KAMATI KUU CCM yawafunga midomo KAMATI KUU CDM

KAMATI KUU CCM yawafunga midomo KAMATI KUU CDM

"Hakuna kitu kibaya sana kama njaa ya asubuhi"
 
NIMEJARIBU KUSUBIRI KWA HAMU KUBWA TAMKO LA CDM, hasa baada ya move nzuri ya kuwabana mawaziri kupitia kwa waziri mkuu bungeni wawajibike, nilitegemea kabisa baada ya CC ya CCM< kamati kuu au baraza Kuu la CDM Taifa wangekuja na mkakati wa nyongeza kwa kile walichokianzisha bungeni.... lakini kwa maajabu ya mwaka baada ya Nape kusema kilichoamualiwa na CC ya CCM CDM wakanywea kama vile wamemwagiwa maji vile... Huu ni udhaifu mkubwa katika medani ya vita... ukimpiga adui kwa kutumia silaha flani akarudi nyuma, husimami hapo unasonga mbele kwa kutumia silaha nyingine inayofaa zaidi....kitendo cha CDM kusimama na kubaki kurudia kile walichosema CCM talalila ya MFUMO ni udaifu mkubwa kwa uongozi. Au mnataka tuamini ile stori ya kuwa hamkuelewana ndani ya Kamati kuu juu ya nanai hasa mmiliki wa hoja? ( kwamba hoja ilikuwa ya Zitto tu tena kwa kupewa na wabunge wa CCM bila kuwa na baraka za Chama Zitto akaibeba??!!!

Gizakuu

Join Date : 29th April 2012
Posts : 9
Rep Power : 302
Likes Received 7
Likes Given 0
TAFAKARI

Gizakuu, shida ni giza kuu limekutanda hata huoni chochote. Kama macho hayaoni kwa sababu ya giza kuu, nakushauri ujitahidi kutumia masikio yako utapata majibu ya maswali yako. Kwa kifupi, CDM haiendeshwi na Kamati kuu ya CCM kiasi kwamba isubiri tamko la CC ili ijipange. Ninachojua mimi ni kuwa kuna hoja kwa Spika wa Bunge la kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu. Hadi hapo mawaziri waliotuhumiwa kufuatia ripoti ya CAG watakapowajibishwa, tunachosubiri ni hatua zaidi baada ya siku 14. Kwa hiyo, taarifa ya CC, haijajibu hoja ya msingi. Mwenyekiti wenu wa Taifa presha inampanda na kushuka ya namna gani afanye kabla siku 14 haizijaisha. Leo ni siku ya 9 bado 6.
 
Magamba ni mabingwa wa kuiga kunya kwa tembo..watapasuka msamba mwishowe. Wako remote controlled na CDM kwa sasa. Kila wanacho fanya wanaangalia response itakuwaje kwanza. Baada ya kuona hoja ya kuwajibisha PM inashika kasi na kama isipofanyika basi nguvu ya umma itashika hatamu wakaogopa.

Kumbukeni wabunge wa magamba walikuwa ni kulalamika tu wakati wakichangia hoja zao pasipo kutoa way forward, baada ya kuona hoja ya Zitto inashika kasi ndipo nao wakaitisha CC haraka ili kuonyesha umma kuwa walikuwa na dhamira ya kushughulikia suala hilo.

Sasa ili kuonyesha kuwa hoja hiyo ilikuwa siyo yao mtaona UTEKELEZAJI WAO HASA KATIKA KUWAPELEKA MAWAZIRI WENYE TUHUMA MAHAKAMANI NA KUWATIA HATIANI. Hizi hatua wanazichukua kwa mashinikizo siyo dhamira yao.
 
Ukweli ni kwamba Hoja ya kuiwajibisha serikali iliibuliwawaa na wabunge wa CCM . Zitto kama kawaida yake akadandia Hoja ya wana CCM ili kujitafutia umaarufu. Timing ya Kamati kuu ya CCM imewaacha Chadema midomo wazi. Gharma ya kudandia Hoja za Watu bila utafiti.
wewe mwehu namba moja,mbona hawakuzungumza chechete walibaki kua mabubu mpaka zito alipo sema wapige kura za kutokua na imani pm ndipo na wao wachache waka onekana?
 
Ukweli ni kwamba Hoja ya kuiwajibisha serikali iliibuliwawaa na wabunge wa CCM . Zitto kama kawaida yake akadandia Hoja ya wana CCM ili kujitafutia umaarufu. Timing ya Kamati kuu ya CCM imewaacha Chadema midomo wazi. Gharma ya kudandia Hoja za Watu bila utafiti.

hivi huwa unafatilia bunge kwa makini au unasubiri magazeti yenu yale??
iweje wenye hoja wasaini watano (5) tu???
Laiti mngejua wananchi walivyolipokea hili jambo msingeendelea kujidanganya na hizi hadithi za kusadikika.
 
NIMEJARIBU KUSUBIRI KWA HAMU KUBWA TAMKO LA CDM, hasa baada ya move nzuri ya kuwabana mawaziri kupitia kwa waziri mkuu bungeni wawajibike, nilitegemea kabisa baada ya CC ya CCM< kamati kuu au baraza Kuu la CDM Taifa wangekuja na mkakati wa nyongeza kwa kile walichokianzisha bungeni.... lakini kwa maajabu ya mwaka baada ya Nape kusema kilichoamualiwa na CC ya CCM CDM wakanywea kama vile wamemwagiwa maji vile... Huu ni udhaifu mkubwa katika medani ya vita... ukimpiga adui kwa kutumia silaha flani akarudi nyuma, husimami hapo unasonga mbele kwa kutumia silaha nyingine inayofaa zaidi....kitendo cha CDM kusimama na kubaki kurudia kile walichosema CCM talalila ya MFUMO ni udaifu mkubwa kwa uongozi. Au mnataka tuamini ile stori ya kuwa hamkuelewana ndani ya Kamati kuu juu ya nanai hasa mmiliki wa hoja? ( kwamba hoja ilikuwa ya Zitto tu tena kwa kupewa na wabunge wa CCM bila kuwa na baraka za Chama Zitto akaibeba??!!!
TAFAKARI

Pana watu humu Kama huyu mtoa mada,wasipolitaja ama kuliandika jina la Chadema basi hawali wala kwenda chooni.Nani amekuambia Chadema wapo kimya?Tatizo mnakurupuka sana ninyi mnaotumwa Kama majini kuja kuchafua chafua hali ya hewa humu jamvini.
 
Kwa mtu makini ni lazima apate wasiwasi juu ya uwezo wa JK kwani uwezo wa kuwawajibisha hao mawaziri upo chini yake lakini kwa kuwa ni mtu ambaye hajiamini alienda kuomba huruma ya CC yake na yeote hii ni kujikosha kwa marafiki zake (mawaziri watuhumiwa ambao inaelekea huo uchafu naye anahusika) kwamba alijaribu kuwatetea ila chama ndiyo kimeamua.
 
Hivi wewe giza tororo naubongo wako uko kwenye giza?hivi hata kusikia chadema wanafanya nini husikii hata kuambiwa sisi tunawashitaki kwa wananchi!!umeona tanga Rais wenu kapokelewa na CUF na CDM pole Giza Tororo lakini hapa hauwezi tupo wengi ndani maanishi wingi kwa namba namaanisha mwanachama mmoja wa CDM ni vichwa kumi vya Magamba!!Tafakari hivyo huwezi katu humu ni mwisho ne Michuziblog
 
Wakurupukiaji wa mambo mnao wengi huko CCM kwa mfano Salva Rweyemamu, hiyo siyo hulka ya movement ya ukombozi na mabadiliko, suala linapimwa na kuchunguzwa kwanza kisha linashughulikiwa; mambo hayaendeshwi kwa matamko.
 
NIMEJARIBU KUSUBIRI KWA HAMU KUBWA TAMKO LA CDM, hasa baada ya move nzuri ya kuwabana mawaziri kupitia kwa waziri mkuu bungeni wawajibike, nilitegemea kabisa baada ya CC ya CCM< kamati kuu au baraza Kuu la CDM Taifa wangekuja na mkakati wa nyongeza kwa kile walichokianzisha bungeni.... lakini kwa maajabu ya mwaka baada ya Nape kusema kilichoamualiwa na CC ya CCM CDM wakanywea kama vile wamemwagiwa maji vile... Huu ni udhaifu mkubwa katika medani ya vita... ukimpiga adui kwa kutumia silaha flani akarudi nyuma, husimami hapo unasonga mbele kwa kutumia silaha nyingine inayofaa zaidi....kitendo cha CDM kusimama na kubaki kurudia kile walichosema CCM talalila ya MFUMO ni udaifu mkubwa kwa uongozi. Au mnataka tuamini ile stori ya kuwa hamkuelewana ndani ya Kamati kuu juu ya nanai hasa mmiliki wa hoja? ( kwamba hoja ilikuwa ya Zitto tu tena kwa kupewa na wabunge wa CCM bila kuwa na baraka za Chama Zitto akaibeba??!!!
TAFAKARI

Angalia hapo kwenye red, hivi vita ilikuwa inahusu nini? hoja ilikuwa nini kwani? Hivi ukiwa unaanda siraha kumuua adui yako na kabla ya kushoot huyo huyo apapigwa kifadulo akafa hivi utaandaa mashambulizi gani dhidi yake?
Ndugu Gizakuu nadhani uanaona giza kuu kweli na si ajabu wewe ni CYLIL CHAMI na unayo haki ya kuona giza kuu. Tunaweza kusema kuwa vita ya kwanza hiyo CDM mshindi sasa imebaki vita phase two ya kuondoa CCM katika nafasi yake. CCM itakosa hata sifa ya kuwa chama cha Upinzani maana hakijasajiriwa na mpaka waupate jasho litawatoka kwa kukosa wanachama kama CCJ. Tumia Bongo Bwanaaaaaa!
 
wewe kweli ni GIZAKUU na huko uliko Gizani endelea kukaa hukohuko hujui wala huelewi kinachoendelea huku duniani hasa Tz, kama hiyo hoja ilianzishwa na ccm ni nini kiliwafanya wasiendelee nayo? Fuatilia mambo uwe na evidence za kweli unapotoa hoja siyo unakurupuka ukiona mwanga from Gizakuu
 
huyu amekurupuka tu,jana mh Mnyika alitoa taarifa ya maazimio ya kamati kuu ya chama ambayo pamoja na mambo mengine ni kushinikiza waliofuja mali ya uma wachukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na wale wa kashfa za richmond,sasa nashangaa huyu jamaa anakurupuka tu wakati hata habari zenyewe hafuatilii
 
So ulitaka cdm wafanyeje? wawafukuze mawaziri? au wabariki maamuzi ya cc ya magamba? do u think cdm ni wakurupukaji kiasi hicho? kumbuka walisema wataenda kwa wananchi kama mawaziri hawatawajibishwa ccm wakaitisha kikao cha cc ghafla, timing vitani ni pamoja na kuangalia adui anatumia mbinu gani na si kubadili silaha tu, cc ya ccm imelazimishwa na cdm kuketi tunachoamini na kinachoonekana cdm wapo makini kuliko ccm yaelekea mambo yanayoendelea nchi hii wewe ni mgeni nayo, NAAMINI na utaona cdm wanasubiri hilo baraza jipya watoe mwelekeo mwingine then you will realize how smart they are.
 
Ukweli ni kwamba Hoja ya kuiwajibisha serikali iliibuliwawaa na wabunge wa CCM . Zitto kama kawaida yake akadandia Hoja ya wana CCM ili kujitafutia umaarufu. Timing ya Kamati kuu ya CCM imewaacha Chadema midomo wazi. Gharma ya kudandia Hoja za Watu bila utafiti.

Vumbi jingine!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
NIMEJARIBU KUSUBIRI KWA HAMU KUBWA TAMKO LA CDM, hasa baada ya move nzuri ya kuwabana mawaziri kupitia kwa waziri mkuu bungeni wawajibike, nilitegemea kabisa baada ya CC ya CCM< kamati kuu au baraza Kuu la CDM Taifa wangekuja na mkakati wa nyongeza kwa kile walichokianzisha bungeni.... lakini kwa maajabu ya mwaka baada ya Nape kusema kilichoamualiwa na CC ya CCM CDM wakanywea kama vile wamemwagiwa maji vile... Huu ni udhaifu mkubwa katika medani ya vita... ukimpiga adui kwa kutumia silaha flani akarudi nyuma, husimami hapo unasonga mbele kwa kutumia silaha nyingine inayofaa zaidi....kitendo cha CDM kusimama na kubaki kurudia kile walichosema CCM talalila ya MFUMO ni udaifu mkubwa kwa uongozi. Au mnataka tuamini ile stori ya kuwa hamkuelewana ndani ya Kamati kuu juu ya nanai hasa mmiliki wa hoja? ( kwamba hoja ilikuwa ya Zitto tu tena kwa kupewa na wabunge wa CCM bila kuwa na baraka za Chama Zitto akaibeba??!!!
TAFAKARI

[h=2]
icon1.png
Taarifa ya Kikao Cha Baraza Kuu- CHADEMA by Mnyika[/h]
BARAZA Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) limesema kuwa mabadiliko ya baraza la mawaziri yanayotarajiwa kufanyika wakati wowote si suluhu ya kupunguza au kumaliza ubadhirifu serikalini kwa madai kuwa ufisadi ni sehemu ya mfumo wa utawala wa CCM.

Aidha kuvunjwa kwa baraza la mawaziri kwa kuepuka ushauri wa wabunge na kutumia kauli ya Kamati Kuu ya CCM, ni matokeo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kuhofia nguvu ya umma.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, alibainisha hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari akielezea maazimio ya baraza hilo lililomaliza kikao chake juzi.

Mnyika alieleza kuwa mabadiliko hayo hayataleta mageuzi ya maana kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete bado atateua sehemu kubwa ya mawaziri waliopatikana kifisadi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

“Kauli ya CCM kuwa watawapeleka mahakamani mawaziri na watendaji wote waliohusika katika ubadhirifu ni siasa tupu, kwani ushahidi uko wazi kuwa mpaka sasa serikali hiihii chini ya chama hichohicho haijawapeleka mahakamani mawaziri waliopatikana na kashfa na kulazimika kujiuzulu mwaka 2008 na wameshindwa kuwafukuza kwenye chama.

“Zaidi ya hayo, kuna orodha ndefu ya mafisadi iliyotolewa hadharani mwaka 2007 na mafisadi wakuu hawajagushwa,” alisema.

Alieleza kuwa CCM iliitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu na kutoa tamko juu ya baraza la mawaziri baada ya kusikia kuwa Baraza Kuu la chama hicho linakutana na kuanza maandalizi ya kuunganisha nguvu ya umma kushinikiza mabadiliko ya kiutawala na mfumo.

“…ni wazi kuwa CCM na Rais Jakaya Kikwete wamekubali kufikia hatua hiyo wakihofia nguvu ya umma.

“Baraza Kuu limeazimia kuwataka Watanzania kutambua kuwa kwa muda mrefu sasa baraza la mawaziri limekuwa kielelezo kamili cha mfumo wa ubadhirifu, rushwa na ufisadi katika utawala wa nchi hii chini ya CCM,” alisema Mnyika.

Alisema chama hicho si cha msimu wala matukio na kwamba wanahitaji uwajibikaji mkubwa nchini na kuongeza kuwa operesheni za chama hicho nchi nzima hazitakwisha.

“Operesheni zetu ziko palepale, tunahitaji mabadiliko ya mfumo, kwani kuna uozo mkubwa kwenye safu za uongozi,” alisema Mnyika wataunganisha nguvu ya umma na kujenga chama katika operesheni hizo.

Hali ya uchumi

Mnyika alisema kuwa baraza hilo limebaini kuwa hali hiyo inasababishwa na uongozi dhaifu wa serikali ya CCM ambayo imeshindwa kudhibiti matumizi mabaya katika serikali na idara zake na kushindwa kuchochea uzalishaji wa chakula na nishati nchini.

Alisema kuwa baraza hilo limeuagiza uongozi wa taifa wa CHADEMA pamoja na wabunge kuwahimiza wananchi kuendelea kuishinikiza serikali kutimiza wajibu wake.

Pamoja na hilo, alisema baraza hilo limewataka wananchi kujiandaa kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi na utawala katika chaguzi zijazo, kwani kikwazo kikubwa cha maendeleo nchini ni CCM inayoendesha serikali kwa mfumo wa rushwa na ufisadi.

Mnyika aliongeza kuwa mabadiliko ya kweli nchini yatapatikana kwa kuiondoa CCM madarakani.

Mauaji ya wanachama

Baraza hilo limelaani mauaji ya wanachama wake huku jeshi la polisi likishindwa kuchukua hatua zozote za maana.

“Baraza Kuu limelaani mauaji ya Mwenyekiti wa Kata ya Usa River yaliyotokea Aprili 28 mwaka huu na pia limeeleza kusikitishwa na jeshi la polisi kwa kushindwa kuchukua hatua za maana dhidi ya watu waliohusika na mauaji ya wanachama wa CHADEMA ambayo yamekuwa yakitokea tangu uchaguzi mdogo wa Igunga,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, alisema baraza hilo limeuagiza uongozi wa chama hicho kuanzisha mchakato wa kulishtaki jeshi la polisi kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake.

Aidha pamoja na hayo, alisema baraza hilo limeagiza chama kusukuma hoja ya kuwapo kwa uchunguzi huru dhidi ya matendo ya kidhalimu yanayofanywa na Jeshi la Polisi na kutolea mfano Arusha, Mwanza, Ruvuma Mbeya na Mtwara (Tandahimba).

Uchaguzi ndani ya chama

Mnyika alisema kikao hicho kimepanga uchaguzi ndani ya chama hicho kufanyika kuanzia Juni mwaka huu kwa ngazi ya msingi na kukamilika Oktoba mwakani kwa ngazi ya taifa.

alisema katika kudhibiti rushwa katika uchaguzi huo, baraza kuu limeiagiza Kamati Kuu kuandaa mwongozo wa kudhibiti hali hiyo, ili kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa uadilifu na maadili.

Masuala ya kijamii

Aidha alisema baraza hilo limeitaka serikali ya CCM kutekeleza tamko la chama hicho kutatua migogoro ya makundi ya kijamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wakulima hasa katika masuala ya ardhi na maslahi ya wafanyakazi.

Alisema kuwa mpaka sasa serikali bado haijapandisha mishahara ya wafanyakazi na kusema kuwa hali hiyo ndiyo inayochangia kuwapo kwa migogoro ya mara kwa mara.

“Tunaamini rasilimali na mapato ya nchi yakitumika vizuri yanaweza kutekeleza mambo haya na wafanyakazi wakawa na maslahi bora,” alisema.​
 
Nimeshindwa kucomment kutokana na jina lako mimi huamini kuwa jina hureflect mtu mwenyewe
 
Ukweli ni kwamba Hoja ya kuiwajibisha serikali iliibuliwawaa na wabunge wa CCM . Zitto kama kawaida yake akadandia Hoja ya wana CCM ili kujitafutia umaarufu. Timing ya Kamati kuu ya CCM imewaacha Chadema midomo wazi. Gharma ya kudandia Hoja za Watu bila utafiti.

ilibidi adandie maana wabunge wa ccm wasingeweka hoja ya kutokua na imani na waziri wao mkuu so somebody from the opposition had to do it and he was brave enough to do what he did.
 
NIMEJARIBU KUSUBIRI KWA HAMU KUBWA TAMKO LA CDM, hasa baada ya move nzuri ya kuwabana mawaziri kupitia kwa waziri mkuu bungeni wawajibike, nilitegemea kabisa baada ya CC ya CCM< kamati kuu au baraza Kuu la CDM Taifa wangekuja na mkakati wa nyongeza kwa kile walichokianzisha bungeni.... lakini kwa maajabu ya mwaka baada ya Nape kusema kilichoamualiwa na CC ya CCM CDM wakanywea kama vile wamemwagiwa maji vile... Huu ni udhaifu mkubwa katika medani ya vita... ukimpiga adui kwa kutumia silaha flani akarudi nyuma, husimami hapo unasonga mbele kwa kutumia silaha nyingine inayofaa zaidi....kitendo cha CDM kusimama na kubaki kurudia kile walichosema CCM talalila ya MFUMO ni udaifu mkubwa kwa uongozi. Au mnataka tuamini ile stori ya kuwa hamkuelewana ndani ya Kamati kuu juu ya nanai hasa mmiliki wa hoja? ( kwamba hoja ilikuwa ya Zitto tu tena kwa kupewa na wabunge wa CCM bila kuwa na baraka za Chama Zitto akaibeba??!!!
TAFAKARI
Hivi mwanao ukimtuma dukani, akabisha halafu baadaye akaenda ndo anakuwa amekufunga mdomo. Kama kufungwa mdomo ni kwa kutekelezewa ninachokitaka, basi naushona kabisa.
 
Back
Top Bottom