SoC03 Kamari na athari zake kwa kizazi cha siku zijazo Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

MrProsecutor

JF-Expert Member
Jun 12, 2017
281
274
UTANGULIZI
Kamari imekua kimbilio la vijana wengi ambao kwa namna moja ama nyingine wanategemea ajira kama chanzo cha kujikwamua na umasikini. Kiukweli hali ya ajira ni ngumu duniani na pia tukubaliane kwamba kama vijana tuna mitazamo tofauti nikimaanisha sio kila kijana anaweza ujasiriamali, na wanaoweza pia wanakumbana na changamoto za mitaji n.k. hivyo kupelekea wengi kujiingiza katika wimbi hili. Kupitia uzi huu tutaweza kuona sababu za kushiriki na suluhisho chanya kwa ajili ya mustakabali bora wa vijana wa Tanzania.

SABABU ZA KUSHIRIKI KAMARI
1. Ndoto ya Utajiri wa haraka: Ukosefu wa ajira unawafanya vijana kushawishika zaidi na ahadi za utajiri wa papo hapo kupitia kamari kila sehemu zinatangazwa hivyo kuvutia zaidi vijana, wakiamini kuwa kamari ndio ufunguo wa maisha baada ya kushindwa kupata ajira kwa muda mrefu. Wengi wanatamani kutoka kwenye minyororo ya umaskini ili kujisaidia na kusaidia familia zao na kuona njia sahihi ni kamari ambapo wanaamini uwezekano wa kushinda ni taa ndogo ya matumaini katikati ya giza nene la umaskini na ukosefu wa ajira.

2. Shinikizo la marafiki: vijana ni watu ambao ni wepesi sana kufuata mkumbo ambapo mtu anaweza kuanza kucheza kamari kwasababu tu rafiki zake wanacheza. Hili ni tatizo lapili ambapo likiongozwa na tatizo la kwanza la hali ngumu ya kiuchumi inayowafanya vijana kutaka mafanikio na njia rahisi za kujikwamua kiuchumi, hivyo akimuona mwenzake amepiga mkeka wa elfu 10 akapata faida laki 2 anaona ni njia sahihi nae kuingia kwasababu ni hela ya haraka ndani ya muda mfupi, ukiingia hutoki.

SULUHISHO
1. Ujenzi wa uchumi endelevu na kuchochea ujasiriamali: sera na uchumi imara utakaojengwa na serikali utaweza kuwafanya vijana kupata fursa nyingi za kiuchumi katika utalii, kilimo, teknolojia, biashara, kuvutia uwekezaji ambao utatengeneza ajira na njia nyingine za kiuchumi ambazo zitasaidia vijana kujikwamua, mfano kuna vijana wameamua kujituma kutafuta kazi nje ya nchi kupitia mtandao lakini bahati mbaya hawawezi kupokea malipo kwa mfumo wa 'paypal' ambao unatumika sana duniani kwa malipo mbalimbali hii ni kutokana na mfumo huo kutoruhusiwa kufanya kazi nchini Tanzania.

2. Kuupitia upya mfumo wa elimu: katika kupitia upya mfumo wa elimu kutapelekea kuandaa mitaala ambayo itawafanya wahitimu kujengeka zaidi kiubunifu na kuwafanya sio tena wenye kutegemea tu ajira bali wanaweza kutumia maarifa yao na kujipatia kipato kwa njia nyingine ambazo ni halali.

3. Kazi mbalimbali za muda mfupi: nitaongelea kazi mbalimbali za muda mfupi ambazo zinapatikana mitandaoni, kwanza kabisa nitataja shughuli hizo lakini lugha ya kiswahili sio rafiki sana ila nitajitahidi kadri ya uwezo ambapo baada ya hapa kijana atakaesoma anaweza kuanza kutafuta angalau dolari 5 kwa siku kwa kufanya kazi hizi kitu ambacho ni bora kwakwe kuliko kukaa bure na kucheza kamari. Kazi hizo ni pamoja na;

a) Uendeshaji wa Blogu ambapo kijana anaweza kuanzisha blogu yake akichagua jambo lolote ambalo ana uelewa nalo vizuri na kufanya machapisho ya makala mbalimbali kitu ambacho kitapelekea kupata pesa kupitia matangazo yatakayopitishwa kwenye blogu yake kutokana na kuwa na watembeleaji wengi.

b) Uingizaji wa taarifa, kuna majukwaa kama fiverr, upwork, n.k. ambayo yanatoa kazi ya uingizaji wa taarifa mbalimbali mfano kujaza taarifa za barua pepe na namba za simu na majina nk.

c) Tafsiri na ukalimani hapa unaweza kufanya tafsiri ya lugha mbalimbali endapo utakuwa na ujuzi wa lugha tofauti tofauti kazi hizi zipo mitandaoni ni jinsi ya kupata taarifa za kutosha na kuanza sio rahisi lakini inawezekana, mfano wa jukwaa ni: transribeme nk.


d) Stoo mtandao, hii nitaielezea kwa urefu kidogo ili kutoa mwanga huenda ikamfaa mtu. Hapa ni sawa na kumiliki duka bila kuwa na bidhaa yoyote ile, kuna majukwaa kama alibaba, aliexpress, ebay, amazon n.k. ambayo yanauza bidhaa mbalimbali. Kitu ambacho unaweza kufanya ni kutengeneza kitu kama hicho, mfano unaweza kutumia wordpress kutengeneza tovuti yako na ukachagua vifaa vya kielektroniki na ukaviweka kwenye tovuti yako.

Jinsi ya kufanya ni kufungua worspress na kutengeneza tovuti kisha unaenda sehemu kama alibaba na kuangalia bidhaa inayoendana na uliyochagua (tumechagua elektroniki) baada ya hapo utatafuta msambazaji wa kuaminika mwenye nyota kuanzia 3 na kuendelea na kuchukua picha za bidhaa zote ambazo umepanga kuziweka kwenye tovuti yako kisha unaweka na maelezo, hapa naomba uwe makini, suala la bei ndipo utakapopatia pesa. Sasa hapa unaweza kukuta mfano kioo cha simu kinauzwa dolari za kimarekani 27 (pamoja na usafiri wa sehemu husika), nikushauri kitu acha tamaa ongeza dolari 5 tu ambapo bei kwako itakuwa dolari 32, hupigi hela?

Sasa tafuta bidhaa zinazouzika sanaaa na weka bidhaa zako hata 100 au zaidi, kila bidhaa utapanga bei kulingana na bei ya kitu. Ukiweza kuuza hata bidhaa 50 kwa mwezi unaweza kupata zaidi ya dolari 200 za kimarekani bila kumiliki bidhaa yoyote ile. Kumbuka sio rahisi ila inawezekana ukituliza kichwa na ukajipa muda wa kutosha kufanya utafiti. Sasa swali, je malipo yanafanyikaje?

Mteja akishatembea tovuti yako akaona bidhaa (kioo cha simu $32) atafanya malipo kwako kupitia mfumo wa malipo ulioweka na kisha wewe utapokea malipo na taarifa zake zote ikiwa ni pamoja na taarifa za makazi, baada ya hapo utatuma kiasi cha $27 kwa msambazaji wa bidhaa ambae umempata alibaba kwa kujaza taarifa zote za mteja wako ili mzigo uweze kutumwa kwake hapo utakuwa umepata faida yako ya $5 na mteja atapata mzigo wake. Nimeandika kwa ufupi ila kuna mengi ya kujua kuhusu fursa hii ndipo mtu aiendee.

MWISHO
Kama jamii ya watanzania na waafrika tujitahidi katika kufanikisha mabadiliko kwa kuanza kusaidiana wenyewe kwa wenyewe kabla ya serikali ili tusiendelee kupoteza muda mwingi kusubiri mabadiliko na mchakato wa kiserikali. Tunaweza kusaidiana kwa kupeana maarifa na taarifa sahihi ambazo vijana wengine wanatumia kupata pesa za kujikimu bila kuwa na ajira ya kudumu kama ambavyo inafanyika kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Jamii Forum, YouTube, Twitter n.k. ahsante.
 
mazingira ya kupata pesa ni magumu.
changamoto ya kupata mtaji ni ngumu.
ajira ni kipato chake avilingani na maisha.
maitaji na maisha yapo tofauti ndio maana akiba hakuna.
serikali sio msaada kuanzia maisha,fursa na n.k

we unatarajia watu pesa watatoa wapi
 
mazingira ya kupata pesa ni magumu.
changamoto ya kupata mtaji ni ngumu.
ajira ni kipato chake avilingani na maisha.
maitaji na maisha yapo tofauti ndio maana akiba hakuna.
serikali sio msaada kuanzia maisha,fursa na n.k

we unatarajia watu pesa watatoa wapi
Ndiomana tunatakiwa kutafuta kazi ambazo ni halali ili kulinda heshima zetu na watoto wetu. Ni vizuri sana kumuambia mtoto wako kwamba "Mimi Baba/Mama yako nimefanikiwa kuweza kumudu maisha kwa kufanya Affiliate Marketing au Remote Jobs kuliko kusema nimeweza kumudu maisha kwa kubeti"
 
Kubeti ni sawa na kuweka hela kwenye kibubu ambacho hujui lini utapata gawio lako
 
Back
Top Bottom