dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 22,121
- 49,376
Samahani bosi wangu; hapo kwenye red sijakupata vizuri. Tukienda kwa arguments na conclusions hizo hakuna asiye mhuni; duniani hadi Mbinguni. Mfano rahisi tu: dini zote zinazoamini uwepo wa shetani zinakubaliana kwa jambo moja kwamba hapo mwanzo huyu ambaye leo anaitwa shetani alikuwa malaika wa nuru lakini baadaye akaasi. Huwezi ku-conlude kwamba kwa kuwa malaika/shetani aliasi (UHUNI) basi na Mungu mwenyewe ni "mhuni".
Daima naamini tabia chafu (UASI, UFISADI, n.k) ni tabia ya mtu binafsi ila inapotokea mamlaka husika kwa mujibu wa kanuni na taratibu stahiki zichukue hatua bila kusita. Hata shetani/malaika alitimuliwa kutoka Mbinguni mara moja ili kuondoa uozo wake. UBARIKIWE.
Yaani unadiriki kusema kuwa Mungu ni mhuni? Ni mara yangu toka kuzaliwa kusikia jamb kama hili. Hii akili ya CHADEMA ni hatari kwa ustawi wa dunia hii.
Kwanza mimi sio CHADEMA ila kwa kuwa ume-quote post yangu; isome vizuri kisha nioneshe ni mahali gani nimesema "Mungu ni mhuni". Tumia ubongo wako wewe. Nimesema hivi:
"Huwezi ku-conlude kwamba kwa kuwa malaika/shetani aliasi (UHUNI) basi na Mungu mwenyewe ni mhuni".
Mbona unanyofoa vijimaneno kwenye sentensi yangu na kuacha maneno mengine? Usinichonganishe na Muumba wangu tafadhali.