Nov 03, 2023 03:29 UTC
Kamanda huyo wa Hizbullah ameashiria mpaka wa Lebanon wenye urefu wa kilomita 70 uliopakana na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na akasema: Sasa hivi hapa nyuma ya mpaka, sisi tuko tayari kwa vita vya pande zote. Moja ya malengo yetu bayana na ya wazi kabisa lilikuwa ni kuuelekeza utawala wa Kizayuni upande wa kaskazini ili watume kuleta upande wetu sehemu ya vikosi vyake na nguvu yake kutoka Gaza, na lengo hili muhimu limefikiwa".
Kamanda huyo wa Hizbullah ameendelea kueleza kwamba: "sasa hivi utawala wa Kizayuni umeweka brigedi tatu za majeshi mbele yetu na kuunda tabaka tatu za ulinzi, lakini kama tutapokea amri ya kuingia katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, tutayasambaratisha matabaka yote matatu".
Ameongeza kuwa: "sasa hivi tuko kwenye mapigano na Wazayuni na tumeshatokomeza baadhi ya vifaa na teknolojia na bila shaka hata nguvu zao."
Kamanda huyo wa Hizbullah amebainisha kwa kusema: "Tumejiweka tayari kwa nguvu zetu zote; tumefanya mazoezi ya kuingia katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na kuliteka kikamilifu eneo la Al-Jalil; tunao mpango wa operesheni hiyo na tunachongojea ni amri tu".
Amefafanua zaidi kwa kusema: "tumeshazitambua sehemu zote zilizpowekwa Ngao za Chuma na tutazishambulia zote siku ya mapambano. Walikuwa wakidhani hatungeweza kuvipiga vifaru vya Merkava, lakini sasa tumefikia kuwa na teknolojia na ubunifu wa kuviripua vifaru hivyo katika awamu mbili kwa makombora ya Cornet. Kama vita vitaanza kwa maana ya sisi kushambulia kwa ardhini, vifaru vya Merkava itabidi vifichwe".
Kamanda huyo wa Hizbullah ameongezea kwa kusema: "tukipokea amri, tutazipiga manowari zote ambazo hivi karibuni zimetoa msaada kwa utawala wa Kizayuni au zimejitokeza kuulinda. Hatusemi tutazipiga vipi na kwa silaha gani lakini kila mtu ataona pale itakapohitajika".../