nyamadoke75
Member
- Apr 1, 2020
- 93
- 288
Mahakama ya kijeshi la jeshi la polisi imewatia hatiani wakaguzi waandamizi wanne wa polisi mkoani Arusha kwa makosa matatu ikiwemo kushawishi na kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 na kuachia madawa ya kulevya aina ya mirungi kilo zaidi ya 1200 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60 katika tukio lililotokea Desemba 5 mwaka jana eneo la Burka kata ya Elerai ndani ya jiji la Arusha majira ya saa 5 asubuhi. Mahakama hiyo iliteuliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini {IGP} Cmilius Wambura iliongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa njia ya kisayansi Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara {SSP} Msongalaza akisadiwa na Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasi mkoa wa Manyara {FFU} Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi {ASP} Meniko iliwatia hatia vigogo hao Julai 3 mwaka huu wakati wakisomewa mashitaka yao katika kituo cha polisi cha utalii mkoa wa Arusha.
Vigogo wa polisi waliotiwa hatiani kwa makosa hayo matatu ni pamoja na Mkaguzi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Arusha, Mwinyimvua Shomari ambaye yuko ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha {RPC} Justin Masejo. Wengine walikutwa na makosa ni pamoja na Mkaguzi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Yahaya Mokiwa ambaye yuko kituo cha polisi Post Soko la Tengeru wilayani Arumeru mkoani Arusha, Mkaguzi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Riziki Khatibu ambaye yuko ofisi ya Kamanda Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha {RPC} Masejo na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi aliyetambuliwa kwa jina moja la Rashid ambaye yuko kituo chake cha kazi ni polisi uwanja mdogo wa ndege Kisongo Air Polisi Port Arusha. Shitaka lingine walilokutwa na hatia vigogo hao wa polisi Arusha ni pamoja na kwenda kinyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi na shitaka la tatu walilokutwa vigogo hao wa polisi Arusha ni pamoja na kuachia baadhi ya watuhumiwa wa tukio hilo pamoja na kuachia baadhi ya vielelezo ikiwemo gari na madawa ya kulevya aina ya mirungi.
Habari kutoka ndani ya jeshi hilo mkoani Arusha zilisema kuwa baada ya kutiwa hatia watuhumiwa hao kwa makosa hayo matatu viongozi wa mahakama hiyo ya jeshi la polisi waliwaeleza watuhumiwa kuwa uamuzi huo wa mahakama ya kijeshi wanaupeleka mamlaka za juu za Jeshi la Polisi nchini kwa hatua zaidi za kinidhamu. Awali wakaguzi hao baada ya kufanya tukio hilo walifunguliwa jalada la uchunguzi katika kituo kikuu cha polisi Arusha lenye namba ARS/IR/10741/2023 na kufanyiwa mahojiano na habari zilisema kuwa vigogo hao wa polisi mkoani Arusha walikamata gari aina Prado yenye namba za usajili T683DZZ rangi ya silver iliyokuwa na mirungi kilo 1200 na watuhumiwa wawili waliokuwa ndani ya gari hilo likiwa na madawa hayo haramu muda huo eneo ya Burka njia ya By Pass ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Vigogo hao walishawishi na kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 lakini walifanikiwa kupata rushwa ya shilingi milioni 6 kwa makubaliano ya kuacha baadhi shehena ya madawa kilo 496 waliyoibeba katika gari nyingine aina ya Toyota Mark 11 yenye namba za usajili T536BQB kwa lengo la masharti ya kumaliziwa kiasi kilichobaki cha shilingi milioni 4 ili wakabidhiwe madawa hayo.
Vyanzo viliendelea kusema kuwa majira ya saa 7.15 usiku wa Desemba 6 mwaka jana taarifa ya kukamatwa kwa mirungi katika eneo hilo zilimfikia Mkuu wa Polisi Arusha {OCD} na yeye kuweka mtego wake kwa kutumia gari mbili za doria zinazotambuliwa kwa jina la chita 5 na chita 7 kwenda eneo la tukio. Habari zilisema kuwa magari hayo ya doria yalikuwa yakiongozwa na askari kanzu mbobevu Sajenti Abdallah Haji hadi eneo la tukio lakini walipofika eneo la tukio walikutana na upinzani mkali kwani waliokamata mirungi na kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 wana vyeo vya juu kuliko Sajenti Haji. Vyanzo ndani ya Jeshi la Polisi vilisema kuwa baada ya Sajenti Haji kukutana na upinzani huo na kutakiwa kuondoka eneo la tukio, Sajenti huyo alimpigia OCD George Malewa kumweleza hali hiyo na vigogo hao walivyosikia sauti ya Kamanda Malewa waliamua kutimua mbio na OCD alimwamuru Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Kulewa Mziray kwenda kuongeza nguvu katika eneo la tukio hilo. Habari zilisema kuwa baada ya Mkaguzi Msaidizi Mziray kufika eneo hilo alimkamata Alfayo akiwa katika gari Toyota Mark 11 akiwa na mirungi kilo 496 na hadi sasa Alfayo yuko magereza kwa kesi ya kusafirisha mirungi na kesi hiyo haina dhamana kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai.
Wakati huo huo kikao kingine cha mahakama ya jeshi la polisi ilimkuta na hatia Mkaguzi Mwandamizi wa Polisi, Deo Babile baada ya kukutwa na hatia ya kushawishi na kuomba rushwa ya shilingi milioni 6 baada ya kumkamata raia mwenye asili ya Kisomali, Mohamed Al Nour aliyeingia dola 600,000 kwa njia za panya eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru mkoani Arusha. Tukio hilo lililotokea Novemba 10 mwaka jana ambapo Mkaguzi Babile alikuwa na askari watatu ambao wote wameshafukuzwa kazi mapema mwaka huu baada ya wote kukiri kosa na kurudisha fedha mbele ya Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Kamishina Msaidizi, Justine Msejo kiasi cha shilingi milioni 6 kwa Al Nour.
Kesi ya Mkaguzi Babile, mahakama iliongozwa na Mrakibu Msaidizi wa Polisi {ASP} Asia Matauko kutoka ofisi ya Kamanda wa Polisi Kilimanjaro ambapo mtuhumiwa alikutwa na shitaka moja la kushawishi na kuomba rushwa baada ya kukiri mbele ya Kamanda wa Polisi mkoani Arusha. Hakimu wa mahakama hiyo alisema kuwa uamuzi wa kesi hiyo ameupeleka kwenye mamlaka za juu za Jeshi la Polisi Tanzania kwa maamuzi mengine.