Kamanda Kova asilaumiwe!

Unajua huyu Msangi ni kama keshakufa.
Maneno yetu watanzania na sala zetu zishamuua mara zaidi ya mia.
Kabaki kama zombie tu
 
Ulimboka alisema Msangi alikuwepo ?

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
mkuu ndo lile sakata la James Isame?Usishangae ndiyo maana polisi wengi wakishastaafu maisha yao huwa yanakuwa ya dhiki sana sababu ya laana mbalimbali wanazokuwa wamekusanya
 
Ngoja Dr Ulimboka arudi,kwanza alitakiwa atoe taarifa kwa mwanasheria wake kushinikiza mtuhumiwa aliyetambuliwa akamatwe.However sidhani kama it will be possible,labda kama ccm itaondolewa madarakani.
 
Mkamateni ahmed msangi-Ngwajima
Mkenya hawezi kuja kutubu kwangu kwa nini asiende kwenye kanisa lake- Ngwajima
 
Hofu yangu ni ukanjanja,usanii,magumashi ya Kova yasije kuteletea matatizo ya Kidiplomasia na Kenya nchi jirani,kashawapakazia kwamba wana kundi hatari linajiita Gangstar

Tusubiri kauli ya Kenya, Fikra kwamba majambazi sugu ni wakenya
 


Duuuuuu!, Poleni saana kwa mtendwa. Too bad
 
Nawashauri maaskari wote anaowaongoza wamsuse!
 

wametudanganya na wanajua kwamba wametudanganya, haina haja ya kujiuliza yote hayo
 
Nchi za wenzetu baada ya tukio wangechukua DNA ambazo zilikuwepo kwenye nguo za Dr. na alama za vidole ambazo zingesaidia kubaini kama Joshua alihusika. Sasa kwa vile hatuna utaalamu huo, tutabaki na labda!
 
Pia na mimi nakumbuka wameshawahi kunikuta mtaani, wakadai ni mzurulaji, waliniomba rushwa nikakataa, wakasema twende kituoni, kwa kuwa nilijiamini sikuwa na tatizo lolote nikawambia twendeni, kama hatua mia moja kufika kituoni wakaniambia haya shika bangi yako, nikashtuka!, ikabidi niwape tu buku 10 ili nisije swekwa rumande, na tatizo kubwa ni kwamba jamhuri inadai polisi haongopi, tafakari sasa ni watanzania wangapi wanaobambikiwa kesi kwa kukataa kuwapatia kitu kidogo.
 

Jakubumba,

Ni kweli polisi wa Tanzania wana Tabia ya kuwataka watu wawapelekee ushahidi and this can only happen in Tanzania. Akina Kova wamwkulia kule Police lines pale Moshi. Ni matunda ya polisi kurithisha kazi watoto wao.

Elimu Yao wengi ni ya kuungaunga. Most have IQ below normal.

Kuhusu kuweka kichwa kwenye guest house ya Baba yako hiyo ni Vandetta! Chacha ana Tabia ya mazishi huwa halipi watu kwenye deals au wanazokubaliana na watu kwa hiyo imefanyika ili kumtesa. Itabidi wapeni polisi rushwa ya kutosha watawaambia nani kasuka hilo Dili.
 
Huyu KOVA, MWIGULU, CHILIGATI n.k wanatoka mahala kumoja.........sitaki kuamini kuwa watu wote wa huko wako hivi
 

BIG SHAME!!!!! Hiki ni kituko na ni aibu kwa waliompa madaraka Kamanda Kova. Inakuwaje ishu tete kama hii unathubutu kukurupuka na kutoa maelezo ambayo hayana utafiti wa kuaminika?

Sioni sababu inayosababisha kamanda kova apate usongo wa tatizo hili kiasi hiki, wanaweza kutokea watu kumi waliohongwa ili kudhoofisha upelelezi na kudai kuwa ni wahusika wa tukio je atakubaliana nao tu bila kujua undani wa taarifa wanazotoa?

Watu wa aina ya kova ndiyo wanaosababisha serikali ionekane ina tatizo, katika karne hii yenye watu wenye elimu na uelewa wa kutosha ukimkuta mtu mzima anadhani anaweza kuwahadaa watu hivihivi hicho ni kichekesho!!! kwa hali ya kawaida tu kama kweli mtu aliyejitambulisha kuwa ni mmojawao wa waliomshambulia Dk Ulimboka amekamatwa, shahidi wengine wa uhakika ni kanisa la Ufufuo je kamanda Kova nao amewaunganisha kwenye watu muhimu wa kutoa ushahidi?
 

tuko pamoja mkuu. Sidhani kama kova amefanya analysis ya kutosha juu ya athali ya kauli yake. Yaani kuhusisha utekaji wa ulimboka na huyo mkenya na pia kanisa kwa upande mwingine. Kwangu mimi naona kuna implication mbaya kwani katika harakati tunazoendelea nazo za ushirikiano-eac- naona kama ni tatizo kubwa. Kwani kova anataka tuanze kuwaona makenya ni watu hatari na wasiofaa kuwanao katika jamii. Kwa mtu makini na aliyeenda shule huhitaji nusu saa kujua kuwa alichokisema kova ni uongo. Nilikuwa sifahamu upeo wa kufikiri wa kova pengine na watalaam wengine wa jeshi letu la polisi, sasa nimefahamu kuwa hatuna polisi makini. Alichokifanya kova na waandamizi wake kinadhalilisha jeshi zima la polisi kuwa ni watu ambao pengine wanafikiri kwa kutumia maka...kwangu mimi naona hapo ndo walikaa na kuona wakisema hivyo watanzania wataamini. Duuuuu...maskini kova sijui karogwa?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…