Kamanda wa Polisi Kinondoni: Mwandishi wa the Guardian aliyeokotwa Bunju alikuwa amelewa wala hakutekwa

craq

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
859
1,864
Kamanda wa Polisi wilaya ya Kinondoni afande Jumanne afunguka kuhusiana na tukio la mwandishi wa gazeti la the Guardian kuokotwa maeneo ya Bunju akiwa hajitambui

"Mwandishi wa habari wa gazeti la the Guardian bwana Finnigan alfajiri ya leo amekutwa akiwa amelala maeneo ya Bunju A, Bunju A ni mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kwahiyo taarifa zile tulivyozipata tulituma askari na askari walikwenda wakakuta mtu huyo wakamkagua, ukaguzi wa awali ukienda sehemu ya tukio ikaonekana mtu yule hajitambui taarifa za awali za maafisa waliofika pale walimuona katika hali na mazingira ya ulevi kwa maana ya harufu ya pombe -Jumanne murilo mkuu wa Polisi wa Kinondoni

Kwahiyo moja ya majukumu tunayoyafanya sisi tukikutana na hali ya namna hiyo bila kujali yeye ni nani kwasababu tumeshakutana na watu wa namna hiyo mara kadhaa hasa siku za mwisho wa wiki kwahiyo tulimchukua na kumpeleka kwenye hospitali ya Mwananyamala kwaajili ya uchunguzi zaidi.

Uchunguzi wa awali wa Polisi waliofika eneo la tukio wamethibitisha kwangu kuwa mtu yule hakuwa na jeraha lolote lile hata michirizi ya damu hakuna bali amekuwa amelewa kwa kiwango kikubwa

Mimi kama afisa wa Polisi kazi yangu ni kuchunguza ni kwanini mtu yule amelewa kwa kiasi kikubwa kitu gani kilimfanya alewe vile, sisi kama Polisi hatupendi kufanya kazi kwa hisia.-Jumanne Muliro

craq Nitawaomba sasa wale ' Mashambenga Original ' wa humu Jamvini ambao yakitokea tu ' matukio ' kama haya huwa wanakuwa wepesi mno kufanya ' Speculations ' zao kuwa ' Mamlaka ' ndiyo iliyoko nyuma ya mambo yote haya wakati kumbe ni ukweli usiopingika kwamba 80% ya ' matukio ' ya Kutisha kama siyo ya Kusikitisha hutokana na mambo ya Mtu tu Binafsi na ' Washirika ' wake katika harakati zake za Kimaisha na hapa pia tunaweza sasa kupata jambo kwamba huenda hawa Watu tulio wa ' brand ' wasiojulikana wanafanya ' matukio ' kwa ' agenda ' zao na hao Wahusika huku wakiwa wanasafiria ' nyota ' iliyochafuliwa na isiyopendwa ya ' Mamlaka ' ili tu kuweza kuficha ' uhalifu ' wao.

Niliwahi siku moja kusema humu humu kwamba kuna Siku wale ' Mashambenga Original ' watakuja ' Kuumbuliwa ' hasa pale ukweli kuhusu haya ' matukio ' utakapojidhihiri / wekwa wazi. Ni suala la muda tu!
 
TAARIFA YA MWANDISHI WA GUARDIAN KULEWA BILA KUJITAMBUA

Mnamo tarehe 08/04/2018 majira ya Saa 1:30 asubuhi eneo la Bunju A Mianzini mwandishi wa habari aitwaye *Finnigan Frazer Simbeye*,47 yrs Mkristo mwandishi wa habari wa gazeti la Guardian Mnyiha,mkazi wa Bahari beach mtaa wa kondo alikutwa amelewa bila kujitambua na kukutwa amelala mtaroni jirani Bagamoyo road.

Taarifa kamili ni kwamba mnamo tarehe 07/04/2018 Majira ya saa 4:00 asubuhi alitoka nyumbani kwake Bahari beach akiwa na gari lake T383 BCU Toyota Mark ll kwenda Tegeta Kibo ambako aliiacha gari pale na kwenda eneo la Mwenge na baadae alirudi Tegeta kibo na kuchukua gari lake hadi Ununio katika bar ya *Bajet* na baadae alirudi Tegeta darajani katika bar ya *B &DG* ambako alikutana na hawala yake aitwaye *Tonto* mkazi wa Salasala na hapo alikunywa bia 8. Ilipofika saa 1:00 hrs usiku alikwenda katika Bar ya *QR* eneo la Azania Tegeta na kukutana na hawala yake mwingine mhudumu wa Bar hiyo anayeitwa *Grace* na kuendelea kunywa pombe!!!.
Ilipofika saa 3:00 usiku alikwenda katika bar ya *Benten* na kuendelea kunywa na pale alikunywa bia chupa 6 na baadae aligundua kuwa amelewa sana,na hapo hawala yake *Grace* alimshauri watafute Guest walale lakini wakati wakienda gari lake liliingia katika dimbwi la maji na kuzimika na alipoomba msaada wa kulitoa ikashindikana hivyo akaliacha hapo hapo na wakati huo huo hawala yake *Grace* alichukua simu yake ya Smart Phone aina ya *LG* na kuondoka huku akimuacha pale.

Majira ya saa 10:00 usiku alichukua bodaboda kwenda nyumbani kwake Bahari beach ambako aligonga lakini hakufunguliwa na baada ya kutofunguliwa aliamua kwenda tena katika Bar ya Kibo ambao alifika saa 11:00 alfajiri na kukuta watu wanatoka na Bar ikiwa imefungwa,hivyo kuchukua bodaboda kurudi nyumbani tena lakini pia hakufunguliwa na kwa kuwa alikuwa amelewa sana aliamua kuondoka na hakukumbuka tena kinachoendelea hadi asubuhi anajikuta yupo Mwananyamala Hospitali.
Katika mahijiano tumegundua kuwa mwandishi huyo amekunywa pombe sana na kulewa kushindwa kujitambua, amekutwa na ufunguo wa gari lake mfukoni mwake akiwa hospitali na hana jeraha,uvimbe wala mikwaruzo yoyote mwilini, amewekewa dripu za maji na anaendelea vizuri japo bado amelazwa Hospitali Mwananyamala .

Tayari polisi amefunguliwa jalada Kosa la *KULEWA BILA KUJITAMBUA WMB /IR/1565/2018* Taarifa za mitandao kuwa ametekwa sio kweli.
 
kilambalambila Kwanini asiwe nae anaenda Kunywa katika Baa ya Kistaarabu( japo ina rekodi ya Wanywaji wake wengi Kufa kwa ajali za Gari Usiku ambazo huwa zinatokea kimaajabu ajabu tupu ) ya ' Kwa Mbaga ' pale Mbezi Beach njia panda ya kwenda Times FM ambayo hata Bosi wake Mkuu Richard Mghamba huwa anakunywa sana pale kila Siku kuanzia Saa 12 jioni hadi Saa 5 au Saa 7 za Usiku huku akibadilisha tu Gari zake mbili za ' thamani / fahari ' kabisa za Audio na Mazda Nyeusi ili hata basi kama atazidiwa ' Bosi ' wake huyo anaweza akamsitiri kuliko sasa kuja ' Kuumbuka ' kama hivi?
 
Umehama kutoka ' Kuwadhihaki ' Wazee wa JWTZ naona sasa umeanza ' Kuwadhihaki ' Wazee wa PT. Angalia tu usije ukawa umetoka katika afadhali na umeenda katika potelea mbali. Take Care Mkuu!
Haaaaa MKUU Taarifa za awali za Polisi sio za kuziamini sana,ngoja tusikilize upande wa mtuhumiwa wa "ULEVI WA KUTOJITAMBUA". Rejea Taarifa za Polisi zilivyojichanganya kwenye matukio mbalimbali kama la Akwilina,Nondo etc
 
Nakuonea huruma sana Mkuu. Nakuomba tena kwa kukuambia kuwa ' take care ' Mkuu. Usiseme hatukuambia mapema.
 
Taarifa ya Polisi ina ukakasi mwingi, ngoja kwanza tupate taarifa za mkewe ambaye inadaiwa alimkatalia kumfumgulia mumewe

Hata hivyo hii story imavyohadithiwa na Polisi ni kama vile movie, kwa kuwa wao wanaelewa kila kitu ya tukio zima lile.......

Wameweza kueleza jinsi nyendo za huyo mwandishi zilivyokuwa siku hiyo pamoja na hayo majina ya "mabarmaid" aliokunywa nao huyo mwandishi!

Sasa mtu pekee atakayetupa "ukweli" wa jambo hili ni mke wa mwandishi huyo ambaye inadaiwa kuwa aligoma kumfungulia "mlevi" huyo Mara 2 usiku huo, jambo lililomsababisha mwandishi huyo kukutwa na maswaiba hayo
 
Nyumbu hawatapenda hii taarifa kwa kuwa wanataka habari za kutekwa tu ila ndo ukweli

*TAARIFA YA MWANDISHI WA GUARDIAN KULEWA BILA KUJITAMBUA*

Mnamo tarehe 08/04/2018 majira ya Saa 1:30 asubuhi eneo la Bunju A Mianzini mwandishi wa habari aitwaye *Finnigan Frazer Simbeye*,47 yrs Mkristo mwandishi wa habari wa gazeti la Guardian Mnyiha,mkazi wa Bahari beach mtaa wa kondo alikutwa amelewa bila kujitambua na kukutwa amelala mtaroni jirani Bagamoyo road.

Taarifa kamili ni kwamba mnamo tarehe 07/04/2018 Majira ya saa 4:00 asubuhi alitoka nyumbani kwake Bahari beach akiwa na gari lake T383 BCU Toyota Mark ll kwenda Tegeta Kibo ambako aliiacha gari pale na kwenda eneo la Mwenge na baadae alirudi Tegeta kibo na kuchukua gari lake hadi Ununio katika bar ya *Bajet* na baadae alirudi Tegeta darajani katika bar ya *B &DG* ambako alikutana na hawala yake aitwaye *Tonto* mkazi wa Salasala na hapo alikunywa bia 8. Ilipofika saa 1:00 hrs usiku alikwenda katika Bar ya *QR* eneo la Azania Tegeta na kukutana na hawala yake mwingine mhudumu wa Bar hiyo anayeitwa *Grace* na kuendelea kunywa pombe!!!.
Ilipofika saa 3:00 usiku alikwenda katika bar ya *Benten* na kuendelea kunywa na pale alikunywa bia chupa 6 na baadae aligundua kuwa amelewa sana,na hapo hawala yake *Grace* alimshauri watafute Guest walale lakini wakati wakienda gari lake liliingia katika dimbwi la maji na kuzimika na alipoomba msaada wa kulitoa ikashindikana hivyo akaliacha hapo hapo na wakati huo huo hawala yake *Grace* alichukua simu yake ya Smart Phone aina ya *LG* na kuondoka huku akimuacha pale.

Majira ya saa 10:00 usiku alichukua bodaboda kwenda nyumbani kwake Bahari beach ambako aligonga lakini hakufunguliwa na baada ya kutofunguliwa aliamua kwenda tena katika Bar ya Kibo ambao alifika saa 11:00 alfajiri na kukuta watu wanatoka na Bar ikiwa imefungwa,hivyo kuchukua bodaboda kurudi nyumbani tena lakini pia hakufunguliwa na kwa kuwa alikuwa amelewa sana aliamua kuondoka na hakukumbuka tena kinachoendelea hadi asubuhi anajikuta yupo Mwananyamala Hospitali.
Katika mahijiano tumegundua kuwa mwandishi huyo amekunywa pombe sana na kulewa kushindwa kujitambua, amekutwa na ufunguo wa gari lake mfukoni mwake akiwa hospitali na hana jeraha,uvimbe wala mikwaruzo yoyote mwilini, amewekewa dripu za maji na anaendelea vizuri japo bado amelazwa Hospitali Mwananyamala .

Tayari polisi amefunguliwa jalada Kosa la *KULEWA BILA KUJITAMBUA WMB /IR/1565/2018* Taarifa za mitandao kuwa ametekwa sio kweli.
675cf91f-663f-4e8c-b8a3-43830ad4a184-jpg.737908

mbona hii picha inaonesha kama ana damu kichwani!?
 
Nitawaomba sasa wale ' Mashambenga Original ' wa humu Jamvini ambao yakitokea tu ' matukio ' kama haya huwa wanakuwa wepesi mno kufanya ' Speculations ' zao kuwa ' Mamlaka ' ndiyo iliyoko nyuma ya mambo yote haya wakati kumbe ni ukweli usiopingika kwamba 80% ya ' matukio ' ya Kutisha kama siyo ya Kusikitisha hutokana na mambo ya Mtu tu Binafsi na ' Washirika ' wake katika harakati zake za Kimaisha na hapa pia tunaweza sasa kupata jambo kwamba huenda hawa Watu tuliowa ' brand ' wasiojulikana wanafanya ' matukio ' kwa ' agenda ' zao na hao Wahusika huku wakiwa wanasafiria ' nyota ' iliyochafuliwa na isiyopendwa ya ' Mamlaka ' ili tu kuweza kuficha ' uhalifu ' wao. Niliwahi siku moja kusema humu humu kwamba kuna Siku wale ' Mashambenga Original ' watakuja ' Kuumbuliwa ' hasa pale ukweli kuhusu haya ' matukio ' utakapojidhihiri / wekwa wazi. Ni suala la muda tu!

Uko sahihi, lakini hukupaswa kuwa na upande hadi mwisho wa saga!! Mzee wa mazoezi pale Muhimbili!!!
 
Nakuonea huruma sana Mkuu. Nakuomba tena kwa kukuambia kuwa ' take care ' Mkuu. Usiseme hatukuambia mapema.
Mkuu, tafadhali tusitishane...alichokisema ni kweli kwa asilimia mia moja! kwani kosa lake nini? kwa nini mnapenda tisha tisha tactic! mujewe kwa wakati huu tulionao hamuwezi kufanikiwa kwa kutumia mbinu za tisha tisha! Hizo mbinu zimepitwa na wakati mkuu!
 
Back
Top Bottom