Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,236
Kwanza kabisa ni lazima mamlaka za Tanzania zifahamu kwamba sisi wananchi tuna akili timamu alizotupa Mungu , ule wakati alipotuumba , lakini pia tukaongeza maarifa mengine kwa kusoma shule , hivyo wanavyotupa taarifa ni lazima watambue kwamba sisi wanaotupa taarifa hizi tuna uelewa kama wao ama pengine tunawazidi.
Kama mapato yaliyotokana na kivuko cha MV NYERERE waliyapokea siku zote basi ni wazi kwamba walikuwa wanafahamu juu ya kivuko hicho kupakia idadi kubwa ya abiria kuliko uwezo wake , kama nauli ya abiria mmoja ni elfu 1 ( huu ni mfano tu ) basi kwa abiria 101 kinachotakiwa kupatikana ni Tsh laki 1 na elfu 1 au chini ya hapo kulingana na idadi ya abiria kwa tripu hiyo , hapa tutajumlisha na mapato yatokanayo na mizigo kulingana na tani zilizoruhusiwa kwa mujibu wa utaratibu , bila shaka rekodi zipo .
Hii maana yake ni kwamba kama serikali ilikuwa inapokea hela zaidi ya mara 3 kuliko ambayo ingepata kwa abiria 101 basi bila shaka mamlaka zilifahamu kuhusu hatari iliyojitokeza na kuuwa mamia ya wananchi , mamlaka inajua kwamba hela ilizopokea zilitokana na tripu zilizojaza abiria kuliko kiwango kinachoruhusiwa , NAMBA HAZIJAWAHI KUDANGANYA , Na kwa kweli kwa hesabu hii ni kama uchunguzi wa kamati umekwisha , maana mtungo wote wa waliohusika kupokea pesa ikiwa ni pamoja na waliozitambua wanahusika moja kwa moja .
Kwa vile kamati tayari imeundwa naiomba ije jf imsome Erythrocyte ipate pa kuanzia ambapo kimsingi ndio pa kumalizia pia .
Naomba kuwasilisha .