Kamata kamata na kile kinachoendelea Pemba, IGP Sirro sikiliza ushauri huu

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,099
2,000
Mada inahusika.

Nadhani wote tunaelewa kinachoendelea katika kijiji cha Kangagani huko Pemba, baada ya usiku wa kuamkia juzi tarehe 22 Septemba, 2020 , kulitokea tukio la kushambuliwa kwa mapanga waumini msikitini na baadae kujulikana walioshambuliwa kuwa makada wa CCM.

Sote bila kujali itikadi tunalaani matukio ya aina hii. Nakupeni taarifa kidogo kuhusu Kijiji hiki na mivutano ya kisiasa nadhani ndugu IGP inaweza kukusaidia kuujua ukweli. Tumefatilia vya kutosha.

Kijiji hiki cha Kangagani kina wafuasi wengi wa Upinzani na ni kijiji ambacho kwa Pemba kuna wanachama wa CCM wengi ukilinganisha na vijiji vyengine ingawa wingi huo hauzidi ule wa Upinzani.

Kijiji hiki kina historia ya uhasama wa vyama kwa wakati huo ilikuwa ni kati ya CUF na CCM na sasa ni ACT na CCM.
Kuanzia 1995 hadi sasa mvutano na chuki unaendelea na kutambiana.

Yalishatokea matukio mengi ya watu kuchomeana nyumba, kupigana, kuharibiana mazao na kilimo na kila aina ya vitimbi.

Kijiji hiki kinasifika kwa fitina ambapo ilishawahi kuripotiwa baadhi ya vijana wa Upinzani kunyimwa ajira kwa kuwekewa fitina na wenye mamlaka na ushawishi ndani ya CCM kutoka kijiji hiki. Ndugu IGP fuatilia vizuri ujuwe mzizi wa fitina ili haki itendeke.
Zipo taarifa kwamba kuna wana CCM walishawafitinisha hadi watoto wao wa kuwazaa na kufukuzwa kazini miaka ya 1995- 2000.

Kwa ufupi kuna uhasama wa kudumu na si wa kutokea tu.

Tukio la tarehe 22 Septemba, 2020
Kuna taarifa ndugu IGP hutazipata popote maana wasemaji na wenye mamlaka wanaogelea kwenye mzozo huu.

Jioni ya tarehe 22 zilipatikana taarifa za kutiliwa fitina baadhi ya wafuasi wa ACT ili wakamatwe na Polisi( Uzuri Pemba watu wanajuana na taarifa zinafika kwa wahusika kabla ya tukio) kwa hesabu za kisiasa ikisemekana eti wanahamasisha vurugu na mipango ilikuwa wakamatwe ili kupata mtaji wa kuelekea kwenye uchaguzi wa wabunge na uwakilishi.

Ndugu IGP fuatilia vizuri nini sababu ya kutumwa Polisi tarehe hiyo ili kuwakamata vijana watatu mashuhuri na mwiba kwa CCM kijijini hapo. Fuatilia kwa nini Polisi / vikosi vya SMZ walimdhalilisha mke mmoja wa watu waliotafutwa na kumvua nguo.

Kutokana na uhasama huo waliokuwa wakitafutwa ni wazoefu wa kuwekwa ndani Polisi na huwa wanalalamika kwa kuonewa kwa chuki za wana CCM. Kwa ufupi wanajuana.

Ndugu IGP Fuatilia taarifa vizuri. Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba wanajua matatizo ya kijiji hicho na kwa miaka ya karibuni wamejitahidi kujiepusha na mitego ya maelekezo ya kisiasa.

Ukweli ni kwamba CCM wanalivitumia vyombo vya ulinzi kuwadhibiti wapinzani wao kutokana na kuzidiwa na wapinzani na CCM hupanga njama na viongozi wa serikali wenye ushawishi ambao baadhi wanatoka kijiji hicho (ulizia yule Mkuu wa Wilaya moja hapo Pemba anayetoka kijiji hicho anavyotumia madaraka yake )

Ndugu IGP tukio la Juzi ni mripuko wa Hasira kwa mtuhumiwa mmoja ambaye inasemekana Mke wake alidhalilishwa na huyu ni muhanga wa kila mara wa kukamatwa na kuteswa kwa fitina tu. Juzi yalimshinda. Mpaka hapo ujuwe kuwa kijiji hiki kina historia na kila kipindi cha siasa mambo haya hutokea.

KILICHOFUATA.
Usiku wa kuamkia jana tarehe 23 Septemba, 2020 kwa mfumo ule ule na kwa njia zile zile za maelekezo kwa kisingizio cha kuwatafuta watuhumiwa (ingawa muhusika anajulikana) Vikosi vya SMZ na POLISI viliamua kutumia njia ya kuvamia waumini msikitini ( msikiti wanaoswali wapinzani) kuwakamata watu wote waliokuwemo, kuwapiga na kuwasomba.

Walivamia nyumba za watuhumiwa na viongozi wa ACT , kuvunja milango na zipo taarifa za kuibiwa mali na uharibifu mbali mbali. Ndugu IGP sijui kama taarifa za tukio hili utaambiwa maana akina mama walidhalilishwa na kugaragazwa chini kwa hasira baada ya wanaume waliokusudiwa kukosekana kwenye majumba yao.

Unashangaa uhasama wa kijiji unajulikana baada ya kutumia njia za uweledi Polisi na Vikosi vya SMZ vilitumika beyond kwa masindikizo na kuwadhuru watu wasiohusika. Fuatilia vizuri Mkuu.

Hatma yake kuna kukuzwa kwa Tukio eti walilengwa wana CCM na upinzani kwa ujumla. Ni uhasama maalumu kwa watu maalumu. Fuatilia vizuri ingawa siasa inahusika.

Kwa nini waliachwa wana CCM wengi na kushambuliwa hao watatu tena na mtu maalumu Fuatilia Kamanda.

Kwa nini Polisi na Vikosi walitumia njia hio wakati kuna njia nyingi tena nzuri zisizo na madhara kwa jamii? tukisema ni sindikizo tutakosea?

USHAURI
Jeshi la Polisi lijiweke katikati na kamwe lisifuate midundo ya kisiasa. Kijiji hiki kina historia bila kutumiwa weledi Polisi watatumika na wataacha mgogoro ukiendelea miaka yote bila sababu. Kijiji hiki wenyewe wanajuana

Polisi ipate uzoefu wa miaka ya nyuma kule Mjini Magharibi Unguja, UVCCM ilitumia njia hizi za kutoa maelekezo kwa Polisi na wakati mwengine Polisi waliingizwa kwenye matatizo bila sababu za msingi.

Kipindi hiki ni Muhimu kutumika WELEDI na Polisi kutenda haki bila uonevu kwa wafuasi wa vyama.

Polisi isitumike kukuza mambo ambayo yana harufu ya siasa kwa ajili ya nchi yetu Tanzania.

Polisi ielewe kipindi hiki kuna watu wana ushawishi wa kimamlaka, watumie weledi na sheria ili kutenda haki. Kwa Mazingira ya Pemba, chochote kitakachotamkwa na upande wa CCM/ watawala dhidi ya Upinzani bila kutumia jicho la tatu unaweza kutumbukia bila kujua. Polisi ijitahidi kuwa Makini.

Ni hayo kwa sasa.

Kwa niaba ya Crew iliyoko Zanzibar.

Kishada.
 

Ngisibara

JF-Expert Member
Jan 2, 2009
2,867
2,000
Mada inahusika.

Nadhani wote tunaelewa kinachoendelea katika kijiji cha Kangagani huko Pemba, baada ya usiku wa kuamkia juzi tarehe 22 Septemba, 2020 , kulitokea tukio la kushambuliwa kwa mapanga waumini msikitini na baadae kujulikana walioshambuliwa kuwa makada wa CCM...


Unategemea Polisi ktk hili?
 

issa yurry

JF-Expert Member
Apr 20, 2014
611
1,000
Yule jamaa hakupigwa msikitini bali ni uongo yeye ilikua anatoka usiku anapigiwa simu na askari kama mida ya saa7 usiku wanakuja askari kwake na kuwatembeza nyumba wanazokaa viongozi wa ACT halafu polisi wanawavamia usiku na kuwapiga sasa kilichofanyika kama siku 3 jamaa wakakaa kikao na kuchunguza anae kuja kuonyesha nyumba za wapinzani ninani ndio wakagundua niwale jamaa wa ccm sasa jamaa wa kamfuata kwake na kumpiga tena kidogo tu kama kumpa onyo sasa wao wataka kusema ni msikiti ili wauchafuwe uislam wala siyo kweli.
 

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
1,777
2,000
Mada inahusika.

Nadhani wote tunaelewa kinachoendelea katika kijiji cha Kangagani huko Pemba, baada ya usiku wa kuamkia juzi tarehe 22 Septemba, 2020 , kulitokea tukio la kushambuliwa kwa mapanga waumini msikitini na baadae kujulikana walioshambuliwa kuwa makada wa CCM...
Aisee
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
2,275
2,000
Nimesikiliza maelezo ya Sirro anaongea kishabiki sana, Sirro amejisahau sana, anatakiwa akumbuke umuhimu wa nafasi yake na ajue jinsi ya kuitumia hiyo nafasi aliyopewa asije kusababisha matatizo zaidi badala ya kuyamaliza, jeshi la polisi lifanye uchunguzi kamili kabla ya kutoa taarifa yoyote ili kuepuka kutoa taarifa zitakazoacha maswali kwa jamii.
 

komamgo

JF-Expert Member
Sep 14, 2012
2,028
2,000
Yule jamaa hakupigwa msikitini bali ni uongo yeye ilikua anatoka usiku anapigiwa simu na askari kama mida ya saa7 usiku wanakuja askari kwake na kuwatembeza nyumba wanazokaa viongozi wa ACT halafu polisi wanawavamia usiku na kuwapiga sasa kilichofanyika kama siku 3 jamaa wakakaa kikao na kuchunguza anae kuja kuonyesha nyumba za wapinzani ninani ndio wakagundua niwale jamaa wa ccm sasa jamaa wa kamfuata kwake na kumpiga tena kidogo tu kama kumpa onyo sasa wao wataka kusema ni msikiti ili wauchafuwe uislam wala siyo kweli

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
"Kupiga kidogo tu" bado ni kosa kisheria
 

komamgo

JF-Expert Member
Sep 14, 2012
2,028
2,000
Dawa ya hicho kijiji ni kupandikiza miradi mikubwa ya serikali na kuwa changanyia ratiba za kupigana , watajikuta wanatumbukia kwenye uzalishaji na kupokea wageni.
 

Malcom XX

JF-Expert Member
Sep 12, 2020
382
1,000
Mada inahusika.

Nadhani wote tunaelewa kinachoendelea katika kijiji cha Kangagani huko Pemba, baada ya usiku wa kuamkia juzi tarehe 22 Septemba, 2020 , kulitokea tukio la kushambuliwa kwa mapanga waumini msikitini na baadae kujulikana walioshambuliwa kuwa makada wa CCM...
aijipi keshaingia kwenye mtego wa kisiasa, mwache atolewe ngebe, after election siyo AIJIPI TENA
 

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,099
2,000
Kamanda sikia. Halo kuna fitna na kutiana adabu. Upande mmoja unafaidi dola kutimiza matakwa ya kisiasa, upande wa pili unajitetea hats kwa njia zisizo ilimradi hawapati pa kusemea na kusikilizwa.

Fuatilia na hapo kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya. Huyo attached army officer kama sio mwana CCM mkubwa anayepokea maelekezo ya kichama.

Huu mgogoro ni mkubwa asee.

Polisi jinasuweni mapema
 

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,099
2,000
Kamanda sikia. Halo kuna fitna na kutiana adabu. Upande mmoja unafaidi dola kutimiza matakwa ya kisiasa, upande wa pili unajitetea hats kwa njia zisizo ilimradi hawapati pa kusemea na kusikilizwa.

Fuatilia na hapo kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya. Huyo attached army officer kama sio mwana CCM mkubwa anayepokea maelekezo ya kichama.

Huu mgogoro ni mkubwa asee.

Polisi jinasuweni mapema
Tena kumbe taarifa zinabainisha Huyo mjeda anatoka kijiji hicho hicho.
 

kichakani

Member
Dec 20, 2013
15
45
Ushaur wangu kwa viongo wote was kisiasa na kidini acheni kugombna kwa dunia Kama mnajua haina Faida yyte kwenu fitna ni mbaya wangap walikuwepo na madaraka yao mpaka ilifikia hatua ya kujiita mungu leo wamelala kwenye tumbo la ardhi
 

Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,498
2,000
Huko Pemba ni kwa kudhibitiwa kisawasawa, vyombo vya ulinzi vikiwadekeza hao wahalifu Tanzania na Jumuiya Afrika Mashariki itakua matatani
 

ngozimbili

JF-Expert Member
Jul 28, 2011
1,365
2,000
Huko Pemba ni kwa kudhibitiwa kisawasawa, vyombo vya ulinzi vikiwadekeza hao wahalifu Tanzania na Jumuiya Afrika Mashariki itakua matatani
Wameshauawa ila kwakuwa tatizo halijatatuliwa mambo yatakuwa yaleyale
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom