Kamata kamata Tanzania kwa wanaopinga mkataba wa bandari

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa Bujumbura, tarehe 4, Februari 2023.Picha na Tchandrou Nitanga / AFP.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa Bujumbura, tarehe 4, Februari 2023. Picha na Tchandrou Nitanga / AFP.

Polisi nchini Tanzania wamewakamata wakili mmoja na mwanasiasa wa upinzani, wakiwahutumu kwa kuchochea na kupanga maandamano kote nchini humo kwa lengo la kuiangusha serikali. Wakili Boniface Anyasile Mwabukusi na Mpaluka Nyagali walikamatwa jumamosi.

Wakili Mwabukusi, alikuwa miongoni mwa mawakili waliowasilisha kesi mahakamani kupinga mkataba huo, na kesi ilitupiliwa mbali alhamisi wiki iliyopita. Amesema atakata rufaa. Wakili wa wawili hao, Philip Mwakilima, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba alikuwa anafanya kila juhudi kuzungumza na wateja wake wanaozuliwa na polisi, na kwamba madai dhidi yao ni ya uongo.

Mkuu wa polisi wa Tanzania Camillus Wambura amesema katika taarifa kwamba anachukua hatua dhidi ya kundi lililokuwa linapanga kuandaa maandamano kote nchini humo, kwa lengo la kuuangusha utawala wa rais Samia Suluhu Hassan kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Amesema kwamba wawili hao wamekuwa wakiandika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii tangu tarehe 10 mwezi Agosti, wakiwa na lengo la kuchochea na kuwashawishi raia wa Tanzania kufanya maandamano kote nchini, na kwamba mmoja wao alisema kwamba wataipindua serikali ya rais kabla ya uchaguzi mkuu, jambo ambalo ni uhaini.

Wambura amesema kwamba wanaoitisha maandamano wanapinga maamuzi ya mahakama kutupilia mbali kesi inayopinga mkataba kati ya serikali na kampuni ya Dubai ya DP World kuhusiana na usimamizi wa bandari ya Dar-es-salaam. Bunge la Tanzania liliidhinisha mkataba huo mnamo mwezi June.

Watetezi wa haki za binadamu wamesema kwamba watu 22 wanazuiliwa na polisi au kutishiwa tangu mwezi June kwa kulikosoa bunge baada ya kuidhinisha mkataba kati ya serikali na DP World.

Msemaji wa serikali Gerson msigwa amepuuza madai kwamba serikali inawanyamazisha wanasiasa wa upinzani kwa nguvu.
 
Mnajitaidi kupotosha, lakini mumeangukia patupuu. Wananchi wamewapuuuza saana. Mnajitaidi ili mpate kiki ya kisiasa, cha ajabu wananchi wamewagundua.
 
Mnajitaidi kupotosha, lakini mumeangukia patupuu. Wananchi wamewapuuuza saana. Mnajitaidi ili mpate kiki ya kisiasa, cha ajabu wananchi wamewagundua.
Hili suala limetuma ujumbe hasi kule duniani,sasa hata Dunia iliyokuwa haijui chochote kuhusu dubwasha letu na dp imeanza kutizama na kujiuliza kulikoni pale kutangaziana Nia ya kutaka kutiama kitanzi sio ishu ndogo huko dniani brother. Muda si mrefu utaona matokeo yake, nawasihi sisi Kama ndugu turudi tukae chini tuyamalize kifamilia tunakoenda siko.
 
Chadema mnahangaika kutafuta kiki, wala hamtaambulia chochote.
 
Dr Slaa(jasusi la ccm) linajidai kutukana utawala na kusema mapinduzi yafanyike ili Chadema wamrejeshe😂
 
Tatizo la wanaccm kujiona wao ndiyo wenye hati miliki ya taifa hili. Mijitu mipumbavu hua inawaza ujinga, na ujinga hautalifikisha taifa mahali popote. Ccm imezoea kuwatia ujinga watanzania inapotokea watu wanaowaambia watanzania ukweli basi kwa gharama zozote watawateka, mfano Dr Ulimboka.

Lakini wajue wananchi wanamadukuduku yao wanashindwa pa kusemea, ila kwa kujitoa ufahamu mnaona wananchi wanafurahia utawala wenu wa kiimra, endeleeni kujidanganya ila wananchi mtaani mioyo yao unaandamana kila siku isipokuwa wanashindwa kuingia mtaani maana mlishasema kama wakiingia mtaani mtawavunja miguu.

Uhalisia mioyo ya watanzania ipo kwenye maandamano ingawa kimwili wanalazimishwa na kutishwa wakiandamana watawavunja miguu. Hawa wajinga wachache wanaoona wanahatimiliki ya Tanzania ndiyo wahaini namba moja kuliko hao mnaowakamata.
 
Hili suala limetuma ujumbe hasi kule duniani,sasa hata Dunia iliyokuwa haijui chochote kuhusu dubwasha letu na dp imeanza kutizama na kujiuliza kulikoni pale kutangaziana Nia ya kutaka kutiama kitanzi sio ishu ndogo huko dniani brother. Muda si mrefu utaona matokeo yake, nawasihi sisi Kama ndugu turudi tukae chini tuyamalize kifamilia tunakoenda siko.
Hata mkituma ujumbe mbinguni, tayari hata nako huko wanawajua kuwa nyinyi mnapotosha uharisia.
 
Back
Top Bottom