Kamati Kuu CCM moto, baridi leo!

Kamati Kuu CCM moto, baridi leo!

Toka chama kilipotelekeza majukumu yake ya kusimamia utendaji wa serikali na kuchukua hatua dhidi ya watendaji wabovu vikao kama hivi vimegeuka kuwa ze komedi. Chama sasa hivi kimebaki ni mhuri na hakina falsafa wala mwelekeo wowote. Chama kilipo ni chama cha kuanguka tu. Suala ni kitaanguka chenyewe au kitaanguka na Tanzania yote.

Watanzania wanaweza kujisaidia na kukisaidia chama wakifanya jambo moja tu; kukinyima chama kura kwenye uchaguzi ili hatimaye kianguke chenyewe peke yake. Tukishindwa ni kwamba chama hiki kitaanguka na nchi yetu pamoja. Kuanguka kwa CCM ni jambo ambalo haliwezi kubishaniwa leo hii.

Kadri tunavyopoteza nafasi za kukiondoa chama madarakani ndivyo tunavyozidisha uwezekano wa chama kuanguka na nchi pamoja. Angalia mijadala iliyotawala anga ndani ya vyombo vya habari sasa hivi, utajua mahala chama kinapoipeleka nchi hii na hatima yake ni nini.

Kikao cha kamati kuu zamani ilikuwa ni mahali pa kuangalia msimamo na mwelekeo wa nchi kwa maono ya falsafa zilizo kuwepo. Sasa hivi vikao pama hivi ni vya kujadili "petty issues" za askofu au shekhe ana msimamo gani. Misimamo ya watu walio nje ni ya muhimu zaidi kwa sababu hakuna falsafa wala mwelekeo unaojulikana.

Chama hiki ni cha kuanguka, kilipofikia ni kama mtoto aliyekwisha zaliwa; hawezi kurudi tumboni mwa mama yake asilani! CCM haiwezi kujirekebisha na hakuna anayeweza kuirekebisha. Tusubiri tu kitaangukaje!
 
alafu kuna hii kitu huwaga najiuliza how come kamati kuu ya ccm ikutane ikulu badala ya lumumba

It is good question. Katika hali ya kawaida shughuli za chama zinatakiwa kufanyika nje ya ofisi na idara za serikali, no exceptions. Lakini swahili hili linaweza kuonekana kuwa........kwa kuwa hapa kwetu ni TZ.
 
Hamna jipya wala haina haja ya kujipa presha...Weak President,Weak Chairman!....Watajidai kuja na tamko la kulaani mauaji ya Arusha baada ya kuona ngoma ngumu! Dowans watajikausha!..
 
Back
Top Bottom