CHADEMA
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 488
- 2,468
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo Jumamosi, Mei 9, 2020, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Freeman Mbowe, imeanza vikao vyake vya ki-digitali (Chadema Digital).
Vikao hivi vitajadili Agenda mbalimbali ikiwemo Hali ya Janga la Corona na Hali ya Siasa nchini na kufikia maazimio mbalimbali ambayo yatatolewa kwa umma baada ya vikao kukamilika.
Kufanyika kwa mfululizo kwa vikao hivi kwa njia ya mtandao, Chadema imetekeleza kwa vitendo, ushauri ambao Chama kimekuwa kikitoa kwa Serikali na Bunge katika kuchukua tahadhari ya kupunguza mikusanyiko katika kuendesha shughuli zake, ili kusaidia wahusika kujikinga dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19.
Imetolewa leo Jumamosi, Mei 9, 2020 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
Sent using Jamii Forums mobile app