Kamati Kuu CCM moto, baridi leo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati Kuu CCM moto, baridi leo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 20, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete.


  Mwandishi Wetu

  KAMATI Kuu (CC) ya CCM leo inakutana jijini Dar es Salaam, huku chama hicho tawala kikikabiliwa na mtihani wa kutanzua baadhi ya migogoro ya chinichini inayowahusisha baadhi ya makada wake pamoja na matukio makuu ya kisiasa yaliyojitokeza nchini.

  CCM katika kikao muhimu cha ambacho ni cha tatu tangu kufanyika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana, inatarajiwa pamoja na mambo mengine kujadili hali ya kisiasa nchini.

  Kwa mujibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, chama hicho kitakutana chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ajenda kuu za mkutano huo, ni pamoja na kujadili hali ya kisiasa nchini, maandalizi ya Sherehe za Miaka 37 ya CCM na kupokea taarifa mkutano wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika.

  Mkutano huo ambao CCM iliwakilishwa ulifanyika mjini Luanda, Angola kuanzia Desemba 7 hadi 10 mwaka jana.

  Hata hivyo, CCM pamoja na kuweka bayana ajenda hizo, habari za kidadisi za kisiasa ndani ya chama hicho zimeweka bayana mambo mengine yanayoweza kujitokeza katika mjadala wa hali ya kisiasa, ajenda inayopewa umuhimu mkubwa katika kikao hicho CC.

  Kwa mujibu wa duru hizo za kidadisi za siasa ndani ya CCM, mambo hayo ni pamoja na kusudio la mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, kutaka kuwasilisha hoja akimshitaki Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kutokana na kile alichokiita ni "kukirarua chama nje ya vikao".

  Mgeja alitangaza kusudio hilo baada ya Sitta ambaye alikuwa spika wa Bunge la Tisa, kuweka bayana msimamo wake akipinga malipo ya Sh94 bilioni kwa Kampuni ya Dowans.

  Sitta ambaye amefungua pazia kwa mawaziri kupinga hadharani mipango inayotiliwa shaka na umma, tofauti na utaratibu wa kawaida wa kulindana serikalini, anatarajiwa kukabiliana na wakati mgumu kutoka kwa makada wenye kuamini katika maslahi ya chama kushika hatamu ya dola.

  Duru hizo ziliongeza kwamba, jambo la pili linaloweza kutikisaa chama hicho kwa leo ni pamoja na mvutano wa umeya katika jiji la Arusha.

  Katika mvutano huo, CCM mbali ya kuvutana na chama cha upinzani na maaskofu, bado pia makada wake akiwemo Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa, alitaka chama hicho tawala kifanye mazungumzo na Chadema.

  Ingawa Lowassa si mjumbe wa CC kwa sasa, ajenda hiyo inatarajiwa kuingizwa katika mjadala wa ajenda kuu ya hali ya kisiasa.

  Kauli ya Lowassa kutaka suluhu kati ya Chadema na CCM akitahadharisha Arusha kugeuka Ivory Coast, ilipingwa na Katibu Mkuu wake, Yusuph Makamba aliyetaka wapinzani hao waende mahakamani huku kada maarufu, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu mzee Cleopa Msuya, akiunga mkono akisema hakuna haja ya mazungumzo kwani hiyo ni sheria inapaswa kutafsiriwa mahakamani.

  Duru hizo ziliongeza kwamba, katika ajenda hiyo ya Arusha CCM inatarajiwa kuangalia athari za udini zilizoanza kujitokeza baada ya baadhi ya mashekhe na maaskofu kupingana, huku chama hicho tawala kikiingia kwenye malumbano na baadhi ya maaskofu.

  Katika ajenda hiyo, wadadisi wanaangalia kikao hicho kama muhimu kuangalia vurugu zilizotokea Arusha, hali halisi baada ya vurugu, njia ya kutatua tatizo hilo na nguvu zilizotumiwa kati ya polisi na Chadema.

  Wadadisi hao wa siasa ndani ya CCM, wanataja jambo jingine ni pamoja na chama kujitathimini baada ya kupigwa kwenye ngome muhimu za majimbo ikiwemo Nyamagana, Ilemela Mwanza, Maswa Magharibi Shinyanga, Arusha Mjini, Hai, Moshi Mjini, Singida Kusini, Mbeya Mjini, Kawe na Ubungo jijini Dar es Salaam.

  Mapema wiki iliyopita akizungumza na gazeti hili, Mzee Msuya alisema chama hivi karibuni kingekaa na kujitathmini namna kilivyotikiswa kwenye ngome zake muhimu za kisiasa.

  CCM tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya awamu ya nne, kimejikuta kikipigwa na mawimbi mazito yanayotokana na mpasuko kati ya genge la watuhumiwa wa ufisadi na wapambanaji wa ufisadi, ambao wameasi kutoka kundi moja la mtandao baada ya kupingana kimsimamo.


   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Kamati Kuu CCM kuketi Dar leo


  Na Tumaini Makene

  SAKATA la Kampuni 'tata' ya Dowans inayotakiwa kulipwa mabilioni ya fedha na serikali baada ya kushinda katika Mahakama ya usuluhishi wa Biashara (ICC) na vurugu za kisiasa za Arusha, ni mambo yanayotarajiwa kutinga katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) inayotarajiwa kuketi leo.

  Wachambuzi wa masuala ya siasa nchini waliozungumza na Majira jana juu ya kikao hicho ambacho ni moja ya vikao nyeti na vya ngazi ya juu katika uendeshaji na ufikiaji wa maamuzi ya chama hicho, wamesema kuwa ni vigumu kwa CC kutozungumzia sakata la Dowans ambalo kwa sasa ni moja ya mijadala iliyochukua nafasi kubwa katika duru za siasa nchini.

  Ugumu huo, kwa mujibu wa wachambuzi hao, unatokana na ukweli kuwa sakata hilo mbali ya kuwa limevuta hisia za watu mbalimbali na kuibua mijadala mikali nchini, kila wananchi wa kada mbalimbali wakitoa maoni yao tofauti tofauti, limewagawanya baadhi ya viongozi waandamizi serikalini na ndani ya CCM yenyewe.

  Pia mkutano huo umeitishwa muda mfupi tu baada ya kuibuka mgogoro wa umeya Arusha, ambapo CHADEMA walipinga uchaguzi ulioipa ushindi CCM, na kuamua kufanya maandamano ya amani yaliyozimwa kwa risasi na polisi hadi watu watatu wakauawa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa.

  Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM, CC itakutana leo Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete katika kikao chake cha tatu tangu kufanyika uchaguzi mkuu mwaka jana, ambapo kinatarajiwa kuwa na ajenda tatu.

  "Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, itakutana tarehe 20 Januari, 2011 mjini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete. Katika kikao hicho, Kamati Kuu pamoja na mambo mengine, itapokea na kujadili mambo yafuatayo;

  "Hali ya kisiasa nchini, maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 34 na matembezi ya mshikamano na kupokea taarifa ya mkutano wa makatibu wakuu wa vyama vya ukombozi kusini mwa Afrika uliofanyika mjini Luanda, nchini Angola kuanzia tarehe 7-10 Desemba, 2010, ambao Chama Cha Mapinduzi kiliwakilishwa," ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya CCM.

  Kikao hicho kinafanyika siku chache baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana chini ya mwenyekiti wake, Rais Kikwete, ambacho taarifa zinasema suala la Dowans kulipwa mabilioni ya fedha, ni moja ya hoja zilizopata nafasi kubwa kujadiliwa barazani, ambapo kumekuwepo na mgawanyiko wa wazi na wa chini chini, kundi moja likipinga, lingine likiunga mkono serikali kutekeleza uamuzi wa ICC.

  Suala jingine kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya siasa waliozungumza na Majira ni juu ya mjadala mwingine mkali wa katiba mpya, ambapo imeanza kudaiwa kuwa CCM kinaonekana kukosa mtu wa kuzungumzia mchango wa chama hicho, hata baada ya Rais Kikwete kuweka bayana kuwa haliepukiki.
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Don't expect anything new
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Tatizo la CCM ni kukwepa kufikiria kuunda Tume ya Bunge na kuchunguza ukweli wa ya kuwa kati ya Jk na Dr. Slaa ni nani alishinda Uraisi 2010........Ili kumpa mshindi uhalali wa kuliongoza taifa hili.........................................JK hana legitimacy ya kuliongoza taifa hili hata chembe.................
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,476
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hakuna jipya lolote litakalotokea hapo!
   
 6. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  from Ghost busters
   
 7. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,805
  Likes Received: 6,315
  Trophy Points: 280
  Katiba yetu hairuhusu jambo hilo!
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,808
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Same old story - Usitegemee chochote hapo

  Makamba + Kikwete = Nil Value!

  Nil Value * DOWANS = RA

  RA + EL = Tanzania
   
 9. K

  Kipara kikubwa Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Natabiri Sita anaweza kukutanana na mapya yanayoweza kuathiri future yake kisiasa. Simnakumbuka yule mwenyekiti wa CCM wa Shinyanga naye ana bifu naye. Tusubiri tuone na huenda pia tukajua mwelekeo na siasa za Tanzania kama tuendako tuna muelekeo mwema au tutzidi tumbukia shimoni
   
 10. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145


  Jamani msitabili yatakayotokea!waswahili wanasema saa mbovu wakati mwingine huonyesha majira sahihi!!
   
 11. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hakuna jipa CCM= Chama cha Malindano:frusty:
  :frusty:
   
 12. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Watu wale wale, mawazo yao yaleyale, kamati imejaa mafisadi walewale wanaosumbua kila siku hivyo hakuna jipya la manufaa kwa wananchi na nchi kwa ujumla wake labda mapya kwa mafisadi ili wanufaike zaidi au kuwafunga midomo wapiganaji
   
 13. escober

  escober JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nothing new, new moves to steal from poor Tanzanians
   
 14. t

  togo Member

  #14
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  alafu kuna hii kitu huwaga najiuliza how come kamati kuu ya ccm ikutane ikulu badala ya lumumba
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Ruta.

  Ni vizuri ungekuwa unataja chanzo cha habari yako.Post namba #1 & #2 bila shaka chanzo ni magazeti kutoyataja maana yake habari hizo chanzo chake ni wewe.
   
 16. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kama kuna kitu nakitamani siku zote ni kuona Mzee Makamba anaendelea kuwa Katibu mkuu wa CCM hadi 2015.
  Na tena natamani CCM na serikali yake wazidi kupoteza mawasiliano na Reality hadi 2015.

  Natamani hata kwenye mkutano wao leo makundi yenye masilahi kinzani yaendelee kuwepo na kustawi.
   
 17. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  They have alot to discuss kama wapo serious na nchi hii......ila koz hawana seriousness yoyote then watakaa na kuulizana why wewe ulisema hivi au vile...inshort i expect nothing out of them........................
   
 18. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ni mipango ya kinyonyaji tu kuendelea kusukwa........
  haiwezekani chama watu wanakubaliana na kila kitu,waige mfano kwa cdm,ndani ya vikao vya chama watu wanapiga kura katika kufanya maamuzi........:A S 39:
   
 19. chalinze

  chalinze New Member

  #19
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mikakati zaidi ya wizi.....
   
 20. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Non of my concern... CCM ni chama tu cha siasa kama vingine... hakina lolote la kutufundisha sie tuliojitambua tayari. There was a time kilikuwa na dira lakini kwa safu huu
  1. Makamba
  2.Tambwe Hiza
  3. Chiligati
  4. JK
  5. LA, EL, na wengineo wengi

  Si tu mafisadi, pia hawana fikra pana zenye mtazamo. Ndio maana mpaka leo tunajifunza kwa hotuba za Nyerere si wengine, sikumbuki hotuba ya JK niliyowahi kuipenda.. CCM imechoka sana. Bongo fleva na taarab ndio hujaza watu m ikutanoni sio hotuba zao...
  I AM VERY SORRY FOR THEM!:A S 39:
   
Loading...