Kamanda Sirro atangaza oparesheni maalum kwa wenye vyeti vya kugushi

Heee!!! Sekta ya polisi ambayo jukumu lake kuu na la msingi ni ulinzi na usalama wa Raia na Mali zao limebadilika na kuwa katika sekta au wizara ya elimu????
Tafadhali mnisaidie hili to me is very incredible as I see ni kama interaction of responsibilities,roles & accountabilities.
 
View attachment 365614

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro amewataka wale wote waliyo na vyeti vya kugushi (vyeti feki) wajisalimishe mapema kwa jeshi hilo kabla ya kuanza kwa oparesheni maalum utakaowabaini na kuwachukulia hatua za kisheria.

Kamanda Sirro ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar na kuongeza kuwa, watuhumiwa wamekuwa wakibanwa na kuwataja baadhi ya vigogo wa seriaklini kuwa ndiyo wanaohusika kuwatengenezea vyeti hivyo na kwamba huvitumia vyeti hivyo walivyotengenezewa kwa kuajiriwa serikalini na taasisi nyingine.

===================

Watu watatu wanaosadikiwa kuwa vinara wa kutengeneza vyeti bandia pamoja na nyaraka mbalimbali za Serikali wamekamatwa eneo la Buguruni wakiwa na mitambo yao.

Kukamatwa kwao kulitokana na msako mkali uliofanywa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam hivi karibuni na hatimaye watuhumiwa walinaswa wakiwa nyumbani wanakoishi eneo la Buguruni Ghana wakitengeneza nyaraka bandia.

Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Ashraff Maumba (37) mkazi wa Buguruni Ghana, Mwamba Seif (38) mkazi wa Mnyamani, na Mahmudu Zuber (24) mkazi wa Buguruni.

Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba Julai 8, saa 4.00 usiku walifanya upekuzi katika nyumba wanayoishi na kukuta nyaraka mbalimbali vikiwamo vyeti bandia vya kidato cha nne 50 na vyeti vya vyuo vya uuguzi.

Kamanda huyo alisema nyaraka nyingine bandia zilizokamatwa ni stika 20 za Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), vyeti vya kuzaliwa 10 na vya Chuo cha Ufundi (Veta).

Nyaraka nyingine zilizokamatwa, kwa mujibu wa Sirro ni leseni za biashara, stika 100 za bima za magari, mitambo na vivuli 10 bandia vya vyeti vya Chuo cha Biashara (CBE).

Katika upekuzi huo pia walikamata mihuri mbalimbali ya ofisi za Serikali na binafsi ukiwemo muhuri wa Bibi na Bwana.

“Tulifanikiwa kukamata vifaa mbalimbali vya kutengenezea nyaraka zikiwamo karatasi maalumu zilizo na nembo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kutengeneza zaidi ya kadi 500 za vyombo vya moto, kompyuta nne na mashine moja ya kuchapisha,” alisema Sirro.

Kamanda Sirro alisema watuhumiwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi huku upelelezi ukiendelea na ukikamilika watafikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka yanayowakabili.

Katika hatua nyingine, Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo alisema Serikali haitakubali kuhujumiwa na watu wachache hivyo itachukua hatua kali kwa wote wanaojihusisha na utengenezaji vyeti bandia vya Serikali.


“Tunashukuru jeshi la polisi kuibua shina ambalo lilikuwa linatusumbua sana kutambua ni wapi wanatengeneza vyeti hivi vya bandia na tumepata taarifa za mawakala wanaofanya ujanja huo,” alisema Chibogoyo.

Angeanza na bashite...
 
Sirro anatia Huruma

Bashite kamuhangaisha na kumshusha kumbe jamaa nae kagushi

Nashangaa Sirro na timu yake wameshindwa kumbaini Bashite.


Tanzania Ngumu sana

Inaongozwa na bichwa box
 
Watu wenye vyeti halisi hawapewi Ajira, walio na ajira vyeti feki, hafu wanaagza vjana wajiajir, ***** kabsa! Toen wote ili haki itendeke,
 
Safisha safisha
Naona Tanzania inakuwa ya viongozi makini na wenye vigezo.
Mambo yakuishia form Six ZERO
Nakuongoza Watu wenye Elimu zao
Mwisho 2015
Unaionaje Six Zero na Four Zero sasa? Ilikuwaje hakukamatwa?
 
zoez la uhakiki limeshawashinda hao kwa bado watumishi karibu 80% wanatumia vyet vya kughushi, matokeo yake wanaacha kupambana nao ndio kwanza wanatuambia sisi raia ndio tuwatajie sasa si wanataka kutugombanisha na watu?
 
Jamaa walituingiza mjini kwenye hili .... kwa kweli siwaamini tena.

Hivi kuna operation gani imeanzishwa na ikafanywa na kufanikiwa katika awamu hii. Mkuu wa Nchi majuzi kadai bado anashughulika na HEWA .... Hizi hewa hazitakwisha.
 
Vyeti feki vingi sana kitaani ila wahusika wakipewa taarifa hawashughulikii hata kidogo, NECTA wakipewa taarifa wapo kimya kama hawajui vile. Tatizo lipo tena linaanzia palepale NECTA

Yule aliyekuwa mkuu wa NACTE Nkwera si alikuwa na PhD fake mpaka kakimbia kazi ili Prof Ndalichako asimnase? Sasa kama viongozi ndo wenye vyeti fake hii vita haitaanza Leo wala kesho for certain!!!!
 
Back
Top Bottom