Kwa elimu yangu ndogo niliyonayo, Diploma hawaandiki paper( Reasearch), ingekuwa Advanced Diploma hapo sawa ningekubali. Nina kuwa na wasiwasi kwanza kutokana na masomo ya EGM kule alikoyachukulia,naogopa kusema yawezekana hata hilyo research paper ni magumashi kama hiyo form six, miaka yote hata kabla bosi huyu wa Itikadi ya Chama kongwe hajazaliwa chuo cha Butimba hakijawahi kuwa high school! Mi ni mzaliwa wa mji wa Mwanza nazijua shule zote za sekondari mkoani Mwanza. Butima TCC ni chuo cha ualimu,kilianza kama chuo cha kutoa cheti cha awali na leo hii kinatoa diploma. Nahisi huyu bwana alimaliza Nsumba akaingia kuchukua cheti cha ualimu na cheti chake kikafanyiwa UTAFITI na kuwa kamaliza EGM Butimba TTC ili aingie kivukoni kufanya research ya ordinary diploma. Tanzania tutafika.