Kamanda Halima Mdee kutikisa Bukoba Mjini leo

Kamanda Halima Mdee kutikisa Bukoba Mjini leo

Umeona eeeeeh huo ndo ufa ambao CCM atapitia
HISTORIA YA KURA ZA URAIS TANZANIA 1995 - 2010
Mwaka 1995 jumla ya kura za wapinzani zilikuwa 2,486,323, sawa na asilimia 38.17. Uchaguzi uliofuata wa mwaka 2000 wapinzani walipata jumla ya kura 2,309,123, sawa na asilimia 28.26 na kupungua zaidi mwaka 2005 walipopata kura 2,241,525 (sawa na asilimia 19.72. Mwaka 2010, upinzani ulipata kura 3,121,136. Ingawa kwa asilimia, kura hizo zilikuwa asilimia 37.16 pungufu ya asilimia za uchaguzi wa 1995, idadi ya kura za wapinzani ilikuwa kubwa kwa tofauti ya zaidi ya kura 700,000.

Kwa trend hiyo mwaka 2015 upinzani watashuka tena kwa takribani asilimia 13 au 11 kutokana na vurugu zilizosheheni katika chama cha Chadema na CUF. Zitto Kabwe na kundi lake na Hamad Rashid na kundile wote hawa watasababisha negative performance ktk matokeo ya ubunge na urais.

MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA! KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Fanya mambo mdee tunaweza kubadilika waambie wana bukoba waache uccm, waangalie maendeleo ya mji wetu na waache malumbano yasiyo na tija. big up mdee! chadema mwanzo mwisho mpaka kieleweke!
 
Siyo siri CCM bado imara ila kwa spidi aliyoanza nayo Madame Halima Mdee baada ya kuchaguliwa mwenyekiti wa BAWACHA ni kali mno. Mwaka 2015 siyo ajabu UKAWA ukashinda uchaguzi mkuu,
 
Last edited by a moderator:
Bukoba ni wasomi, hawawezi.kukubali kuburuzwa na vilaza chadema

Kama Halima ameweza kukusanya akina mama wa kihaya wengi kiasi hicho na akawakalisha kitako kumsikiliza,hakika watu wameichoka ccm!!!
laki si pesa kama huamini katika mabadiliko anza kuamini sasa mkuu nilikuwa bukoba kwenye biashara zangu kila kijiwe walikuwa wanaongea story za mdee mdee tu,sijui kihaya ila nilikuwa nasikia jina tu mdee mdee....
__kazi ipo kazi ipo kwa ccm
 
Last edited by a moderator:
HISTORIA YA KURA ZA URAIS TANZANIA 1995 - 2010
Mwaka 1995 jumla ya kura za wapinzani zilikuwa 2,486,323, sawa na asilimia 38.17. Uchaguzi uliofuata wa mwaka 2000 wapinzani walipata jumla ya kura 2,309,123, sawa na asilimia 28.26 na kupungua zaidi mwaka 2005 walipopata kura 2,241,525 (sawa na asilimia 19.72. Mwaka 2010, upinzani ulipata kura 3,121,136. Ingawa kwa asilimia, kura hizo zilikuwa asilimia 37.16 pungufu ya asilimia za uchaguzi wa 1995, idadi ya kura za wapinzani ilikuwa kubwa kwa tofauti ya zaidi ya kura 700,000.

Kwa trend hiyo mwaka 2015 upinzani watashuka tena kwa takribani asilimia 13 au 11 kutokana na vurugu zilizosheheni katika chama cha Chadema na CUF. Zitto Kabwe na kundi lake na Hamad Rashid na kundile wote hawa watasababisha negative performance ktk matokeo ya ubunge na urais.

MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA! KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Uchambuzi wako ni dhaifu sana, hauna mashiko. Kama ungekuwa unafuatilia kwa karibu mnyambuliko wa kisiasa nchini usingekuja na simple analysisi kama hiyo. Kumbuka kuwa kila wakati una mambo yake na watu wake. Kwa Tanzania 'determination ya matokeo ni zaidi ya balot box!!! Kwa Mfano rejea idadi ya watu waliojiandikisha kuwa ni zaidi ya Miliono 18 na waliopiga ni chini ya Milioni 10. Swali dogo: Nini kitatokea iwapo watu zaidi ya Milioni 15 watajitokeza kupiga kura? MACHO SIO KWA AJILI YA KUONA TU, ni KUSAIDIA KUTAMBUA UKWELI NA KUUFANYIA KAZI!!
 
Nafarijika sana ninapoona mama zangu wakiwa mstari wa mbele kuusaka ukombozi wa pili! Big up sana akina mama wa Bukoba!
 
Hongera kwa wanawake wa CHADEMA kwa uamuzi sahihi wa kumchagua Mdee
 
B1K341zCMAA_TJx.jpg

Bila shaka hawa kina Mama walifika katika mkutano wa Mdee bila kubebwa na Malori,bila kuwepo wasanii wa kutumbuiza mkutano....walichofuata ni ujumbe na si vinginevyo.
 
Wadau,
Pamoja na sekeseke dhidi ya polisi aliyokutana nayo kamanda Mdee m/kiti wa BAWACHA tatifa na timu yake leo wanaendelea kutimua vumbi mkoani Kagera na sasa wako Bukoba mjini tiyari kuwasha moto katika viwanja vya Uhuru maarufu kama viwanja vya Mayunga.

Shamlashamla za kumpokea Mdee zimeanza mapema asubuhi,huku katika vijiwe mbalimbali watu wakitathimini na kupongeza uwezo wa CHADEMA wa kutengeneza wanasiasa wazuri.Hasa wakizingatia jinsi Mdee alivyoyatikisa magamba na polisi wake kote alikopita.

Wadau tutaendelea kuwajuza yanayoendelea na walioko karibu,karibu tuhudhulie kwa wingi.

B1K6ipuIYAAq_3P.jpg

B1K341zCMAA_TJx.jpg
Eee bhana hii nyomi mbona balaa!!!
 
B1K341zCMAA_TJx.jpg

Bila shaka hawa kina Mama walifika katika mkutano wa Mdee bila kubebwa na Malori,bila kuwepo wasanii wa kutumbuiza mkutano....walichofuata ni ujumbe na si vinginevyo.
Sasa nimejua kwanini polisi wanazuia mikutano ya Mh Halima Mdee .
 
Kwa mara ya kwanza nashukudia wanawake wengi wakihudhuria mikutano ya vyama vya upinzani maana mara nyingi wanaoonekana ni vijana tu. Bravo Halima Mdee
 
Kwa mara ya kwanza
nashukudia wanawake wengi wakihudhuria mikutano ya vyama vya upinzani
maana mara nyingi wanaoonekana ni vijana tu. Bravo Halima Mdee

mkuu, kwa bukoba ni kawaida..hii inatokana na kazi nzuri ya mama conchesta Rwamlaza, amefanya kazi kubwa sana kuwahamasisha wanawake jimboni kwake
 
Back
Top Bottom