Kamanda Sirro pia amulikwe kwenye tuhuma za rushwa na unyang'anyi wa mali

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,386
Nailinganisha 'vita' ya madawa ya kulevya ya Daudi Bashite(Paulo Makonda) sawa na vile vituko vya 'Siku 7' vya Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Augustine Lyatonga Mrema....Mrema alijitajirisha mno kupitia kampeni yake hiyo.

Kwa tuhuma zilizoibuliwa leo hii ni wazi pia kampeni ya Makonda ya ya madawa ya kulevya ilikuwa ni namna yake rahisi ya kujipatia fedha, magari, nyumba na mali zingine kutoka kwa matajiri wakubwa...na hivi majuzi ametangaza kuwalenga wamiliki wa Bureau de Changes...maana mtu unajiuliza, kwanini huyu mtu yeye anaandama wafanyabiashara tu? Manji bila shaka aligoma kutoa hela na sasa wanamsingizia kutokuwa raia na wamemshikilia kwa siku 22 sasa pasipo kumfikisha mahakamani.

Mimi nadhani karma imejibu na sasa wote waliohusika na kadhia hii wamulikwe na wawajibishwe, akiwemo Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro...naamini na yeye amenufaika na uovu hii, lazima kuna uchafu wake tunapaswa kuujua. Wengine twende taratibu ikibidi hata aliyewatuma, hawa jamaa wana ujasiri wa ajabu sana ni vigumu kuamini wanayafanya haya bila nguvu ya kiongozi mkuu

[HASHTAG]#AmkaTanzania[/HASHTAG]
 
Hata yule aliyedai kukataa milioni hamsini za shisha naye achunguzwe,tutaamini vipi kuwa alizikataa hizo fedha wakati hakutoa ushahidi wowote unaonyesha kuwa alizikataa hizo fedha,ukizingatia kuwa ni mtu anayejidai kuwa ana pambana na maovu,ilikuwaje siku hiyo waovu anaopambana nao wakamwendea ofisini kwake na kielelezo halafu aseme kuwa aliwaachia?.
 
Ningekuwa rais ningetafuta namna nzuri ya kudeal na yule dada badala ya kutumia nguvu!
Kwa kufanyia kazi zile tuhuma no matter what hata kama nitaonekana nimempa credit za bure huyu mange na kuwashughulikia waliotajwa wote!

Maana naona anazidi kuwavua nguo!

Kama marekani na teknolojia yao yote Edward snowden aliwatesa sembuse bongo hii!

Ona sasa barua iliyotumwa kwa siri imevuja!
"if you can't fight them join them ndio option iliyobaki"
 
Sirro nitamtetea mpaka siku ya kiama,ukimuangalia usoni Sirro hayuko happy huyu dogo janja anampelekesha bila kujali umri wala adhi yake,kampeni hii Sirro hakutaka iendeshwe hivi
 
Nailinganisha 'vita' ya madawa ya kulevya ya Daudi Bashite(Paulo Makonda) sawa na vile vituko vya 'Siku 7' vya Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Augustine Lyatonga Mrema....Mrema alijitajirisha mno kupitia kampeni yake hiyo.

Kwa tuhuma zilizoibuliwa leo hii ni wazi pia kampeni ya Makonda ya ya madawa ya kulevya ilikuwa ni namna yake rahisi ya kujipatia fedha, magari, nyumba na mali zingine kutoka kwa matajiri wakubwa...na hivi majuzi ametangaza kuwalenga wamiliki wa Bureau de Changes...maana mtu unajiuliza, kwanini huyu mtu yeye anaandama wafanyabiashara tu? Manji bila shaka aligoma kutoa hela na sasa wanamsingizia kutokuwa raia na wamemshikilia kwa siku 22 sasa pasipo kumfikisha mahakamani.

Mimi nadhani karma imejibu na sasa wote waliohusika na kadhia hii wamulikwe na wawajibishwe, akiwemo Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro...naamini na yeye amenufaika na uovu hii, lazima kuna uchafu wake tunapaswa kuujua. Wengine twende taratibu ikibidi hata aliyewatuma, hawa jamaa wana ujasiri wa ajabu sana ni vigumu kuamini wanayafanya haya bila nguvu ya kiongozi mkuu

[HASHTAG]#AmkaTanzania[/HASHTAG]
Nani wa kuwachinguza? Kuna msemo tuliyomo enzi zetu kama ilivyo na kwenye biblia takatifu "like father like son"
 
Ningekuwa rais ningetafuta namna nzuri ya kudeal na yule dada badala ya kutumia nguvu!
Kwa kufanyia kazi zile tuhuma no matter what hata kama nitaonekana nimempa credit za bure huyu mange na kuwashughulikia waliotajwa wote!

Maana naona anazidi kuwavua nguo!

Kama marekani na teknolojia yao yote Edward snowden aliwatesa sembuse bongo hii!

Ona sasa barua iliyotumwa kwa siri imevuja!
"if you can't fight them join them ndio option iliyobaki"
Na ndiyo Maana wewe Siyo rais kwa sababu ungewapa taabu sana hawa jamaa. Niliwahi kuandika hapo zamani hakuna mtu hata mmoja aliye msafi ndani ya mfumo huu. They are all rotten. Na kama unafuga samaki baba yao akioza kichwa hakuna namna nyingine. dawa yake ni kutafuta a new species uwafuge tu. I think you understand what I mean
 
Kwakweli mimi sipendagi polisi lakini kwa hili siro sidhani kama anahusika coz hata body language yake haionyeshi kabisa kama anajua kinachoendelea au may be anajua but what could he do naye ni mpokea amri. Kwahili sitamvisha taji la miba Kamanda Siro but kwa maadili ya kikazi na ushahidi wote huu asipoufanyia kazi then hapo ndio ntamvua vyeo vyote na.manyota yake ....ingawa pia this is africa najua anatamani afanye kazi yake ipasavyo but mikono lazima iende kinywani so anaogopa kigusa mtoto wa mkulu
 
Mmmh ifike mahali tuambiane ukweli kama rais anaweza kwani sisi wananchi tusihoji,naunga mkono,bashite toa vyeti vyako na nyaraka za hayo wewe siro taja mali zako!
 
Na ndiyo Maana wewe Siyo rais kwa sababu ungewapa taabu sana hawa jamaa. Niliwahi kuandika hapo zamani hakuna mtu hata mmoja aliye msafi ndani ya mfumo huu. They are all rotten. Na kama unafuga samaki baba yao akioza kichwa hakuna namna nyingine. dawa yake ni kutafuta a new species uwafuge tu. I think you understand what I mean
Nimekuelewa sana mkuu
 
Inashangaza sana kuona mkurugenzi wa Takukuru yupo ofisini narushwa kubwa namna hii zikiendelea. Naweza sema hakika hakuna taasisi duni kama Takukuru. Wanazuia rushwa gani iwapo mkuu wa mkoa anamiliki migari na mijumba ya kifahari huku akiws na mwaka tuu kazini. Hivi mtu huyu akikaa miaka aliyokaa Lowassa ama Kingunge si atamiliki dar nzima. Bashite dangote
 
Wamulikwe na nani wakati wao ndo walitakiwa wammulike makonda? Kama mambo yako hivyo unawezaje kumshawishi mtu mwenye akili timamu akubali kwamba Tanzania kuna serikali?
 
Siro anayo haki ya kujua na kuhoji. Sasa kama yeye hajui si aulize? Kama haulizi maana yake anajua kinachoendelea. Tunamuweka katika kundi moja.
 
Siro hovyo sana. Nilimdharau siku Ile akihojiwa nakuturingia etivanasumbiliwa na wanawake Kwa kupigiwa simu hadi usiku wa manane wakimsifu eti yeye ni hendsam boy.
 
Bashite asingeweza kufanya umafia mkubwa kiasi hiki bila kuwa na JITU kubwa nyuma yake
Kama alimtimua nduguye 'Chapombe' kwa nini amlinde huyu?
Kuna kolabo kubwa sana kwenye muziki huu
 
Kwa wanaojua polisi wanaamini fika sirro lzma anahusika hapa na njia pekee alioje ga makonda kula mpk kupitiliza ni kumshirikisha sirro sasa ttz mi kwamba makonda ulimbukeni unamsumbua yy anataka magari wakat akina sirro wakongwe wa hizo kazi wao wanataka muamala tu hapo ndipo alipoharibu dogo
 
Kwakweli mimi sipendagi polisi lakini kwa hili siro sidhani kama anahusika coz hata body language yake haionyeshi kabisa kama anajua kinachoendelea au may be anajua but what could he do naye ni mpokea amri. Kwahili sitamvisha taji la miba Kamanda Siro but kwa maadili ya kikazi na ushahidi wote huu asipoufanyia kazi then hapo ndio ntamvua vyeo vyote na.manyota yake ....ingawa pia this is africa najua anatamani afanye kazi yake ipasavyo but mikono lazima iende kinywani so anaogopa kigusa mtoto wa mkulu
Kwa nn mnadeal na Siro na sio Mangu?

Sent from my Lenovo A2010-a using JamiiForums mobile app
 
Sirro nitamtetea mpaka siku ya kiama,ukimuangalia usoni Sirro hayuko happy huyu dogo janja anampelekesha bila kujali umri wala adhi yake,kampeni hii Sirro hakutaka iendeshwe hivi

Mkuu huko kwetu kuna msemo unasemaga..'usimwapie mtu" kwa tafsiri isiyo rasmi.

Yaani ni kwamba mtu/mtoto wako anaweza kutuhumiwa kuwa ni mwizi..wewe ukatoka ukaapa kwa jina la Mungu kuwa huyu mtu/mtoto sio MwiZi kumbe.....??

Mkuu moyo wa mtu ni kichaka...elewa tu hvo...tusije tukakimbiana hapa siku zijazo.

Kuna watu hapa walikuwa ukimsema Makonda negatively walikuwa wanatamani ungekuwa karibu yao wakuzabe kibao ila tangia asubuhi hawajaonekana humu.
 
Back
Top Bottom