbele ya kamati hiyo kama alivyotakiwa, ambae hajakwambwa la balaa hilo ni Crispian.. nawasilisha
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Aug 7, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Kamati kuu ya chadema imewafukuza madiwani sita waliokaidi agizo la chama kutokana na kuingia muafaka feki wa kumtambua meya wa kichina.
   
 4. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #4
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Kamati kuu Chadema leo tarehe 7/8/2011 majira ya saa saba usiku imefikia maamuzi magumu baada ya kuwafuta uanachama madiwani wasaliti watano ambao ni kama ifuatvyo , John Bayo kata ya Elirai , Estomih Malah ( Kimandolu ) , Charles Mpanda (Kaloleni) na Rehema Mohamed wa viti maalumu. Hawa ni wale baadhi ya madiwani walioingia kihuni bila kufuata utaratibu wa Chama .

  Kutokana na uamuzi huu Tume ya Uchaguzi italazimika kupanga tarehe ya uchaguzi mdogo.
   
 5. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  tunaunga mkono maamuzi hayo ya chama, sasa warudushe pesa walizohongwa.
   
 6. K

  KAMALELA JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 213
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Safi sana CHADEMA safisha uchafu wote, hao madiwani hawana nidhamu kabisa. Potelea mbali bora JESHI DOGO LENYE NIDHAMU KULIKO JESHI KUBWA LISILO NA NIDHAMU.... Mapambano bado yanaendelea.
   
 7. Elba

  Elba JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 383
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bado Shibuda... sijui watamwondoa lini mtu huyu!!!
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Aug 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Swali ni jamaa wataamua kuingia CCM ili wajaribu kugombea tena?
   
 9. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2011
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kudadeki shibuda kakalia pasi ya moto.... L
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,146
  Trophy Points: 280
  Tunasubiri jimbo letu kwa hamu kubwa sana.
   
 11. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni uamuzi wenye busara. Chadema kamwe isisite kuchukua maamuzi magumu pale inapobidi kusafisha uchafu
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa siasa za Arusha hiyo itakuwa ngumu kidogo, anywayz tusubiri tuone.......Kwa upande wangu napongeza the principled stand iliyochukuliwa na CDM.
   
 13. Elba

  Elba JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 383
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  What if wakienda mahakamani? Wanasheria tusaidieni...
   
 14. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  chadema ni chama dume kwa kweli.
  Ingekuwa CCM wangeanza kupeana siku 90 au kuogopa kupoteza nafasi hizo za udiwani.


  ili uwe msafi mbele ya jamii unayohitaji waamini kuwa wewe ni msafi basi ni lazima ujisafishe.
   
 15. m

  mtoto wa mama Senior Member

  #15
  Aug 7, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 186
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hii inaonyesha ndani ya chadema kuna watu wenye uroho wa pesa na hawana uchungu na nchi hii..,hivyo hata kama chadema itapewa nchi 2015 yatazuka yaleyale tu ya kashfa nyingi..,
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kool-aid will work better for you!!!!!!!
   
 17. opwa

  opwa Member

  #17
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 10, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cdm keep it up! We gat ur back fellas!
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #18
  Aug 7, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Vipi kuhusu Shibuda
   
 19. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ndio maana wewe ni mtoto wa mama hujui mambo. Subiri. Halafu angalia bado unanuka uvumba. Subiri subiri uwe walau menber ndio uanze kutoa hoja za namna hii.
   
 20. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #20
  Aug 7, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Ngoja tusubiri, soon mtajionea wenyewe wanachama na chama kilichopo kwa ajili ya uchaguzi.
   
Loading...