Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,067
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Simon Siro, amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye ni shabiki na ‘anazikubali’ nyimbo za Icon Diamond Plutnumz.
Akizungumza kupitia kipindi cha Sun Rise cha Times Fm, Siro amesema pia ana hamasika na hatua aliyopiga kimaisha Diamond na amewataka wanamuziki wengine kuiga mfano wake.
“Kiukweli hakuna nyimbo ya Diamond ambayo siikubali, zote nazipenda, anajua nini anafanya angalia mafanikio aliyoyapata yamekuja baada ya kujituma na kuimba vizuri, naomba niseme mimi ni shabiki wake mkubwa kwakweli.
“Kila nyimbo yake mimi naikubali aisee, anafanya kazi nzuri na ni mfano wa kuigwa” alisema Kamanda Siro.
Chanzo: Times FM
My Take:
Si ajabu Kamanda kashacheza sana Ngololo, Mdogomdogo na Moyo wangu akiwa ofisini au sebuleni kwake kupunguza stress.. Kazi zao ngumu hizi jamani!