kamanda mwafirombe

camp konzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2025
Posts
562
Reaction score
1,083
Alikua ni mmoja kati ya asikari wazamani waliopambana vita ya uganda. ili kupona katika uwanja wa vita basi anasema alisababisha mauwaji kwa mamia ya binadamu.

atimae vita ilimalizika na alirudi nyumbani akiwa salama kabisa lakini tangu alejee kutoka vitani alikua amebadilika sana. kwa waliokua wanamfahamu kiundani walikua wakimwambia kuwa amebadilika sana amekuwa ni mtu tofauti kabisa na yule wamwanzo

usiku mmoja akiwa zamu kwenye lindo lake alimuuwa asikari mwenzake aliemfata kwa ajiri ya kuvuta nae sigara kwa kua ndio ilikua tabia yao lakini siku iyo alimchapa risasi na baadae alijitetea kwa kusema kuwa alikua kwenye ndoto nzito kuwa yuko vitani kwenye mapambano mazito na gafla alipofumbua macho aliona mtu mwenye silaa yuko mbele yake kwaiyo alizani bado yuko vitani ndio mana akamchapa risasi

Badae aliachiwa huru lakini aliendelea kusababisha matatizo mengi ya umwagaji wa damu swali ninaojiuliza ni kwamba kamanda mwafirombe alichanganyikiwa akili au mamia ya roho alizozipoteza bado zilikua zikimlilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…