Mkubwa Fella adai hakuna msanii anastahili kulinganishwa na Diamond Platnumz Bongo

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
410
1,000
Meneja wa Diamond Platnumz, Mkubwa Fella amesisitiza kwamba mwanamuziki anayewakilisha ndiye kigogo wa muziki nchini Tanzania.

Akiwa kwenye mahojiano ya hivi majuzi na Mbengo TV, Fella ambaye pia ni mwanasiasa alisema kwa sasa hakuna mwanamuziki anayestahiki kulinganishwa na Diamond Platnumz kote Bongo.

Meneja huyo aliwasihi Watanzania waache kujaribu kumshindanisha Diamond na wanamuziki wengine wa Bongo huku akisema kiwango chake ni cha kimataifa.

"Diamond ashindanishwe na mtu ambaye anaweza kustahiki kushindanishwa naye. Hapa Bongo jamani watu waache kwanza. Huko mwanzo tulikuwa tunatafuta numba, lakini sasa hivi ashakuwa mwakilishi wa taifa letu. Lazima tuwe wapana kidogo kuzungumzia hili. Tusiseme kwamba anaweza kashindanishwa na mtu fulani, hamna!" Fella alisema.

Fella alidai hata mmiliki wa lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize hajatosha mboga kuwekwa katika nafasi moja na bosi wake wa zamani.

"Watu wakimshindanisha Harmonize na Naseeb wanafeli. Harmonize ametengenezwa na Naseeb. Harmonize ana nafasi yake na Diamond ana nafasi yake zaidi. Diamond kwa Harmonize anasimama kama baba. Ukimfananisha mtu na babake ni uongo" Alisema Fella.

Fella hata hivyo alimkubali Harmonize kama msanii mkubwa ambaye anafanya vizuri katika nafasi yake

images (8).jpeg
 
Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
21,971
2,000
Anaposema hakuna wa kumshindanisha anatakiwa aweke wazi hakuna kumshindanisha kwenye kipengele gani

Umaarufu?

Kama umaarufu naweza kuungana naye kwa hilo, diamond amekuwa maarufu sana nje na ndani ya ya tanzania. Na tena kuna hadi ule umaarufu alioupata ambao haujachangiwa na muziki saizi tunaita kiki, lakini pamoja na hayo bado nitapinga nikiskia anaitwa super star.

Kimuziki?

Hapa napo zipo factors za kuangalia, kama mlinganisho uta-base kwenye mauzo na views bado ataendelea kuwa on top

Trend?

Kama trend hii haiko costant kulingana na misimu, haijalishi diamond ana fan base kubwa kiasi gani ila kuna wasanii na wanaojitokeza na kuvuma sana na kuteka media kufanya waongelewe wao tu katika hiyo season. Hapa naweka mfano wa darasa kwenye maisha na muziki namna alivyo trend japo huyo diamond naye aliachia ngoma yake lakini ilifichwa.

Pesa?

Hapa kwenye pesa ni siri ya mtu, kama fella kasema diamond hana msanii wakushindana naye kwa kigezo cha pesa basi ni wazi kuna mtu ambaye alikua amem-target hakutaka kwenda direct.

Wasanii wenye pesa kumzidi diamond wapo, utofauti unaookuja ni kwamba watu wengi wamejikita kumfuatilia msanii ambaye ni maarufu. Yani ni sawa useme ukiitoa club ya simba hakuna mchezaji anayeshiriki ligi ya NBC mwenye kiwango kumzidi mayele

Huyo mayele kwasababu yupo kwenye timu kubwa yenye wadau wengi anakuwa na muda mwingi wa kutazamwa zaidi kuliko moses george wa geita gold.

Lyrical na delivery?

Hapa sasa huwezi kumuona diamond wala crew ya wcb iki fit kwenye hii category. Hiki ni kipengele kimoja kigumu sana na ndio maana wanaoweza kufanya hiki wanaitwa wagumu.

Kwa hiyo kama fella alimaanisha diamond hakuna wa kumlinganisha naye hapa bongo naweza nikakubaliana naye kwa vingine ila kwa hapa tutakesha

Huwezi ukasema diamond ni mkali kimashairi kuliko dizasta, p mawenge, nikki mbishi, songa, nash mc, ghetto ambassodor, nala mzalendo nk.
 
herman joshua

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
1,896

Mshairi bora n Dzaster tu hapo, kidogo na Songa,
Afu naona umebez kwa tamaduni tu, kwamba Nacha, Mwana FA, Fid Q, huwafahamu....?
 
herman joshua

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
1,896
2,000
Tamaduni ndiko mitutu inako fichwa, huyo nacha sijawahi kumuelewa

Fid Q wa mara ya mwisho naye mkubali ni yule wa sumu, mwana Fa sio sanaaa
Tamaduni hakuna zaidi ya Dizasta labda nimuongeze One na Songa wengine wakawida tu.
 
Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
21,971
2,000
Tamaduni hakuna zaidi ya Dizasta labda nimuongeze One na Songa wengine wakawida tu.
Story teller dizasta ni on top, kwa michano ya punch lines na diss namuweka mawenge na nikki

Songa kwa rap comedy pamoja na kucheza na maneno ni hatari, kadgo kwa miondoko ya huzuni yuko vizuri

One kwa mistari fikirishi ni mbaya, yani kuna nyimbo nimekuja kuzielewa juzi yani siku zote nilikuwa naziskiliza ila sijawahi kudecode
 
DON

JF-Expert Member
May 6, 2008
921
1,000
Anaposema hakuna wa kumshindanisha anatakiwa aweke wazi hakuna kumshindanisha kwenye kipengele gani

Umaarufu?
Kura zetu ndizo zimemfikisha hapo, hana ubunifu wa beat ya muziki inayomtambulisha yeye. Apige na band live ataonyesha ukomavu wake
 
Yehoshafati

Member
Apr 7, 2021
50
125
Anaposema hakuna wa kumshindanisha anatakiwa aweke wazi hakuna kumshindanisha kwenye kipengele gani

Umaarufu?

Kama umaarufu naweza kuungana naye kwa hilo, diamond amekuwa maarufu sana nje na ndani ya ya tanzania. Na tena kuna hadi ule umaarufu alioupata ambao haujachangiwa na muziki saizi tunaita kiki, lakini pamoja na hayo bado nitapinga nikiskia anaitwa super star.
Nje ya mada Mayele alikufanya nini? Maana naona anakukosesha sana raha
 
mludego

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
1,816
2,000
Story teller dizasta ni on top, kwa michano ya punch lines na diss namuweka mawenge na nikki

Songa kwa rap comedy pamoja na kucheza na maneno ni hatari, kadgo kwa miondoko ya huzuni yuko vizuri

One kwa mistari fikirishi ni mbaya, yani kuna nyimbo nimekuja kuzielewa juzi yani siku zote nilikuwa naziskiliza ila sijawahi kudecode
Umechambua vizuri sana ni kama tunafanana, vipi khs kina ghetto ambassadors, ZaiiiD,nash mc,hivi kilinge bado kipo?
 
Feisal2020

JF-Expert Member
Nov 15, 2018
544
1,000
Star ni kama ki tiny tu kilicho jichomoza angani kinaonekana kwa mbali sana na tena kwa kufifia fifia na kukiona sometimes mpaka ufumbe jicho moja au utumie binocular ya galileo

Afu superstar hizi ndo zile nyota za kibishi ambazo hadi mchana zinaonekana
Kwa hiyo tunaweza ku conclude kuwa Tanzania hakuna super star?
 
Feisal2020

JF-Expert Member
Nov 15, 2018
544
1,000
Tamaduni hakuna zaidi ya Dizasta labda nimuongeze One na Songa wengine wakawida tu.
Dizasta ni amekamilika kwa kila kitu, hakuna msanii (awe wa kuimba au kuchana) alie master art ya story telling zaidi ya, au kama Dizasta... Hayupo na hajawahi kuwepo! Dizasta akiamua ku flow pia ni mbaya mno, sikiliza zile nobody's safe!

One is the most underrated MC kwa hapa Tz... Nafikiri ni kwa sababu anaandika kwa namna ambayo watu wanaita kigumu sana.

Songa mkali tu wa kuchezea maneno na mistari ya kuchekesha chekesha, ila hafikii hata nusu ya uwezo wa hao hapo juu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom