Anyongwe mtu aliyemdanganya Simon Sirro hadi akamfukuza Kazi Afande Meshack Samson Laizer pamoja na kushambuliwa na risasi na Askari wenzie

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Wakuu,

Nahisi Jeshi letu la Polisi limenajisiwa. Bora IGP Sirro ajiuzulu kama ameshindwa kuwatetea na kuwalinda Askari wake. Namshauri Sirro awatetea Askari wake Wanyonge kuliko kujipendekeza kwa Wanasiasa. Nilikuwa Nasikia Sirro ni Mlokole, lakini Ulokole wake nina mashaka nao sababu anautumia kama Kivuli kuficha maovu.

Meshack Samson Laizer, amefukuzwa kazi sababu ya kuwataja Viongozi wa Polisi wanaofanya kazi kinyume na kiapo chao. Kumbe kuna Askari Polisi hadi Vibaka wauaji na Wahujumu uchumi. Afande Samson Baada ya Kuwataja Majina akaanza kuwindwa.

Afande Samson Laizer akatekwa na kuteswa. Baada ya kupona akaanza kuwindwa ili auawe, Askari Polisi wa Sirro wakamfuata kwake wakamfyatulia risasi nyingi bahati nzuri akawahishwa Hospitali akapona.

Akiwa Hospitali akafukuzwa kazi kwa sababu ya Utoro wakati Polisi wenyewe ndo Waliompeleka Hospitali na kumpa PF3.

Hakuna anayemsikiliza. Si Sirro wala Mkuu wake wa Polisi.

MESHACK SAMSON LAIZER NI NANI?

Alikuwa Askari Polisi Arusha Mjini.

Mwaka 2019, Walitembelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Masauni kuzungumza na Askari Polisi na Askari Magereza. Akawataka Askari Watoe Kero zako. Samson akasimama akawataja Askari Pilisi Viongozi wanaofanya Vitendo kinyume cha maadili ya Kiapo chao. Alipoanza kutaja Majina akakatishwa kusema Masauni akataka amtumie majina.

Samson akaandika taarifa ikapokelewa na Kamishina Msaidizi Mwansasu. Likafunguliwa file kwaajili ya Uchunguzi. Wakapatikana Askari 22 kwamba walikuwa wanajihusisha na Vitendo hivyo na Wakahamishwa sehemu mbalimbali.

Baada ya Siku kama 22, nikaitwa na mbele ya Maofisa wa Polisi kumpongeza. RPC Ramadhan Hanje alimuita na kumpongeza kwa Mdomo na akampa kalamu nyeupe na kumwambia Utanikumbuka. Akamuuliza kwanini? Akamjibu wewe nenda tu utakuwa rafiki yangu.

Baada ya hapo alikamatwa na Viongozi wa Polisi Wakaguzi akawekwa Korokoroni siku tatu akateswa sana hadi Figo la kushoto likaharibika sana. Akatengenezewa kesi ya Utovu wa nidhamu, akaambiwa baada ya Saa 24 aende kufuatilia kesi yake.

Polisi Wakaendelea kumuwinda kwa Bunduki hospitali anapofanyiwa Matibabu akawa anajificha. Hadi alipopata namba ya Usalama wa taifa Dar Es Salaam, baadaye Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Masauni akampigia simu akamwambia ameshaongea na RPC Ramadhani. Alipoenda kwa RPC alibambikiziwa Kesi tatu za kutoa lugha chafu lengo likiwa kumnyanyasa sababu kasema Ukweli. Pia wakamvua Cheo chake Corporal.

Baada ya kuendelea kulalamika, tume ikaundwa ikaonekana hana kosa. Baadaye Waziri Lugola akamhamisha RPC kwa kosa la kumnyanyasa askari aliyejitolea kutetea Nchi yake.

Tume baada ya kuona nimeonewa na kunyanyaswa, nikapewa cheo cha Ushujaa cha Sergeant.
1654674951620.png

Baada ya hapo nikaletewa Rushwa Mil 10, kwa sababu alikuwa Askari mwenzangu, nikatoa taarifa TAKUKURU, yule Askari Akafukuzwa. Nikapandishwa tena cheo changu hadi Staff Sergeant. IGP Sirro hakufurahishwa na mi akanipigia simu akasema Hafurahishwi na vile ninavyo fanya na hakufurahishwa na Askari aliyefukuzwa pia" anasema Afande Samson

Akaambiwa aende kusomea Cheo chake. Lakini walimnyima barua ya kwenda kusoma Chuo. Huwezi kwenda nje ya Mkoa bila barua ya Mkuu wako wa kazi lakini akanyimwa barua. Na baadaye ikaripotiwa kwamba amevuliwa vyeo alivyopewa sababu kakataa kwenda kusoma.
1654674770603.png

Meshack Samson Laizer ni askari polisi kutoka mkoa wa Arusha. Askari huyu alipandishwa cheo na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro kwa mamlaka aliyopewa kutoka sajenti (sgt) kuwa stesheni sajenti(ssgt) baada ya kukataa kupokea rushwa ya sh 10,000,000/- .

“Baada ya askari huyo kupandishwa cheo kwa mujibu wa kanuni za Jeshi la Polisi anatakiwa ahudhurie mafunzo ya cheo hicho ili kumjengea uwezo wa kufanya kazi zinazoendana na ngazi ya cheo hicho,ila wakati ulipofika wa kuhudhuria mafunzo hayo kwa mujibu wa tarajtibu alielekezwa kwenda kuhudhuria kozi ya cheo hicho lakini bila sababu zozote za msingi alikataa kufanya hivyo.

Kutokana na utovu huo wa nidamu ambalo ni kosa la kukataa amri halali ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, alishitakiwa kijeshi na akapatikana na hatia na kwa mujibu wa kanuni baada ya kupatikana na hatia inabidi kushushwa ngazi moja ya cheo ambayo ni kutoka stesheni sajenti (Ssgt) kuwa Sajenti wa Polisi na ndivyo ilivyofanyika.

Mkuu wa Jeshi la Polisi ametoa karipio kali kwa askri huyo ikiwa ni hatua za awali wakati hatua zingine zinafuata kutokana na kukiuka sheria,kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi linahitaji askari wanaofuata sheria,wenye nidhamu na wanaofuata kanuni na taratibu za mawasiliano ya ndani na ya nje.” David A. Misime – SACP | Msemaji wa Jeshi la Polisi

Wakaanza kumuwinda ili Wamuue sababu alikataa rushwa ya Mil 10.

Akaenda kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu akaagiza apewe Ulinzi na kifuatilia swala langu.

"Sijawahi lipwa Mshahara unaoendana na cheo changu" anasema Sam.

Alivamiwa Usiku nyumbani kwake na Askari anaowamu wakampiga risasi na kumpiga akaokolewa na Majirani.

Damu zikiww zinamtoka Nyingi Polisi wengine wakaja wakamoeleka Hospital Mount Meru.

Baadaye Polisi wakamfuata Hospital wakamsomea shitaka la Utoro kazini. Baadaye akaja OCD wa Karatu akanisomea hukumu kwamba nimeoatikana na hatia. Baadaye akaja Ssp Almatus Mchunguzi kwamba nimefukuzwa kazi kwa fedheha kwamba nilitoroka jeshini. Wala hawakunipa barua.

Samson Meshack anaomba Waziri wa Mambo ya ndani amsaidie. Na mateso anayo yapata.

Kosa lake ni kufichua matendo mabaya ya jeshi la Polisi anasema Samson
 
Hili ni jukwaa la siasa, vilio vya polisi sio jukwaa hili. Halafu hao viongozi wanaodanganywa tu huwa wanakaa ofisini wakifanya nini?
Punguza Chuki zako.
 
Mimi sikuzote huwa nasema suala lolote la kipolisi huwa hela inatangulia mbele...
Polisi wetu ukiwa huna kosa na ukajidai mjuaji wa sheria basi jua ni rahisi sana kufungwa jela.. Polisi wakipewa chochote na mtu mashtaka yanatengenezwa na unakwenda na maji ukijiona..

Watu wengi wenye makosa huwa wanajidai sana kwakuwa wanajua kucheza vizuri na polisi... Hata uwe na ushahidi wa CCTV.. Mtu kama anawapa chochote.. Huwezi kufungwa... Ukitoa kesi za kisiasa zenye mikono ya wakubwa

Nilishatoa kisanga kimoja.. Jamaa kakamatwa bar usiku saa 8, akapelekwa kituoni akaambiwa una kiasi gani? Akajibu mi sina kosa na sitoi kitu...
Akazamishwa ndani.. Asubuhi akaomba msaada wa mawasiliano kutoka kwa askari ili ndugu zake wajue yupo wapi..
Baada ya masaa mawili ndugu hao.. Akatolewa mahabusu ooh mi sina kosa.. Mara wananionea tuu..
Akaletwa mpelelezi akawaambia ndugu.. Suala la huyu mtu ni kubwa sana.. Subiri kuna askari kutoka makao wanakuja.. Njooni kesho

Usiku akiwa mahabusu akaitwa akaambiwa chagua silaha mojawapo hapo.. (zina vumbi zimetoka store)
Akaambiwa hii silaha ni yako.. na wewe ni jambazi..
Ndugu kuja asubuhi wakapewa info.. Mtu wenu anamiliki gobore.. Na tunajiandaa kumpeleka kwa pilato.

Ndugu walijichanga vya kutosha.. Akatoka...

Funzo askari wetu wapo kimaslai zaidi.. Na hili haliishi leo au kesho..
Bila kutoa chochote.. Unajidai unafuata sheria.. Utakula Mvua za kutosha kimasihara hata kama huna kosa..

Tayari tabia hii imekuwa mfumo rasmi
 
Duuuuh hawa Askari Sina hamu nao hasa hawa wenye division mbovu za form four Wana makasiliko sijapata kuona .

Kwa kifupi Askari wa Tanzania ni zaidi ya majambazi na Mila rushwa namba moja.
Uzuri naamini kila lenye mwanzo na mwisho upo tu.
Atakuja patikana tu kiongozi sahihi wa kuifumua hii sekta na kuifanya ifanye kazi kwa haki.
Na haki ikijaanza kupatikana Askari wengi watadhoofu na kukonda na mistress kibao .
Maana mishahara yao ni kiduchu Sana ndio maana wanaishi kwa ujanja ujanja sana
 
Back
Top Bottom