Kamanda Nzowa ajitokeza, ataja mchungaji anayejihususha na dawa za kulevya

akili ya mtu haipimwi kwa kumuonmekano ni matendo nzowa yeye mwenyewe ndiye anauza na anashirikiana kuuza dawa za kulevya analeta ujinga wake hapa. kama amekamatwa weka ndani na siyo dhamana na kesi hakuna upelezi ni kifungo mmoja kwa moja unampeleka mahakamani kudhibitisha ndio hayo sasa upelelezi ufanyike mbona nchi nyingine ukikamatwa hakuna mjadala ni lupango tu au kifo. nzowa acha usanii weka RA, EL, Karamagi mtoto wa mkulu au unawaongopa?
 
Rais Kikwete alitoa shutuma hizo za viongozi wa dini kujihusisha na biashara ya kulevya mbele ya umati na viongozi wa dini ya katoliki, ningetegemea basi kama kuna hao waliokamatwa wangekuwa wa dini hiyo na sio vinginevyo kwavile ni maaskofu wa kikatoliki ndio wanaoweza kuwapa muongozo wafuasi wao na si wafuasi wa dhehebu jingine!! Huyu aliyetajwa na kamanda Nzowa hakidhi vigezo vya kuwatuhumu wakatoloki kwani dhehebu lake tokea huko Nigeria halimo katika jumuiya ya wakatoliki!! Tunangojea hao wengine wanaochunguzwa pengine shutuma za Rais kwa viongozi wakristo wa TANZANIA zitadhihilika.

Ni bora urejee nukuu za Mheshimiwa Raisi kabla hujatowa tuhuma zako..vinginevyo licha ya kuandika kwa uvchungu mkubwa hoja zako zitaonekana, hazina mashiko na lemavu mno kutumainiwa. Raisi nikweli alitamka maneno yale katika hafla ya dini ya kikristo kwenye dhehebu la kikatoliki. Ufahamu wako na wa wengi humu ni kuwa Raisi waliwakusudia wa Katoliki.

Hii inashangaza. Kabla Nzowa haja taja jina la kiongozi wa dini anaehusika na biashara hii, wakristo wote kwa umoja wao waling'aka na wakisema kama Raisi amewapazia waumini wa Kikristo. Lakini hata magazeti pia yooooote yalinukuu yakitaka Raisi aageuzia kibao wakristo.
Leo Nzowa amemtaja Kiongozi wa dini ya kikristo (ambaye si- Mkatoliki) kuwa amekamatwa na shehena ya kilo 81!!! za madawa then comes again Wakatoliki kama eti Raisi amewataja wao kama wanajihusiha na biashara ya madawa.

Sasa kama hii ndio tafsiri na analysis zetu, basi Tanzania kama Taifa tuna tatizo. Ikiwa kama hawa ndio wasomi watu basi kuna tatizo kubwa zaidi. Ndio maana si siri kuona licha ya wote hawa kusemwa kama ndio wamesoma sana na kutunukiwa shadaza za uzambivu (Dr. degrees), inashagaza!!!
 
Hii apelekewe mkurupukaji Mokiwa, asikae mbali chakula kinaiva majina yatabwangwa pwaaa mbele yake na atakimbia ofisi.

Heshima ulishatupa chooni. Labda hata wakati mwingine humwambia baba yako anakurupuka.
 
Mbona Fundi Maumba aliwahi kukamatwa akivila vitoto vya shule ya Mtendeni na hatujawahi kumsikia huyu jamaa akiwataka Wakw ere waache kuvila witi vitoto!

Kumkamata mjinga mjinga mmoja kwa kosa lake haku-justify kwamba watu wote wa jamii hiyo ni watenda dhambi hiyo.

Na dawa ya Mtendamaovu ni kumkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria hata awe nani na si kuanza kuwatukana na wengine wote waliopo kwenye jamii ile kwamba ni waalifu,

Ni kama vile mfano mnyakyusa akikamatwa na madawa ya kulevya basi kila ukikutana na wanyakyusa unawaambia ninyi wanyakusa nyie mnauza madawa ya kulevya. Matokeo yake wanyakyusa wote sasa wataonekana ni madrug dealer-this is very unfair kwa kweli yaani class nzima unaipaka kinyesi kwa kosa la mmoja au wachache. Presidaa kwanini usiombe radhi tu?
 
Mch. Kuchupu Denis Okechuku ! Huyu ni Mtanzania ? Siwezi kushangaa huenda hata hayupo. Kwanini amtaje badala ya kuwa huyu jamaa rumande?

mkuu, jamaa anafanya kila analoambiwa!! anatapatapa. kakosa kiongozi wa dini anatuletea Okechuku hapa!!
 
Mpaka juzi...Dr. Mokiwa alikua ni mmoja wa viongozi niliokuwa nikiwakubali, umakini wake na uwezo wake wakujieleza. Ni faswaha wa lugha na bila shaka ni mweledi kwenye taaluma na imani yake.

Nimeshtushwa mno na nikiri kama ameni-disapoint sana. Lugha na uslubi alioutumia kuomba ufafanuzi kwa mkuu wa nchi, Raisi imeonyesha dharau ya hali yajuu. Ultimatum aliyoitoa na kumuamuru Raisi afuate matakwa yake imeshangaza wengi. Kama kiongozi mkubwa angeweza kufikisha ujumbe wake na maoni yake nahata maombi yake katika hali ya adabu zaidi na akaeleweka.

Lakini kusema kama '' ikiwa Raisi hataweza kututajia viongozi wa dini wanaohusika na biashara ya madawa ya kulevya....basi tutamdharau na tutaona kama amekurupuka''. Hizi ni kauli za kifedhuli sana kulekezwa kwa kiongozi mkuu wa nchi.

After-all watu wanalazimisha kama mbona mafisadi walitajwa basi na Raisi nae alipaswa wataje hapo viongozi wa dini. Jibu nikuwa JK hajawahi kuwataja mafisadi ila wametajwa na CDM pale Tandika na PCCB kupitia kwenye kesi zinazoendelea.

Kamanda Nzowa leo kupitia Channel Ten amemtaja Mchungaji, mtumishi wa Mungu aliyekamatwa na shehena ya madawa. Kuna watu humu wamesema kama yule si Mtanzania. Jibu nikuwa ni kiongozi wa dini, anaendesha ibada zake Tanzania na wafuasi wake ni wa Tanzania na ameshikwa Tanzania.

Kikwebo.

Ungekuwa na busara ungemueleza Mokiwa maneno haya. Si memba wa JF. Kwa hiyo kutueleza baadhi yetu waumini wake ni kukosea kama wewe unavyodhani amekosea. Eleza hoja yako kunakostahili.
 
Orodha yao ni nyingi
1.okechuku
2.chang
3.mabele
4.obiang
5.obua
6.al muntazir
7............
8.......................
Karibu kamanda nzowa uendeleze list.
 
Subiri orodha inaendelea Mch.Taribo West

na Mch. Sheikidola Omarisegun Obilemehi, huyu ana sura saba zenye jinsia mbili tofauti na paspoti za mataifa mbalimbali, ni jitu la hatari sana! Bado hajakamatwa....popote utakapomuona toa taarifa kwa kamanda nzowa au kituo cha polisi kilicho karibu nawe.
 
Ni kama vile mfano mnyakyusa akikamatwa na madawa ya kulevya basi kila ukikutana na wanyakyusa unawaambia ninyi wanyakusa nyie mnauza madawa ya kulevya. Matokeo yake wanyakyusa wote sasa wataonekana ni madrug dealer-this is very unfair kwa kweli yaani class nzima unaipaka kinyesi kwa kosa la mmoja au wachache. Presidaa kwanini usiombe radhi tu?

Masaa 48 yameshakwisha, sasa tunamdharau, amepoteza uaminifu wake kwetu na tumedhibitisha KIKWETE si mtu makini na mwenye dhamira ya dhati kupambana na madawa ya kulevya.
 
na Mch. Sheikidola Omarisegun Obilemehi, huyu ana sura saba zenye jinsia mbili tofauti na paspoti za mataifa mbalimbali, ni jitu la hatari sana! Bado hajakamatwa....popote utakapomuona toa taarifa kwa kamanda nzowa au kituo cha polisi kilicho karibu nawe.

kwa kwa kwaa.......bwabwabwabwaaaaa!!!
 
Zile shutuma za mtoto wa Mengi kutaka kupandikizwa dawa za kulevya zimeishia wapi?
 
Yeye angesema "kuna watu wana tumia mwanvuli wa dini kufanya biashara ya madawa ya kulevye.." siyo kusema maaskofu wanafanya biashara hiyo.

Jk hana wasaidizi wazuri kwenye upande wa kuandaa hotuba zake, nadhani makosa haya yalikuwa ya wasaidizi wake ndo maana jana kawaambia wajibu wenyewe na police nao wawasaidie kwa kutengeneza mashitaka feki kama hili la kinigeria. Nani asiyejua kuwa wananigeria hutumia dini kufanya vitendo haramu kama hivi. Hata haikuhitaji akili ya ziada kugundua hili badala ya kuchomoka na kuropoka eti maaskofu wanafanya hii biashara.
Jk alikuwa anajaribu kuwatisha hawa viongozi ili wanywee wasimkosoe, maana anatumia kila mbinu kuzuia ukosoaji unaofanywa na viongozi hawa.

Na huyu kamanda anaye tumiwa kusafisha makosa ya bosi wake akibanwa yatamshinda maana kama ni uongo njia yake ni fupi atakamatika mahali fulani na aibu itamkumba, yeye aendelea kutumiwa kama tambala la deki atajiju!
 
Aiseee.. katumwa kutaja? mbona ikulu jana walisema anayejihisi ajitokeze?

By the way hilo jina sio la pande hizi za africa bana..

Acha use...... Nyie si mlijiona mna viongozi wasafi sn, kumbe wanawapoteza nyie wote. Ulijua hawatatajwa eeh! shame on u!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Huu ndio usanii wa WaTz. Mtu ni RAIS wa nchi. Kapewa vyombo vya ulinzi na usalama, Badala ya kuvitumia kuwakamata wahalifu anaenda madhabauni kuhubiri. Kodi zetu ziinapotea bure badala ya kuwaflash wahalifu. Tunatumia nguvu nyingi kupambana na wanasiasa wanaoandamana kuikumbusha serikali wajibu wao na ndio maana ya kuwepo kwa vyama vya siasa. Sasa tuelewe nini kwamba kiongozi wetu anayaogopa majambazi ya unga au vipi. Ingefurahisha kama angehubiri wauzaji wa madawa hayo wakiwa lupango. Wawe wanasiasa, viongozi wa dini hata wengine wote hakuna mtakatifu. Watiwe lupango na ndio kazi ya serikali siyo kulalama.
 
safi sana! hivi neno 'viongozi wa dini' lina-refer dini ya kikristo tu? mbona waislam wapo kimya? au 'huyu ni mwenzetu' inawafanya wanyamaze kimya? dawa za kulevvya ni mbaya sana kwa ustawi wa jamii hasa vijana so lazima ipigwe vita na watu wa dini zote.
 
Kamanda Nzowa wa kikosi cha kuzuia madawa ya kulevya amejitokeza na kumtaja Mch. Kuchupu Denis Okechuku wa kanisa moja la 'kiroho' lililopo maeneo ya Kinondoni Biafra, kuwa ni mmoja wa wachungaji wanaotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya. Amesema akiwa pamoja na watu wengine mchungaji huyo alikamatwa na kilo 81 za cocaine mapema mwaka huu, na kuwa katika pile ya watuhumiwa wa matukio mbalimbali ya madawa ya kulevya, wapo pia viongozi wengine kadhaa wa kidini, ambao watatajwa baadae.

Source; Channel ten (Kipindi cha Baragumu leo asubuhi)
Hapa inaonekana serikali na huyu mkuu wa polisi ni waongo na inaonyesha jinsi wanavyofanya kazi kwa kubahatisha na kuuzia watanzania makesi. Wao wanasema hawana ushahidi sasa huu ushahidi wanaosema hapa wameupata wapi na huyu mtu yuko wapi? Kwa nini kauli zao zinakuwa tata hazieleweki hata rais mwenyewe anaongea hili na wengine wanaongea hili sisi wananchi tuamini lipi. Tunajua ushahidi wanao lakini mapolisi wajanja ndio kazi yao wanalindana. Sasa haya mambo yalihusika vipi na sherehe za huyu Baba Askofu. Haya ni mambo ambayo yalitakiwa kutolewa taarifa wakati hayo madawa yalipo kamatwa. Polisi walishachukua chao na mali walisha uza leo wanatuambia hakuna ushahidi. Tunaomba maaskofu mlivalie njuga mpaka kieleweke. Haya mashudu kama mnakumbuka yalianzia huko Zanzibar kwa kuwapakazia wabara.
 
Ni bora urejee nukuu za Mheshimiwa Raisi kabla hujatowa tuhuma zako..vinginevyo licha ya kuandika kwa uvchungu mkubwa hoja zako zitaonekana, hazina mashiko na lemavu mno kutumainiwa. Raisi nikweli alitamka maneno yale katika hafla ya dini ya kikristo kwenye dhehebu la kikatoliki. Ufahamu wako na wa wengi humu ni kuwa Raisi waliwakusudia wa Katoliki.

Hii inashangaza. Kabla Nzowa haja taja jina la kiongozi wa dini anaehusika na biashara hii, wakristo wote kwa umoja wao waling'aka na wakisema kama Raisi amewapazia waumini wa Kikristo. Lakini hata magazeti pia yooooote yalinukuu yakitaka Raisi aageuzia kibao wakristo.
Leo Nzowa amemtaja Kiongozi wa dini ya kikristo (ambaye si- Mkatoliki) kuwa amekamatwa na shehena ya kilo 81!!! za madawa then comes again Wakatoliki kama eti Raisi amewataja wao kama wanajihusiha na biashara ya madawa.

Sasa kama hii ndio tafsiri na analysis zetu, basi Tanzania kama Taifa tuna tatizo. Ikiwa kama hawa ndio wasomi watu basi kuna tatizo kubwa zaidi. Ndio maana si siri kuona licha ya wote hawa kusemwa kama ndio wamesoma sana na kutunukiwa shadaza za uzambivu (Dr. degrees), inashagaza!!!

Tatizo kubwa ni element za Udini ndizo zinazoimaliza Tanganyika. Kosa aliesema muislam na kawasema wakristo. Sasa ndio revenge hio.

Nawaombea Mola waTanganyika na hizi element za udini , Mola awaepushie muishi kama dugu moja
 
Back
Top Bottom