Kamanda Kova: Tutamfikisha Halima Mdee mahakamani

Kamanda Kova: Tutamfikisha Halima Mdee mahakamani

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
6,909
Reaction score
4,057
Kamanda Kova amedai atamfikisha mahakamani muda mfupi ujao mwenyekiti wa BAWACHA,Mh. Halima Mdee.

Chanzo: Startv magazeti

My take;

UTII WA SHERIA BILA SHURUTI NI JAMBO JEMA

Viongozi tisa akiwamo Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee, wamekamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay baada ya kufanya maandamano yasiyo halali.

Viongozi hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho (Jumatatu) kwa ajili ya kusomewa mashitaka.

Kukamatwa kwao kulikuja muda mfupi baada ya maandamano yao yaliyoanzia kwenye ofisi za baraza hilo, Kinondoni, jijini Dar es Salaam kuelekea Ikulu kwa lengo la kumwomba Rais Jakaya Kikwete asitie saini Rasimu inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba (BMK).

Hata hivyo, maandamano hayo yalizingirwa na polisi na wote hao kukamatwa pindi walipofika eneo la makaburi ya Kinondoni, maarufu kama makaburi ya FM.

Viongozi wengine waliokamatwa na vyeo vyao kwenye mabado ni Martha Charles (Katibu wa Mdee), Rose Mushi (Diwani Viti Maalum Kinondoni), Edward Simbeye (Mratibu wa Uhamasishaji Baraza la Vijana Chadema,Taifa) na Sophia Phanuel (mlinzi wa Chadema).

Wengine ambao vyeo vyao havijapatikana ni Eauty Mmari, Anna Linjewelle, Remina Peter na Mwanne Kassim.

MAANDAMANO
Maandamano hayo yaliyoanza saa 4.00 asubuhi yakitokea katika ofisi za baraza hilo kuelekea Ikulu, yalikolezwa na mabango yaliyosomeka "Rais usipochukua hatua wananchi tutalazimisha uchukue hatua", lingine lilisomeka "Katiba siyo mali ya CCM" na "Hakuna Katiba isiyolinda rasilimali za taifa" .

Hata hivyo, mita chache tu kutoka ofisini hapo maeneo ya makaburi ya FM Kinondoni, kikosi maalum cha polisi kilichokuwa kimetanda eneo hilo kwa ajili ya kudhibiti maandamano hayo, kiliwatawanya kwa kuwamwagia maji ya kuwasha.

Kufuatia kitendo hicho, Mdee ambaye alikuwa akiongoza maandamano hayo pamoja na viongozi wenzake, walitawanyika kila mmoja na njia yake.

Katika purukushani hizo, Mdee na wenzake kadhaa walikimbilia katika nyumba iliyokuwa mita chache kutoka makao makuu ya Chadema kwa ajili ya kujificha.
Hata hivyo, polisi waliokuwa wamevalia magwanda walivamia nyumba hiyo na kuwatoa.

NIPASHE Jumapili lilishuhudia jeshi hilo likitekeleza kazi yake kwa kumtandika virungu Mdee na wenzake hadi walipopanda gari lao aina ya Defender lililokuwa limeegeshwa eneo hilo tayari kuwafikisha kituo cha polisi.

Pamoja na kuwapiga virungu waandamanaji hao, gazeti hili lilishuhudia uharibifu uliofanywa kwenye kibanda kilichokuwa nje ya nyumba waliyokuwa wamejificha viongozi kwa kuvunjwa na polisi hao.

MKUTANO
Kabla ya viongozi hao kukutana na adha hiyo, walifanya mkutano na waandishi wa habari, ambapo mwenyekiti huyo aliwaeleza kuwa maandamano hayo yameruhusiwa na Rais Kikwete.

Alisema Rais Kikwete amewaalika Ikulu na wanashangaa kwa nini polisi wanawaingilia.

"Tulitoa taarifa siku tatu nyuma, lakini polisi wametujibu jana jioni (juzi), Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Sulemain Kova ametoa sababu kuwa maandamano hayapo kisheria,' alisema.

Mdee alisema kuwa, lengo la maandamano ni kupinga Katiba inayopendekezwa na BMK ambapo vipengele muhimu vimeondolewa.

DEFENDER ZATANDA
Gazeti hili lilishuhudia magari ya polisi aina ya defender yakiwa yametanda eneo hilo majira ya saa 2:00 asubuhi huku askari polisi waliokuwa na silaha aina mbalimbali wakiwa wanazunguka mitaa ya Kinondoni na jirani na ofisi za baraza hilo.

Baadhi ya magari ya polisi yaliyoonekana kurandaranda maeneo hayo ni pamoja na PT 1686 na KX 06 E.

MWITIKIO
Hata hivyo, mwitikio wa wanachama katika maandamano hayo haukuwa mkubwa, huku baadhi ya wananchi wakionekana kukaa pembeni kushuhudia kitakachotokea.

OYSTERBAY POLISI
Baada ya viongozi hao tisa kufikishwa kituoni hapo, baadhi ya wafuasi walifika na kusababisha purukushani kati yao na polisi.

Gazeti hili lilishuhudia eneo la kuingilia kituoni hapo likiwa limefungwa kamba maalum ili kuzuia watu au magari kuingia ndani ya kituo hicho huku polisi wenye silaha za moto wakiwa wameweka ulinzi.

Wafuasi hao waliingia kituoni hapo wakiwa na magari tofauti ambapo walishuka na kuanza kujibizana na polisi.

Kufuatia hali hiyo, defender lililokuwa limebeba maji ya washawasha liliwasili kujiweka tayari na hatua yoyote ambayo ingejitokeza.

Askari aliyetambuliwa kwa jina moja la Tille alitoa maagizo kwa wafuasi hao waondoke eneo hilo, huku akiwafuata waandishi wa habari waliokuwa wamejitenga na kundi hilo na kuwataka waelekee walikotaka wana-Chadema waende.

Hata hivyo, kitendo hicho kilipingwa na askari mwingine ambaye alisema waandishi wa habari wanafanya kazi pamoja nao, hivyo sio vyema kuelekea huko kwa kuwa ni eneo hatari.

Baada ya wafuasi hao kutii amri hiyo walikaa upande wa pili wa barabara ya Ali Hassan Mwinyi na kuimba nyimbo mbalimbali huku wakiigiza jinsi askari wanavyotembea wakiwa kwenye gwaride.

Katibu wa Chadema Mkoa Kinondoni, Henry Kileo, alitoka ofisi za kituo hicho na kuwaeleza wafuasi hao kuwa, mpaka muda huo (saa 7:40 mchana), Mdee na wenzake walikuwa wamekataa kuhojiwa hadi mawakili au ndugu wa karibu watakapofika kituoni hapo. Hatimaye wakili Peter Kibatara, aliwasili kituoni hapo.

POLISI WAONGEA
Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi, Simon Siro, alithibitisha kukamatwa kwa viongozi tisa na kueleza kuwa baada ya mahojiano waliachiwa kwa dhamana.

Aidha alisema watafikishwa mahakamani kesho kwa kosa la kufanya maandamano yasio halali.

SOURCE:NIPASHE
 
CCM ruksa kufanya mkutano, CDM hapana sababu mnawambumburua wananchi kuhusu katiba mpya.
 
Huyu Kova ni kichaa mwingine. Ebu atuambie kama kuna mtu yeyote aliyewahi kushtakiwa kwa kuandamana aliwahi kufungwa au hata kupigwa faini. Ni upuuzi mtupu.
 
Kwa sera za Maandamano CHADEMA wanaongoza!.

CHADEMA hawana agenda mbadala za kitaifa zitakazo waweka machoni mwa wananchi wengi, kwa sasa wanachofanya ni kutafuta attention kwa njia zozote.

Who cares about BAWACHA.

Halima Mdee na BAWACHA yake anadhani style ya maandamano yasiyopata go ahead ya polisi BAWACHA watapata positive coverage.
 
Hivi mkuu kova huna mambo mengine ya kufuatilia ? Kwanini usihangaike na majambazi wanaopora kwa kutumia pikipiki za boxer wanaotamba jiji zima ?
 
Kwa sera za Maandamano CHADEMA wanaongoza!.

CHADEMA hawana agenda mbadala za kitaifa zitakazo waweka machoni mwa wananchi wengi, kwa sasa wanachofanya ni kutafuta attention kwa njia zozote.

Who cares about BAWACHA.

Halima Mdee anadhani style ya maandamano yasiyopata go ahead ya polisi BAWACHA watapata positive coverage.

CHAMA CHA SIASA ni MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE , MY TAKE - MAANDAMANO YA KINANA HUYAONI ?
 
Nashangaa mapolisi wa kitanzoo!maandamano ni kazi njia mojawapo ya chama chochote cha siasa kutoa maoni yake.Na ni haki ya kikatiba.Naona mnapoteza muda.Na mnawajenga chadema bila kujua maana si tunaona ccm wanaendelea na maandamano na mikutano ila chadema no no.....tunajua tatizo sio polisi ni ccm maana mnatumika tu.
 
Kwa sera za Maandamano CHADEMA wanaongoza!.CHADEMA hawana agenda mbadala za kitaifa zitakazo waweka machoni mwa wananchi wengi, kwa sasa wanachofanya ni kutafuta attention kwa njia zozote.Who cares about BAWACHA.Halima Mdee na BAWACHA yake anadhani style ya maandamano yasiyopata go ahead ya polisi BAWACHA watapata positive coverage.
Unadhani lini CHADEMA watapata go ahead ya police? Uoga wote mlionao mnaposikia maandamano ya CDM kamwe hamuezi kukubali! (Mkisikia tu mnafikiri ya Tunisia yanakuja) hebu jiulize kidogo, walimu jana waliandamana tena wakiwa na mabango, polisi waliwafanya nini? Au Kinana juzi alipoongoza maandamano Tanga alikuwa anatafuta attention ya nani? Au tuseme kuandamana gani kuliko halali? Mngekuwa na uwezo hata mikutano ya hadhara mngeizuia, maana inaenda sambasamba na kupotea kwenu kwenye medani za siasa hapa nchini. Poleni sana, mabadiliko hayajawahi na wala hayatowahi kuzuiliwa na yeyote!
 
Kwa sera za Maandamano CHADEMA wanaongoza!.

CHADEMA hawana agenda mbadala za kitaifa zitakazo waweka machoni mwa wananchi wengi, kwa sasa wanachofanya ni kutafuta attention kwa njia zozote.

Who cares about BAWACHA.

Halima Mdee na BAWACHA yake anadhani style ya maandamano yasiyopata go ahead ya polisi BAWACHA watapata positive coverage.

Hujitambui
 
Kova ni mshikaj wangu sn.....! Nikiwa naye pale kijiweni lazma nimuulize km ana ujasiri au kazeeka....tena nitamtafuta pia swahiba yangu Mzee Tibaigana kifuba kyaitawa atoe UZOEFU alioutoa philedephia kwenye kozi yake mwaka 1997.
 
Yaani chadema sera zao mbovu mbovu tu, kuhujumu maendeleo, kuandamana, kuongea uongo ktk media, uchochezi, uvunjifu ea amani and so hiki siyo chama kabisa badala kijenge hoja na kuwa mfano kwa chama tawala wao ndiyo wana beza na kuhukumu maendeleo.
 
Atamshitaki kwa kosa gani?

Ni sheria gani inawapa polisi mamlaka ya kutoa vibali vya maandamano?

Maandamano ya wale akina mama yalikuwa yanahatarisha nini kwa nani?

Walikuwa na silaha gani hadi polisi watumie mabavu namna ile?

Hiyo sheir ina apply kwa CDM tu?

Mbona ccm wanaandamana kila siku bila kizuizi?

Tanzania ni ya Watanzania, si ya kinana wala ccm.

Binadamu akichoka anabadilika.
 
Back
Top Bottom