Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,498
Jumapili tarehe 18 Januari, 2026 Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo itakutana jijini Dar es salaam ikiwa ni kikao chake cha kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.
Katika kikao hicho, Kamati Kuu inatarajia kupokea na kujadili taarifa ya Sekretarieti ya Chama Taifa na kutoa maelekezo ya hatua za utekelezaji.
Miongoni mwa taarifa muhimu zitakazopokelewa na kujadiliwa ni pamoja na Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Kamati Kuu itafanya tathmini ya kina ya Uchaguzi huo, tathmini ya hali ya kisiasa nchini na kutoka na maazimio na maagizo mbalimbali yenye kutoa mwelekeo wa Chama.
Mbali na ajenda hiyo, Kamati Kuu pia, itajadili taarifa ya Haki za Binadamu inayotokana na matukio ya Uchaguzi Mkuu huo.
Kikao kitafanyika Makao Makuu ya Chama, Magomeni Dar es Salaam, katika ukumbi wa vikao wa Hakainde Hichilema, kuanzia saa 4:00 asubuhi.