Kamanda Sirro ametoa ufafanuzi kuhusu askari aliyefyatua risasi hewani mbele ya Waziri wa zamani

Kumbe mtu asiye na silaha akigoma kutoa gari mnafyatua marisasi hewani?
Hakuna binadamu asiye Na silaha ngumi ni silaha. Kichwa ni silaha mateke ni Silaha. Kwenye Mambo Ya kijeshi hakuna vita ndogo huyo alidinda ndani ya gari unajua kwenye gari alikuwa na Nini? Jimboni kwake kuna magaidi kibao wanaua polisi huwezi jua Na Kama na yeye yumo kwenye huo mtandao. Maana alishawahi poteza (au aligawa kwa magaidi) Bunduki Ya AK 47 ambayo ni silaha ya kivita. Huyo askari ilitakiwa amlenge KaBissa ukitilia maanani Mambo yanayoendelea jimmboni wake. Ukali Na dharau alizoonyesha kwa huyo askari ndizo hizo hizo wanazoonyesha magaidi jimboni kwake wanaoua askari. Vyombo vyote vya ulinzi muunganishe dots na historical background yake kuanzia zile harakati zake za uislamu wa siasa kali na ile Radio waliyotaka kuanzisha akiwa kile chama cha siasa cha itikadi Kali.
 
mimi ni nani? ndio tabia mbaya sana ninayoichukia. NILIAPA KAMWE SITAICHAGUA CCM KWA TABIA HII MBAYA ILIYOENEA MPAKA MAOFISINI.
 
hii nchi ni kama kila mtu analinda cheo chake hata kama atatetea upuuzi,huyu siro ndio anatia huruma kabiisa maskini!
 
Hapana staha ilihitajika yule aliwahi kuwa kiongozi mkubwa serikalini; walahi hawakuhitaji kupeleka gari yard ni kiasi cha kumwelewesha kiungwana "Polite language"
Lugha gani zaidi ya aliyopewa na kuendelea kukataa huku akitoa maneno ya dharau?
 
Kuna watu bado hawataki kukubali ukweli. Kitendo cha askari kupiga risasi ilikuwa njia ya kuwaondoa raia waliokuwa wanakusanyika eneo la tu tukio, huu ndiyo ukweli ingawa wapo wanaojaribu kuupinga kwa sababu tukio hili limechukuliwa kisiasa. Tukumbushane tu ndugu zangu ukiwa raia wa kawaida au kiongozi tii sheria, kauli za unanijua mimi ni nani zitakuweka matatizoni. Hapa Kazi Tu!

Angalau huyo Sirro angesema hivyo tungemuelewa. Naona wewe unafaa kuwa na cheo chake mara mia zaidi yake. Majibu ya watu kama kina Sirro (sitaki hata kumwita kamanda) ndio yanafanya wananchi watilie shaka uhalali wa vyeti vya polisi wetu. Mtu unashindwa hata kuongea sentensi moja yenye logiki ambayo watu wataikubali? Kwanza majibu kama haya yanachangia kufanya raia wawachukie polisi.

Napendekeza Sirro na watu wanaopewa vyeo kama chake polisi wawe wanafanya kozi ya public communication. Vyeo vyao vinawafanya wawe spokespersons wa polisi na wanaongea vituko vitupu wanapohojiwa. Completely first class stinking nonsense.
 
Ukiona polisi wanamfanyia hivyo mtu ambaye wanajua alikuwa waziri tena kwa kosa dogo tu la wrong parking (tena mahali ambapo hakuna kibao kinachokataza ku park) jiulize: Mtu mdogo wangemfanyaje? Si wangemwangukia kwa vitako vya bunduki na kumrusha kichura?
Wangapi wamepigwa? Au unadhani aliyefanya wrong parking ni malima tu dar?
 
Kamanda Siro ni kweli upadri ulikuacha kando kwa sababu kusema ukweli ni mtihani mkubwa hasa pale unahusu upande unakupa mkate wa kila siku. Anyway is good kesi ipo mahakamani na kwa hakika uamuzi utatwambia nani mkweli kati yako na watu wako au X-Minister?
 
hii nchi ni kama kila mtu analinda cheo chake hata kama atatetea upuuzi,huyu siro ndio anatia huruma kabiisa maskini!
Kawaida polisi akisema simama ukagoma akikuwasha risasi usipige yowe kwani hajui kinachokufanya umdindie ni nini waweza kuwa Na bomu mfukoni ndio maana una jeuri. Tii sheria bila shuruti. Ndio maana watu kwenye maandamano hupigwa mabomu wakikataa kutii amri maana hujui huo umati unajidai kitu gani hadi wadharau wenye silaha
 
Malima anatakiwa afunzwe adabu kabisa anawazuia askari kutenda kazi yao kabisa halafu analeta mambo ya unajua mimi ni nani?
 
Ukileta ukaidi hakuna namna nyingine mimi nashauri, wapigwe tu maana hakuna namna! Katika tukio la jana kama angekua ni raia tu wa kawaida, leo ingekua stori nyingine, pale walimheshimu tu.

Tii sheria bila shuruti kama huna undugu na Bashite
Nasubiri kwa hamu siku wakikupiga wewe.
Yaani itakuwa poa sana maana itakuwa ni fundisho kwa wengine wenye wenye mitizamo ya kiovu kama wewe.
 
Hapa kuna tatizo Tena la msingi. Huwezi kufyatua risasi Tena nje shirika la umaja wa mataifa IOM Tena pembeni ya double tree hotel Kuna watalii huko kwa kosa la wrong parking. Busara Sana ziliitajika.
 
Amerithishwa na bashite kuongea kwa kujiamin bila kumumunya maneno ila raia wamezoea kila kitu uongee kwa kunyenyekea daah hapana lile jeshi acha dingi aongee kwa kauli ya kikamanda
 
Nina wasiwasi Kamanda Sirro zaidi ya kuhadithiwa na hao vijana wake hajaona video inayoonesha tukio hilo. Maelezo yake yanakinzana na kinachoonekana kutokea.

Kwanza kabla ya kufyatua risasi hata hawakuwa na mpango wa kumkamata baada ya hasira za jamaa kupanda na kukoki bunduki yake na kufyatua ndo fikra ya kumkamata ilipoanzia. Naona hata gari wanayosema ilipakiwa vibaya walikuwa hawangaiki nayo tena!
 
Tulia hujui sheria, Silaha ni kitendea kazi cha polisi

Ninapenda hizi principles na sheria za wenzetu:
Officers should consider three core questions when determining when, and to what extent, force may be used.

Halafu hii hapa chini ni crucial:
  • the amount of force used must also be reasonable and proportionate and the degree of force used must be the minimum required in the circumstances to achieve the lawful objective, otherwise, it is likely that the use of force will be excessive and unlawful.
 
Kawaida polisi akisema simama ukagoma akikuwasha risasi usipige yowe kwani hajui kinachokufanya umdindie ni nini waweza kuwa Na bomu mfukoni ndio maana una jeuri. Tii sheria bila shuruti. Ndio maana watu kwenye maandamano hupigwa mabomu wakikataa kutii amri maana hujui huo umati unajidai kitu gani hadi wadharau wenye silaha
rules of engagement unazijua?
 
Kwahiyo now ni mpango wa risasi hewani ukigoma kusogeza gari?? Tulipofika anajua Mungu tu. Haya Je risasi ile ingempata mpita njia angeongea haya anayoongea??
 
Wanaomtetea Malima ni sababu hawamjui, dogo ana kiburi sana huyo, ningekuwa Mimi ningemtandika risasi ya paja

Ndugu yangu wee...wenye jeuri wote mjini wangewashwa za mapaja wananchi wengi wangekuwa wanatembea upande upande.....Risasi siyo suluhisho unless tuko vitani. Mbona kuna makubwa yanapita mbele yetu na suluhisho zinatafutwa bila mtutu?
 
Back
Top Bottom