Jaman yashafika huko; Nakumbuka wakati TENDWA amemshauri Lema kuomba msamaa watu tulimponda sana humu ndani; na kama haitoshi akaibuka bwana mmoja ambaye pia ni Kiongozi wa wameru pande zile na kusema hakuna Tamko lolote lililotoka labda ni mtu mmoja tu yeye kama yeye kaamua kufunguka na huo uzushi wake ila tu wazee hawakupenda kauli za Mh Lema alizozitoa wakat wa msiba wa Mh Sumari; sasa yamefikaje ya kuandaa PLATOON YA ULINZI hivi hamuoni kama tunaandaa mazingira ya kuraruana sime?
Mungu atuepushe na vita kati ya morani dhidi FFU na Green guard hasa wakati wa kampeni za uchaguzi:lol:
Haya yote ni matunda ya uchochezi wa Tendwa
CDM mnaipeleka wapi Arumeru? Kila mtu akiwa warlord kama Somalia, akawa na wanamgambo wake, na silaha zake, si uchaguzi utageuka chanzo cha vita vya wanamgambo?
Msituletee mambo yenu ya shari, lazima usalama ulindwe na Polisi....full stop!
Mkuu hii ni Tanzania wanayoitaka iwe. By the way, kwa mtu aliyepewa dhamana na title ya u-jaji aropoke vile, unategemea watu wenye kuta 28 za elimu maishani mwao wafanye nini?
Shame on you Tendwa.
Kwa nini Lema pamoja na viongozi wa Chadema wasiombe ulinzi kutoka jeshi la polisi, kwa usalama na mustakabali wa nchi yetu tujiepushe vita vya kikabila ambavyo vitatupeleka pabaya, sio vizuri kulindwa na walinzi wa jadi, tujifunze kutoka Tarime.
Mwaka juzi ni zamani umesahau wale polisi wastaafu akiwemo Yohane walivyoongoza wananchi kuvamia mashamba, kama huamini tukutane kesho Kikatiti uwaone vijana toka Mbuguni wao huwa wanajiita nyoka. Hizi ndizo siasa CCM wanazozitaka.Msitake kutishia Watu nyie,wameru labda miaka ya zamani ndio walikuwa wanawababaisha wanakijiji wenzao,hawana lolote. Nyie ngojeni madume ya CCM yatue huko Kama hao morani went hawakushikishwa ukuta. Hi ndio tatizo la JF,Watu wana mkwara babu kubwa wakati hakuna lolote.
Hizi ndiyo siasa mnazopenda CCM hasa mkiishiwa ushawishi. Police hawana legitimacy kwenye hili, wangetaka kujenga uhalali wao wangemkamata Tendwa na kumwambia awataje wazee waliomwambia watamuua Lema, then operation ingeenda na kuwatia nguvuni wote waliotoa tishio la kuua. Hapo Lema na vijana wangekuwa hawana haja ya kujilinda kwani waliopewa dhamana hiyo kikatiba wanatekeleza wajibu wao.
Mbona 300 ni wachache uki compare na green guard wa ccm, police, usalama wa ccm, tendwa et al? Wangefanya at least 1000 na kuendelea!!
Kwa nini Lema pamoja na viongozi wa Chadema wasiombe ulinzi kutoka jeshi la polisi, kwa usalama na mustakabali wa nchi yetu tujiepushe vita vya kikabila ambavyo vitatupeleka pabaya, sio vizuri kulindwa na walinzi wa jadi, tujifunze kutoka Tarime.
Tusiitane shetani. Tanzania makabila ni mengi na majina au maneno yanaingiliana. Kikwetu NGOROMIKO maana yake ni KIONGOZI WA KIMILA.