Kamata kamata ya sakata la MV NYERERE: Mnyororo ni mrefu sana

Jenerali Waitara hajawahi kuharibu kazi popote
Kuna mbunge toka chadema
Kuns DSM zonal crimes officer
kuna mtendaji mkuu wa zamani wa Temesa
Kuna mwanasheria
kuna mtu toka idara ya maafa
kuna mwanamke mtetezi wa haki za wanawake
Naamini mbivu na mbichi zitajulikana tu
Waitara we humjui.Uliza habari za Meremeta
 
Waisome business plan ya Mv.Nyerere....lazma kulikua na cashflow projections na payback period ambayo sensitivity analysis yake lazima ilizingatia best case na worst case scenarios (yaan kama kivuko kitakua kinajaza optimum load na kama kitakua kinapakia below capacity). Then waangalie mapato hua yanasomekaje na waangalie kama hua yanazidi cashflow projection ya best case scenario....duh hapo mnyororo utakua mrefu mkuu.

Coz huez kua na kivuko ambacho kinatakiwa ku payback ndani ya miaka 10 kwa best case afu ikatokea kivuko ku payback kwa miaka 3 na usishtue. Lazima kuna tatzo la governance somwhere. Wengi lazima wakwende na maji!!
 
Mi naomba kamat ianze kutizama mapato siku ya tukio kama itakuwa orodha ya watu 101 hapo ndo watajua nin na wap na nan alikuwa anapga zaid,
ila kama itaonekana tangu tarehe ya tukio mzigo umeingia sehem usika bac ianzia hapo kushuka chin mamlaka zote zihojiwe
 
Bravo bravo!kama serikali ya ccm ingekuwa sikivu.Na kuangalia hata huku nje ya chama tungeshafika level ya south Africa miaka mitano ilopita saiz tungemfukuzia Morroco.Lakin sasa wao ni maprofesa uchwara tu.
 
Kwanza kabisa ni lazima mamlaka za Tanzania zifahamu kwamba sisi wananchi tuna akili timamu alizotupa Mungu , ule wakati alipotuumba , lakini pia tukaongeza maarifa mengine kwa kusoma shule , hivyo wanavyotupa taarifa ni lazima watambue kwamba sisi wanaotupa taarifa hizi tuna uelewa kama wao ama pengine tunawazidi.

Kama mapato yaliyotokana na kivuko cha MV NYERERE waliyapokea siku zote basi ni wazi kwamba walikuwa wanafahamu juu ya kivuko hicho kupakia idadi kubwa ya abiria kuliko uwezo wake , kama nauli ya abiria mmoja ni elfu 1 ( huu ni mfano tu ) basi kwa abiria 101 kinachotakiwa kupatikana ni Tsh laki 1 na elfu 1 au chini ya hapo kulingana na idadi ya abiria kwa tripu hiyo , hapa tutajumlisha na mapato yatokanayo na mizigo kulingana na tani zilizoruhusiwa kwa mujibu wa utaratibu , bila shaka rekodi zipo .

Hii maana yake ni kwamba kama serikali ilikuwa inapokea hela zaidi ya mara 3 kuliko ambayo ingepata kwa abiria 101 basi bila shaka mamlaka zilifahamu kuhusu hatari iliyojitokeza na kuuwa mamia ya wananchi , mamlaka inajua kwamba hela ilizopokea zilitokana na tripu zilizojaza abiria kuliko kiwango kinachoruhusiwa , NAMBA HAZIJAWAHI KUDANGANYA , Na kwa kweli kwa hesabu hii ni kama uchunguzi wa kamati umekwisha , maana mtungo wote wa waliohusika kupokea pesa ikiwa ni pamoja na waliozitambua wanahusika moja kwa moja .

Kwa vile kamati tayari imeundwa naiomba ije jf imsome Erythrocyte ipate pa kuanzia ambapo kimsingi ndio pa kumalizia pia .

Naomba kuwasilisha .

Hapa mtendaji Mkuu wa Sumatra, TEMESA, Mkuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa, IGP upande wa traffic - kujaza abiria zaidi ya kipimo cha serikali wawajibishwe!!!!! Kama hela ilikuwa inaingia kwa mfuko wa serikali ni dhamani(value) ya abiria 101 basi wafanyakazi wote wa MV Nyerere walikuwa wanachukua cha juu!!!wote ni wakutumbua pia - siyo waaminifu(dishonest workers/employees).Period.
 
Bugorola(Ukerewe) to Bwisya(Ukara) nauli ni tsh 800. Yani shilingi 800. Watu 101, total itakuwa ni Tsh 80,800/=. Hii hela haitoshi mafuta tu ya kusafirisha kivuko from one point to another.
 
Hapo kinachofanyika ni kuwatoa watu kafala ili wengine wapone!!! Na hata hao wenyeviti wa bodi hizo wanaotumbuliwa ukiangalia ki undani wao sio wasimamizi wa shughuru za kila siku!!! Unakimbilia kumkamata captain ambaye siku hiyo hakuwa zamu!!! Mala fundi mkuu!!!
Na watakao tolewa kafara mwisho wa siku watakuwa huru mahakamani. Mwisho wa story tutasubiri ajali nyingine
 
Jenerali Waitara hajawahi kuharibu kazi popote
Kuna mbunge toka chadema
Kuns DSM zonal crimes officer
kuna mtendaji mkuu wa zamani wa Temesa
Kuna mwanasheria
kuna mtu toka idara ya maafa
kuna mwanamke mtetezi wa haki za wanawake
Naamini mbivu na mbichi zitajulikana tu
Kwani wale maprof wa makinikia wakati wanatoa ile taarifa yao ungedhani kuwa mpaka leo hatuna Noah zetu. Kuna namna wanafanya sijui ni makusudi au kweli hawajui ila si sawa. Hawaaminiki
 
Kwani wale maprof wa makinikia wakati wanatoa ile taarifa yao ungedhani kuwa mpaka leo hatuna Noah zetu. Kuna namna wanafanya sijui ni makusudi au kweli hawajui ila si sawa. Hawaaminiki
Baada ya kusoma andiko lako kipegere cha makinikia machozi yamenibubujika !
 
Back
Top Bottom