Kamanda Sirro atangaza oparesheni maalum kwa wenye vyeti vya kugushi

Safisha safisha
Naona Tanzania inakuwa ya viongozi makini na wenye vigezo.
Mambo yakuishia form Six ZERO
Nakuongoza Watu wenye Elimu zao
Mwisho 2015
hahaha wakati unayaongea haya hukujua kuwa kuna Daudi Bashite yatakuja kumkuta??? manake sasa hivi unamtetea kweli
 
View attachment 365614

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro amewataka wale wote waliyo na vyeti vya kugushi (vyeti feki) wajisalimishe mapema kwa jeshi hilo kabla ya kuanza kwa oparesheni maalum utakaowabaini na kuwachukulia hatua za kisheria.

Kamanda Sirro ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar na kuongeza kuwa, watuhumiwa wamekuwa wakibanwa na kuwataja baadhi ya vigogo wa seriaklini kuwa ndiyo wanaohusika kuwatengenezea vyeti hivyo na kwamba huvitumia vyeti hivyo walivyotengenezewa kwa kuajiriwa serikalini na taasisi nyingine.

===================

Watu watatu wanaosadikiwa kuwa vinara wa kutengeneza vyeti bandia pamoja na nyaraka mbalimbali za Serikali wamekamatwa eneo la Buguruni wakiwa na mitambo yao.

Kukamatwa kwao kulitokana na msako mkali uliofanywa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam hivi karibuni na hatimaye watuhumiwa walinaswa wakiwa nyumbani wanakoishi eneo la Buguruni Ghana wakitengeneza nyaraka bandia.

Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Ashraff Maumba (37) mkazi wa Buguruni Ghana, Mwamba Seif (38) mkazi wa Mnyamani, na Mahmudu Zuber (24) mkazi wa Buguruni.

Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba Julai 8, saa 4.00 usiku walifanya upekuzi katika nyumba wanayoishi na kukuta nyaraka mbalimbali vikiwamo vyeti bandia vya kidato cha nne 50 na vyeti vya vyuo vya uuguzi.

Kamanda huyo alisema nyaraka nyingine bandia zilizokamatwa ni stika 20 za Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), vyeti vya kuzaliwa 10 na vya Chuo cha Ufundi (Veta).

Nyaraka nyingine zilizokamatwa, kwa mujibu wa Sirro ni leseni za biashara, stika 100 za bima za magari, mitambo na vivuli 10 bandia vya vyeti vya Chuo cha Biashara (CBE).

Katika upekuzi huo pia walikamata mihuri mbalimbali ya ofisi za Serikali na binafsi ukiwemo muhuri wa Bibi na Bwana.

“Tulifanikiwa kukamata vifaa mbalimbali vya kutengenezea nyaraka zikiwamo karatasi maalumu zilizo na nembo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kutengeneza zaidi ya kadi 500 za vyombo vya moto, kompyuta nne na mashine moja ya kuchapisha,” alisema Sirro.

Kamanda Sirro alisema watuhumiwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi huku upelelezi ukiendelea na ukikamilika watafikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka yanayowakabili.

Katika hatua nyingine, Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo alisema Serikali haitakubali kuhujumiwa na watu wachache hivyo itachukua hatua kali kwa wote wanaojihusisha na utengenezaji vyeti bandia vya Serikali.

“Tunashukuru jeshi la polisi kuibua shina ambalo lilikuwa linatusumbua sana kutambua ni wapi wanatengeneza vyeti hivi vya bandia na tumepata taarifa za mawakala wanaofanya ujanja huo,” alisema Chibogoyo.

Kamanda Sirro.

Hivi hujawahi pita hapa na kusoma habari za huyu kijana wa huko Koromije?
CHADEMA kumshitaki Makonda kwa uvunjifu wa sheria
 
Screenshot_2017-03-08-18-16-26.png

Safisha safisha

Hapa ni kabla Mungu wa Dar hajaguswa
 
Teh teh teh teh wakati anapata mihemko hakujua Bashite ana cheti bandia kumbe ndiyo maana alikuwa anamsonga
 
Kamanda Sirro ulitangaza mwenyewe operesheni ya vyeti fake mbona hujatoa kauli yoyote tangu bashite aingie mitini kwa cheti kanjanja?
 
siku zote ametangaza operation yani Bashite yuko kimya ndo kwanza anampelekesha yeye!
 
Ndio wanaotuharibia nchi yetu!!!/yani zero zero zero zero utendaji zero, uongozi zero, maamuzi zerooooba!?.
 
Heee!!! Sekta ya polisi ambayo jukumu lake kuu na la msingi ni ulinzi na usalama wa Raia na Mali zao limebadilika na kuwa katika sekta au wizara ya elimu????
Tafadhali mnisaidie hili to me is very incredible as I see ni kama interaction of responsibilities,roles & accountabilities.
Kughushi ni kosa la jinai..
 
Back
Top Bottom