Kamanda wa Polisi Arusha kanisikitisha

Katika taarifa ya habari ITV ya sa2 ,nmekutana na habari kwamba kikosi cha polisi kimepambana na majambazi piga nikupige kwa dakika 70 yani lisaa limona na dakika 10.kazi nzuri
Kilichonisikitisha ni kamanda kuongea kwa mbwembwe na kujitapa sana kuwa ile piga nikupige,nikupige piga kwa dakika 70.
Cha ajabu jambazi mwenyewe ni mmoja na amekamatwa na silaha moja na risasi 26 tu.yani muda wote huo kumbe kamtu kalikua kamoja tu halafu kamanda anatamba
Walikuwa wawili dhidi ya kikosi kimoja cha polisi zaidi ya ishirini! Kiasi hicho cha askari waliopata mafunzo ya upiganaji hawakuwa na sababu ya kutumia muda wote huo. Hivi polisi walishindwa kuwazingira? Endapo wangewazingira kusingekuwa na sababu ya kuwaua, kuua wahalifu wa aina hii ni hasara kuliko faida kwani mnaishia kwa mlionao na kuwaacha waliojificha ndiyo sababu inayoendeleza mapambano na wahalifu.
Mwisho jeshi la polisi liache mtindo wa kusherehekea mauaji kwa mtindo wa kisiasa, vizuri kusherehekea wanapowakamata kwani kutakuwa na uwezekano wa kuwapata washirika wao.
 
Hapo timing tuu, sababu polisi na hao majambazi wote wanajua kuzitumia silaha, ukienda kichwa kichwa mnapotezana...

Cc: mahondaw
 
Ayo mazingira sio mchezo walipo kamatwa , ilo ni pori tengefu pasikie tu kwa story kuna mambo mazito uko.
 
Tatizo wanataka kuonekana na jiwe .kwahiyo lazima waite media na kujitapa ili waonekane....yani mixer waride wakati wa kutoa habari

Back
Top Bottom