Kamati Kuu CHADEMA kukutana Dar

Kamati Kuu CHADEMA kukutana Dar

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Kamati Kuu ya CHADEMA inakutana jijini Dar kuanzia tarehe 3-4 kwa kikao cha siku mbili.

Kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe na kitajadili mambo kadhaa kwa maslahi ya chama na nchi.=

=======

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa Kamati Kuu ya Chama, chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, itakutana Mei 3-4, katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama.

Katika kikao hicho cha siku mbili kitakachofanyika jijini Dar es Salaam, pamoja na masuala mengine ya kitaifa kuhusu hali ya kisiasa nchini kwa ujumla na mengine mahsusi yanayohusu uendeshaji wa chama, KK itapokea taarifa, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu;

1. Maandalizi ya Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

2. Taarifa ya ziara ya mafunzo kwa timu za kampeni, viongozi wa serikali za mitaa na chama, kukiandaa chama kushinda dola na kuongoza serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

3. Taarifa za utendaji wa chama kupitia kanda zote 10, Tanganyika na Zanzibar.

4. Taarifa ya maendeleo ya mikakati ya kushiriki uchaguzi mkuu kwa kushirikiana na vyama 4 vinavyounda UKAWA.

5. Taarifa za mwenendo wa shughuli ya uandikishaji wa wapiga kura (upya) katika daftari la kudumu kwa teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) na hatma ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Imetolewa leo Jumamosi, Mei 2, 2015 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara a Habari na Mawasiliano- CHADEMA
 
Kamati Kuu ya CHADEMA inakutana jijini Dar kuanzia tarehe 3-4 kwa kikao cha siku mbili.

Kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe na kitajadili mambo kadhaa kwa maslahi ya chama na nchi.
Asante sana kamanda kwa taarifa tupo pamoja
:yo:
 
Inaonyesha issue ya kugawana majimbo Ukawa haijakaa vizuri
 
Hivi huyu binadamu ni mwanachama/mfuasi/shabiki wa CCM au ACT-Tanzania/Wazalendo? Unavyowa-sapport wote huoni kama unajichanganya?

Nisome tena, kisha jibu swali, hivi shule ulienda kusomea ujinga?

quote_icon.png
By FaizaFoxy
Watamjadili Khalid Kagenzi?

Watanzania, chama chetu kiongozi tarajiwa kiko kazini kikiendelea kujiimarisha na kujipanga. Mwaka huu CCM wanalo. Jamaa wana wakati mgumu, hadi wanafikiria kuahirisha uchaguzi mkuu, aisee!

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

C:\Users\hp\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image002.jpg

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa Kamati Kuu ya Chama, chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, itakutana Mei 3-4, katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama.

Katika kikao hicho cha siku mbili kitakachofanyika jijini Dar es Salaam, pamoja na masuala mengine ya kitaifa kuhusu hali ya kisiasa nchini kwa ujumla na mengine mahsusi yanayohusu uendeshaji wa chama, KK itapokea taarifa, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu;

1. Maandalizi ya Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

2. Taarifa ya ziara ya mafunzo kwa timu za kampeni, viongozi wa serikali za mitaa na chama, kukiandaa chama kushinda dola na kuongoza serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

3. Taarifa za utendaji wa chama kupitia kanda zote 10, Tanganyika na Zanzibar.

4. Taarifa ya maendeleo ya mikakati ya kushiriki uchaguzi mkuu kwa kushirikiana na vyama 4 vinavyounda UKAWA.

5. Taarifa za mwenendo wa shughuli ya uandikishaji wa wapiga kura (upya) katika daftari la kudumu kwa teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) na hatma ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Imetolewa leo Jumamosi, Mei 2, 2015 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara a Habari na Mawasiliano- CHADEMA
 
Watamjadili na John Mnyika baada ya kutangaza bila ya kushauriana na viongozi wenzake kuwa adui wao Namba Moja ni Zitto Kabwe?
 
Wakumbeke kuwa chuki hazijengi, ACT wameulizia taratibu za ukawa waache upuzi wao wa mtu mmoja mbowe,
 
Kila kheri CHADEMA chama kubwa chini ya makamanda makini, sasa chama kimetulia swafi kama maji ya mtungini yale magugu yote ya kisaliti tumetupa kule waliobakia na wakombozi tu wenye uchungu na nchi.

VIVA CHADEMA
 
Watamjadili na John Mnyika baada ya kutangaza bila ya kushauriana na viongozi wenzake kuwa adui wao Namba Moja ni Zitto Kabwe?
Watajiuliza kumbe ztt ana nafasiyake pale na watamlaum sana mbowe kwa kuendekeza chuki za kinafik
 
Back
Top Bottom